Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Ujio wa ukoloni umeathiri sana mwenendo mzima wa hali ya afya kwa Waafrika wengi. Mojawapo wa athari za ujio huu ni kupandikizwa katika akili za Waafrika dhana kuwa kila kitu kilicho cha asili ni kibaya na hakina budi kuachwa. Kwa mfano chakula cha asili, nyumba za asili, mavazi ya asili, dawa za asili na hata tabia na mienendo ya asili.
Kwa kuambiwa kuwa kilicho na asili ya Waafrika ni kibaya, tumelazimika kutumia kila kinachotoka ngambo tukidhani ni bora kumbe sivyo.
Kwa mfano, tumeacha kutumia unga wa dona na kupendelea kula sembe. Tumeacha kula magimbi na viazi vikuu vinavyopikwa kwa kuchemshwa au kuchomwa na kukimbilia kula chipsi za viazi mviringo zinazotayarishwa kwa kukaangwa kwa mafuta yenye lehemu. Tumeacha kula vyakula vya mchemsho na kupendelea vya kukaangwa na kutumia chumvi nyingi ya mezani (table salt) na kadhalika.
Mitindo hii ya maisha imesababisha watu wengi kupata maradhi kama presha (BP), kisukari, gaut, vidonda vya tumbo, n.k. Waathirika wakubwa ni wale wenye umri wa miaka 35 hadi 50 ambao ndiyo wenye kushika hatamu za uongozi kwa nchi yetu katika siasa, elimu , uchumi na ujenzi. Tiba iliyopo ni kwa matumizi ya dawa za kisasa ama kwa njia ya vidonge au vimiminika. Dawa hizi huitengenezwa katika maabara kwa kutumia kemikali za aina mbalimbali.
Tiba asilia zimeachwa kwa kupigwa vita na wakoloni na mabeberu na hivi sasa serikali imepiga vita dawa hizi hadi zipimwe kwenye maabara na kupata ithibati kama zinafaa. Kwa kiasi kikubwa tiba asilia imesahaulika. Kwa mfano matumizi ya dawa za asili zilizokuwa zikitibu maradhi kama malaria, vidonda vya tumbo, kichomi na pia maradhi ya tumbo na ya ngozi, n.k. hazitumiki tena.
Badala yake tunatumia dawa za kisasa zenye kemikali. Kemikali hizi zimeonekana kuwa na madhara kwa kusababisha magonjwa mengine kwenye utumbo mpana na mwembamba, tumbo, figo, ini na nyingine kuleta usugu na pia mzio.
Nchi zinazopiga vita madhara yaletwayo na dawa zenye kemikali ni Marekani, China, DPRK na India.
Nimegusia kuwa nchi ya Marekani iko mstari wa mbele kwa kuacha kwa kiwango fulani kutumia dawa zenye kemikali ili kulinusuru taifa lao kutokana na madhara ya matumizi ya dawa hizo.
Kampuni inayoongoza kutengeneza dawa zinazotumia mimea ya asili ni GNLD kutoka Marekani.
Dawa hizi zinatibu maradhi ya ngozi (Nutriance skin care), kuimarisha usafi nyumbani kama chooni, bafuni, jikoni na pia sakafuni ( LDC, LC 30, Golden Home Care, n.k.), kwa kungarisha ngozi zetu (Nutriance Skin Care) na pia kwa kutumia mbolea kwenye bustani zetu na pia mashambani (Super Grow).
Mwanzilishi wa kampuni ambayo ilijishughulisha na ugunduzi wa matumizi ya dawa, lishe na mbolea kwa mashamba yetu zinazotokana na mimea ni Jerry Brassfield. Yeye anasema kuwa kwa kutumia mimea kama majani, mizizi, magamba ya miti, n.k. inawezekana kupata vidonge, vimiminika na pia ungaunga kama poda.
Mafanikio yake yalianza alipokuwa na umri madogo alipokuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu pamoja na mzio (allergy). Hakupona kwa dawa za hospitalini hivyo mama yake alikuwa akimwongezea lishe kwenye chakula pamoja na kula chakula cha nafaka kamili (isiyokobolewa).
Hatua hii ilibadilisha afya yake na ukali wa maradhi ukapungua.