Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Huu ni utaratibu wa kawaida katika kufanya ukaguzi wa matumizi, au taratibu za ujenzi. Kwamba mkaguzi ataibua hoja ya kuwa na wasiwasi juu ya anachokagua pale panapotokea kuwa hakuna vielelezo vya kile anachohoji ili kuthibitisha. Hivyo baada ya kuibua hoja hizo majibu ya uhakika huwa yanahitajika.
Mfano mkaguzi anakagua juu ya manunuzi ya sare za jeshi la polisi, lazima aulizie risiti za manunuzi, usafiri na ikiwezekana aone hizo sare. Asipoziona hapo ndipo huibua hoja ambazo huhitaji majibu.
Kwa hiyo kama CAG ameibua Audit queries sio conclusion kuwa tayari kuna ufisadi. Maana lazima PAC au LAAC watafute majibu ya hizi hoja ili tujue ukweli wake.
Hivyo wanasiasa wapenda sifa kama Zitto wasitumie nafasi hii kupotosha umma kuwa tayari kuna ufisadi.
Mmesahau ishu ya tril 1.5 ambayo ilikuja kupata majibu? Mbona Assad hadi hii leo na hasira zake za kufukuzwa uCAG hajaikumbushia kama kweli zilipigwa.
Tusubiri majibu ya PAC ka LAAC.