Watanzania Mungu atupe nini, hata wana wa Israel aliwaacha

OTTER

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
476
Reaction score
330
Tumshukuru mungu kwa kila jambo. Mwenyezi mungu hawezi kukupa kila kitu. Unaweza ukakufuru kwa baadae.

Mungu katupa amani, maliasili ambayo Tanzania ni nchi ya pili duaniani kuwa na maliasili tuzionazo. Katuondolea korona, nzige hivyo vyote hatushukuru tuu.

Sasa ameona ni vyema atunyime ujuzi wa kusakata kabumbu. Tutaendelea kupigwa hadi akili itukae. Mwache mungu aitwe mungu
 
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ fala
 
Umekiri kucheza mpira ni ujuzi..Sasa ujuzi si unafundishwa? Mungu anahusikaje hapo?
 
Tatizo ni kudanganyana na kushikiwa vichwa vyetu kuwa ni kweli hakuna Corona, ni mabingwa wa siasa, kabumbu na hata ndondi siku tuukitandikwa tumeonewa
 
Umekiri kucheza mpira ni ujuzi..Sasa ujuzi si unafundishwa? Mungu anahusikaje hapo?
Mkuu mbona tuna makocha waliobobea kwenye kabumbu lakini bado tuna tandikwa za uso? yawezekana mpira kwa wanaume ushatuacha, tuhamie kwa wakina mama maana ndiyo wanaiwakilisha vyema nchi yetu
 
Mkuu mbona tuna makocha waliobobea kwenye kabumbu lakini bado tuna tandikwa za uso? yawezekana mpira kwa wanaume ushatuacha, tuhamie kwa wakina mama maana ndiyo wanaiwakilisha vyema nchi yetu
Ni hivi kuwa na ujuzi wa kucheza mpira hakuna tofauti na kuwa daktari, engineer, n.k kwa maana huwezi kuruka hatua iliyopangwa na watalaam na ukawa ni daktari au engineer.

Lecturer kupelekewa wanafunzi waliomaliza shule za msingi kwamba awafundishe wawe maengineer au daktari wakati wameruka hatua kamwe husitegemee kupata ufanisi bora kutoka kwa wahitimu.
Kucheza mpira ni zaidi ya kujua control, kupasia na chenga. Vitu kama nidhamu (ndani na nje ya uwanja),umakini, stamina na kuju mifumo ya soka (formations) n.k ni muhimu sana kwa mchezaji kuwa navyo. Wenzetu washajua ili mchezaji awe navyo ni muhimu zaidi aanze kufundishwa akiwa mdogo na
hapa ndipo tunaporuka.

Hata aje pochettino hatuwezi kuwa na timu bora maana tutampa wachezaji wale wale ambao hawana misingi sahihi ya soka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…