Watanzania na kufurahia vifo vya wanasiasa, ja watawala wanajisikiaje?

Mudawote

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
11,612
Reaction score
16,189
GTs,

Naomba niandike kidogo sana.

Kipindi anafariki Dkt Magufuli wengine tuliumia na kulia wengine walishangilia na kufanya sherehe.

Mi nilichojifunza ukiwa shabiki wa mwanasiasa basi sikiliza watu wanasemaje then mshauri kiongozi wako hivyo hivyi kiuchawa asikilize watu maana akifa utasikitika peke yako wenzako wanashangilia na kunywa na kula nyama kama yaliyotupata sisi chawa wa Dkt Magufuli.

Je mwana JF upo upande gani?
 
Mudawote,

Tulikuwa wazalendo. Tulikubali kazi, kauli zake. Zilikuwa za kujenga Taifa.
 
Mudawote,

Tulikuwa wazalendo. Tulikubali kazi, kauli zake. Zilikuwa za kujenga Taifa.
Sana kwa kweli Dkt Magufuli alitujengea umoja sana. Tatizo lake tu ilikuwa ukali wa kupitiliza matokeo yake wasaidizi wake wakatafasiri kila rais akimlalamikia mtu wanamteka hahaha naona ni kama sasa hivi sina hakika kama Dkt Samia anaagiza ila akina gewra wanaagiza ua teka hahah bila yeye kujua halafu wanamjaza upepo
 
Sasa hivi ukipita kwenye mitandao ya kijamii utagundua kuwa Kuna ombwe kubwa la upendo miongoni mwa watanzania, yawezekana mambo yanayofanywa na kundi fulan la watu yanachukiza zaidi wananchi ila wanaogopa kusema
Sasa hivi si ajabu mtu fulan akipata tatizo comments nyingi zinakuwa ni za kufurahia na kumdhihaki kuliko pole anazopokea
Ndg zangu turudi nyuma tujiulize ni wapi tulipokosea Kisha tujirekebishe
 
Hakuwa mkali. Alikuwa sahihi sana kuongea na hili Taifa, kwa mazingira yake, kulikomboa Taifa. kuliko kiongozi yoyote.
 
Walioshangilia wengi waliumizwa na policy zake moja kwa moja au sio moja kwa moja kupitia watendaji wake.

Wapo waliopendelewa na wapo walioonewa.

Kumbuka!masikitiko yako siyo ya wote, ukiuguliwa na ukifiwa bar hazifungwi kwasababu ya msiba wako au ndugu yako wa karibu.

Unadhani "akifa" sasa hivi kwa maoni yako watanganyika wote wata huzunika?

Matendo yake ndiyo mbegu aliyopanda mioyoni mwetu wananchi, kama ulitendewa wema utahuzunika kama ulitendewa vibaya utafurahi.

Furaha au huzuni zetu hazibadirishi matokeo, kumbuka "Kifo ni kifo tu".
 
Hakuwa mkali. Alikuwa sahihi sana kuongea na hili Taifa, kwa mazingira yake, kulikomboa Taifa. kuliko kiongozi yoyote.
Sema tatizo tuna mfumo mbaya. Yaani polisi wanasikiliza rais yaani mfano sina hakika kama Dkt Samia kaagiza kanisa kufungwa naamini hayo maagizo hajayatoa ila wasiaidizi wake wamefanya bila hata kumhusisha.
 
Umeliweka sawa kwa hekima, nadhani ni wakati Dkt Samia asikilize watu wanasemaje badala ya kuwa kiziwi
 
Chawa ni neno la wahuni wa sasa Samia.
Sisi tulikuwa wazalendo. Tunaangalia Tofauti ya mkataba wa Acacia na Twiga. 90% ya vetu iende kwa wageni au tugawane vizuri kwa rasilimali zote za Taifa.

Magufuli alilet Muongozo, alipambania Taifa kupata mkataba mzuri kwa Tanzania milele. Huo ni uzalendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…