Watanzania na kufurahia vifo vya wanasiasa, ja watawala wanajisikiaje?

Je, kuna kiongozi kadondoka? Tujuze.
 
Hata wewe ukifa wapo watakaofurahi vilevile
 
Mwana ccm yeyote hata akiwa ndugu yangu wa karibu akifa,au akipatwa na tatizo lolote siwezi kuhuzunika, kumuhurumia mtu anayeunga mkono mateso ya wengi ni unafiki mkubwa.
 
Hi hivi hata kabla JPM hajaanza kampeni kulinda rasilimali za nchi. Lissu tayari alianza kampeni ya kumtukana, kumkejeri, kuwa personal. Lissu aliiweka personal sana, badala ya kuangalia hoja JPM., kulinda, kuindeleza Tanzania haraka sana kama Singapore, Malaysia, China

Akamuita ni mshamba, ni msukuma, tume yote ya kulinda mali ta Taifa ni professional rubbish, aliwaambia tume yote ni wajinga kutetea maslahi ya Tanzania.
 
Wewe uliona na kusikia hayo aliyokuwa akiyasema Lissu; uliyaelewa?

Ni muhimu uelewe ninacho kuuliza hapa; ulielewa alichokuwa akisema Lissu, au na wewe ulichukuliwa kimawazo tu na lugha hiyo na kutotilia maanani kilichokuwa kikisemwa?

Ile tume wewe uliielewa kazi iliyofanya? Ile ilikuwa ni "tume ya kulinda mali za taifa"?

Magufuli kwa tabia zake alistahili kabisa hayo unayosema Tundu Lissu aliyazungumzia.
 
Nasimamia ukweli, maslahi ya Taifa. Leo namkubali Heche, Warioba, Mpina, Gwajima.
Inawezekana kabisa unasukumwa na "maslahi ya taifa"; kama Magufuli kwa namna yake tulivyo amini pia kuwa na msimamo wa aina hiyo; lakini akakosa busara ya kusimama ipasavyo. Matokeo yake ikawa ni vurugu tupu.

Ndio, hata sisi wengine tunawatazama hao kwa matumaini; na kwa hali ilivyo sasa, hakuna sababu ya kutomwingiza Tundu Lissu kwenye orodha ya hao uliowataja.

Magufuli na Tundu Lissu hawakuwa mbalimbali sana katika maslahi hayo; tofauti yao ilikuwa ni njia sahihi za kulinda maslahi hayo.
 
Bado hajaanguka tunayemtaka aanguke,akianguka huyo nitafanya matembezi ya shukrani kutoka Tabora to Dar Kwa baiskeli
 
Nakumbuka kipindi cha JPM ulikua huambiliki/hucheki na wowote.
Saizi nkisoma mabandiko yako naona ni "U-TURN" ya nguvu sana.
NB:
Kila kitabu na zama zake
 
Mkuu unawaonea huruma watawala wapuuzi, wanafanya nini cha maana hapa nchini zaidi ya kuliibia taifa? Tuwache tuwaombee vifo vya ghafla na kushangilia kwani hawana maana kwetu wala faida kwa taifa hili.
 
Waache tu wafe, hatuna muda nao.....mtu hujachaguliwa na wananchi, unajipa tu cheo kisha unakuja kuua wananchi wako....utakuwaje na furaha? Yaani hawa watu ni kuwaombea vifo tu na wakifa mnafanya sherehe.
 
Kalamu, njia sahihi ya kulikomboa hili Taifa ni ipi, Wewe ungekuwa kiongozi ungefanya nini?

Ni lazima uwasimamie wahuni,wezi, majambazi, mafisadi wa Taifa wote.

Unafanyaje?

Unapitia mikataba yote ya hovyo na kuivunja na kuweka mikataba mizuri kwa nchi. Unawaweka pembeni au kuwafunga mafisadi wa Taifa kama Mkono, Kikwete na wahuni wenzake wote, vita itakuwa kuwa sana.

Wakati ule Lissu aliipinga kwa kejeli sana nyie mkishangalia hilo zoezi. Mwamba JPM alikomaa nalo.




Aliita rubbish, wote mkashangilia. Heche Leo anaikubali.

kujenga haraka shule, hospitality Barbara, kuunda nidhamu, kuondoa ufisadi, kujenga uzalendo?
 
Wewe ukiwa Rais utafanya nini kulikomboa hili Taifa na mikataba ya hovyo, wahuni, agent wa CIA kibao kama makamu wako?
 
