Watanzania Na Matumizi Ya "TO" Badala Ya "TA"

MwendaOmo

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2013
Posts
774
Reaction score
723
Kwanini WaTZ hutumia kiambishi(?) "to" wanapotaka kukanusha badala ya "ta?" Kwa mfano, atasema, Sitokuja badala ya kusema "Sitakuja." Ni kosa au ni lahja tofauti?

Kwa muda mrefu nilikuwa nikifiri kuwa ni lahja ya KiTZ watu wanapochanganya "r" na "l," kabla ya kujua kuwa ni athari za lugha ya mama
 

  • Sitokuja maana yake hakika sitakuja kamwe yaani apizo na mara nyingi wapenzi hutumia wakiwa na hasira hasa wanawake
  • Pia sitokuja, sintokuja, siji pia ni misemo ya apizo au hamaki
  • Sitakuja maana yake sitakuja leo, samahani sitakuja leo, baadaye n.k ila nitakuja nikipata nafasi ni usemi wa kistaarabu bila hamaki au hasira
 

Asante sana mkuu; kwa mara ya kwanza nimeelewa matumizi haya vyema. Kwa hivyo Sitakuja na Sitokuja; Sitalia na Sitolia yana maana tofauti? Kwa kuelewa kwangu basi, ukisema, Sitokuja, basi ni maamuzi umeyafanya...ilhali sitakuja yaweza kuwa kwa ajili ya sababu zisizohepukika?

Nashukuru sana.
 
Kwa uelewa wangu matumizi ya kiambishi 'to' hutumika kimakosa na wakati mwingine hutumika kimazoea na watu wa eneo fulani (lahaja).

Kiambishi sahihi ni 'ta' na hutumika kama kiambishi kiwakilishi cha wakati ujao.

Ukitaka kung'amua usahihi wa matumizi ya 'ta', jaribu kubadilisha nafsi inayohusishwa katika hali ya kukubali au kukataa.
Mathalani:
nitakuja (sitakuja)

Kitu ambacho hakikubali kama utatumia 'to'...neno nitokuja si neno sahihi.
 
Sauti /l/ na /r/ huchanganywa sana na wasemaji wa Kiswahili hasa wa bara ya Tanzania. Chanzo kimoja ni hizo lugha za kikabila. Nyingi ni za Kibantu ambamo sauti hizo hazina mlinganuo. Nyingi zina /l/ au /r/.
Hata hivyo wasemaji wengi waliokulia mijini hivi leo hutumia zaidi /l/ badala ya /r/. Wasemaji hao wengi wao hata hawasemi lugha za kikabila. Kwa kuwa mlinganuo wa sauti hizo mbili ni mdogo kwa kiasi fulani katika Kiswahili, basi zinachanganywa. Kwa mfano, /lafiki/ v. /rafiki/; /mpila/ v. /mpira/; /uhulu/ v. /uhuru/. Vilevile /chakura/ v. /chakula/, /kabila/ v. /kabira/ n.k. maneno hayo hayatofautishwi sana na baadhi ya wasemaji. Hata ktk JF utaona sana mambo haya.
Sisemi kwamba hakuna mlinganuo kabisa, upo. /karamu/ v. /kalamu/, /kura/ v. /kura/.
Kwa maoni yangu hiyo ni mojawapo ya athari za kutosomeshwa vizuri Kiswahili sanifu. Watu wengi wanafikiri Kiingereza kimekufa Tanzania kwa sababu ya mkazo uliowekwa kwenye Kiswahili. Nasema lugha kwa jumla zilipuuzwa katika mitaala yetu. Matokeo yake yalionekana kirahisi katika lugha ya kigeni. Na ktk Kiswahili, sasa matatizo hayo yanonekana kwa udhahiri zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…