The golden
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 1,382
- 2,582
Du!Mashabiki wa mpira unaowaona kama wameingiwa na kichaa ni kwa sababu wanakuwa wameweka mikeka,wamebeti.Hawawezi kulala mpaka waone hatima ya mikeka yao.
Yaani......Watanzania ni viumbe hai wa ajabu sana duniani, hawana umeme na maji pia vyakula vinapanda bei kila leo ila wao wapo bize na ushabiki wa mipira, ndio maana maisha yanazidi kuwa magumu tu. Wanasahau mambo ya msingi wanajadili mambo mepesi sana.
Maisha waliyoyachagua ndio hayo. Au wewe ulitaka wafanye kitu gani ndio useme wanapigania maisha? Wamechagua hivyo, nawe uchague vile, jambo la msingi isivunjwe sheria ya mamlaka. Maisha ni furaha, kama mtu ameona furaha yake ataipata kupitia mpira, muziki au mapenzi, acha apiganie hilo, na kama wewe umeona furaha yako ni kutafuta hela, shikilia hapo hapo usiangalie wala kulazimisha mwingineWatu wamejitolea kwa jasho na damu kupigania mpira kuliko hata maisha yao wenyewe. Kama binadamu jitahidi sana kuhimili mihemko ya mambo ya dunia hii.