Watanzania msipotoshwe na hoja za kiukaguzi (Audit queries) maana sio hitimisho kuwa ni ufisadi, zikipatiwa majibu ukweli hujulikana

Usiwe unanitumia video za propaganda!Tumia wajinga wenzako ambao hawajua political science.Hakuna kiongozi ambae alitengeneza miradi mingi na imara ndani ya muda mfupi katika historia kuliko Hitler.

Miradi ambayo kwa uongozi wa leo wa Ujerumani itachukua miaka 30 kutengenezwa Hitler alitengeneza miradi hiyo kwa miaka mitatu tu, lakini leo hii katika historia ya dunia hakuna kiongozi ambae anaonekana wa ovyo, katili,hafai na ambae historia inamhukumu kama Hitler. Uongozi siyo kujenga miradi.
 
Kama aliyetoa hiyo report ni mteule wa rais na ana haki zote na ni mbobevu wa hiyo shughuli sisi watanzania ni kina nani hadi tumpinge?

Tunaendelea kumuamini CAG mwanzo mwisho kuwa kuna ufisadi wa kufa mtu katika nchi ambayo tulikuwa tunaambiwa kwa ni ya wasafi na malaika.
 
Hii ni awamu ya 6 kwa mujibu wa mama yetu kipenzi cha watanzania mh Samia.

Hutaki kuukubali ukweli basi hama nchi urudi kwenu burundi tuwachie tanzania yetu ikiwa salama na yenye mshikamano.
 
kabla ya auditor hajaandaa ripoti ya mwisho huwa anawapa management team queries alizozibaini ili apewe majibu, management isipotoa majibu ya kuridhisha ndipo auditor hutoa ripoti yake ya mwisho na ndicho CAG alichofanya, hayo majibu yako ni ya wapi tena ? walishashindwa kutoa majibu ndio maana CAG katoa ripoti yake kama ilivyo.
 
Mleta mada naomba nitofautiane na wewe kidogo

Kikawaida auditor huwa anakagua na kabla hajafunga ukaguzi wake anawatumia wahusika management letter ili wajibu hoja zote ambazo auditor amezitoa ikiwemo kutoa vidhibiti..risiti au uthibitisho wa hoja yoyote ambayo wahusika wanadhani ushahidi upo au kulikuwa kuna namna nyingine ya kukabiliana na hoja aliyoitoa auditor

Mbali na hapo pia kuna kitu kinaitwa exit meeting ambapo auditor hutoa majumuisho ya hoja zake kwa wahusika ili kama na wao wanahoja mbadala basi wanaziwasilisha

Mpaka hoja ikitokea kwenye report ya auditor maana yake haikupata majibu mujarabu kutoka kwa wahusika na katika mantiki hiyo kinachofuatia hapo sasa ni uchunguzi au mamlaka husika kuchukua hatua za kisheria au kinidhamu

Ndio maana kwenye baadhi ya maeneo auditor anashauri mamlaka husika kuchukua hatua kwa wahusika ikimaanisha walishindwa kwa namna moja ama nyengine kutoa ushahidi wa jambo ambalo auditor aliliibua kwamba liko kinyume na mahesabu
 
Acheni utetezi wa kifala.
Mpaka CAG ahitimishe na kuwasilisha ripoti ya yatokanayo na ukaguzi, huwa wameshatoa muda wa kutosha kwa wakaguliwa kutoa majibu ya hoja mbalimbali zilizijitokeza kwenye ukaguzi.
 
Ass! Utamkumbuka sana Hayati Magufuli alikunyoosha kwelikweli mpaka unaingia kaburini utakuwa unamkumbuka tuuu!! Chezea Rais Magufuli wewe!! Hacheki na wizi na wauza madawa ya kulevya na mbaya zaidi Rais Mama Samia naye amesema Kazi Inaendelea sasa sijui utakimbilia wapi!!
 
Nani asikilize mazombie ya Jiwe?pumbafu yaani mim nianze kukusikiliza ww mpiga zumari wa jiwe?
Lazima unyooke tu na Rais Mama Samia ameshasema Kazi Inaendelea sijui sasa utakimbilia wapi! Moto ni ule ule utawachoma sana tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…