Hivi inakuaje kuaje hadi inafikia hapa mtu unajiita chawa
 
Hili jambo linafaa wajitazame watawala
 
Mkuu, 'Lookmasin', kwanza nikwambie tu kwamba unakosea sana unapohitimisha kama hivi unavyofanya hapa: "Wakati ule Lissu aliipinga kwa kejeli sana, NYIE Mkishangilia..."
Maneno kama hayo umeyarudia tena hapa: "Aliita rubbish, wote mkashangilia"
Uandishi wa namna hii unakuondolea umakini. Unaponihusisha mimi ninayejibishana nawe hapa kiujumla jumla tu hivyo bila kufahamu, na wala sijakueleza kuwa hali hiyo unayoieleza wewe ndiyo nilijihisi kuwa nayo wakati ule inanipa matatizo sana.

Maana yako ni kwamba, wewe ulivyokubali yooote aliyokuwa akifanya Magufuli, hata yale mabovu ulikubaliana nayo, hukutaka kuyahoji chochote. Sasa hali hiyo uliyokuwa nayo wewe, unaihamishia kwangu, na namna nilivyokuwa nikimchukulia Tundu Lissu! Itawezekanaje hivyo!

Nimekueleza toka mwanzo, Magufuli alikuwa na nia njema kabisa katika kupigania maslahi ya nchi, hasa katika hayo yote uliyoyataja wewe. Toka mwanzo, binafsi niliyapenda sana; lakini njia alizokuwa akitumia nyingi ya njia hizo zilikuwa za pupa na zisizozingatia taratibu. Kiongozi anapoondoka kwenye kufuata taratibu; hata awe na nia njema namna gani, mambo yataharibika.
Tundu Lissu, naye alikuwa na upungufu wake binafsi, pamoja na kwamba alitaka taratibu zizingatiwe. Katika kushauri kufuata taratibu, upungufu wake ukawa katika namna ya kushauri na matumizi ya maneno mabovu kama ulivyo yasema hapo. Huu naye ndio udhaifu wake; lakini nia ilikuwa ni ileile, ya kulinda maslahi ya nchi hii.
 
Wewe ukiwa Rais utafanya nini kulikomboa hili Taifa na mikataba ya hovyo, wahuni, agent wa CIA kibao kama makamu wako?
Unaniuliza swali hilo linalohitaji jibu la kina kabisa ambalo siwezi kulitendea haki kukupa wakati huu hapa.
Lakini kwa kifupi sana, ngoja nijaribu haraka haraka. Mengi ya haya naazima tu toka kwa Mwalimu Nerere, na baadhi kwa wafuasi wake kulingana na hali ya ulimwengu tuliyomo sasa.

Namba moja, ni kuhakikisha kuwa waTanzania wanakuwa na elimu ya kutosha kila mmoja wao, ya kuwawezesha kuwa na uelewa wa mambo muhimu ya nchi yao, na kulinda maslahi yao wenyewe na vizazi vijavyo.

Kuhakikisha waTanzania wanajijengea uwezo wa kufanya mambo yao mengi ya kujiletea maendeleo yao wenyewe; bila ya kulazimu kutegemea watu toka nje kuja kuleta maendeleo hapa.

Kunakuwa na mifumo ya kiutendaji, kila sehemu ya serikali isiyo vumilia ubofu, kama ufisadi, ufujaji wa mali za wananchi; utendaji hovyo wa wafanyakazi, n.k.; kama alivyo komalia Magufuli.

Kulinda raslimali za taifa hili, na kuhakikisha zinawanufaisha wananchi wote. hayo mambo ya mikataba mibovu imo humu.
Lakini la muhimu zaidi, ni kujiuliza: kama nchi kama Oman, Qatar, Saud na wengi wengine waliweza kunufaika na raslimali zao kwa kiasi kikubwa; inakuwaje sisi tujione kuwa ni tofauti na wao? Kwa nini sisi tunawagawia watu wengine mali zetu, halafu ndiyo nasi tupewe kiasi kidogo ya mali hiyo?

Tanzania ni nchi tajiri sana. Kilimo pekee, bila hata ya hayo madini kinaweza kabisa kuifanya kubadilika toka hapa ilipo na kuwa na watu wenye maisha mazuri zaidi. Maji yapo kila mahali, mito, maziwa, mvua zinanyesha maji yote yanasukumwa baharini, kwa nini?

Nilisema niandike kwa kifupi; najuwa kuna ambayo sikuyagusa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…