Elections 2015 Watanzania na Rais ajaye

Elections 2015 Watanzania na Rais ajaye

Upanga Mkali

Member
Joined
Dec 24, 2014
Posts
96
Reaction score
83
WATANZANIA wanaelekea kutegua kitendawili cha nani awe Rais ajaye. Wametaja wasifu wa Rais huyo na kusisitiza kuwa uchaguzi wa mwaka huu umuweke kiongozi huyo kumrithi Rais Jakaya Kikwete.

Wamesema rais ajaye atashika madaraka, kubeba jukumu zito la kuhakikisha anawatoa watanzania katika hali ya umasikini na unyonge.

“Ni Rais anayekabidhiwa jukumu zito la uongozi wa nchi akiandamwa na changamoto ambazo atapaswa kuzikabili kiuweledi, kiadilifu, umakini na uzalendo unaozingatia maslahi ya Taifa”, amesema Dkt Benson Banna”, Mahadhiri Mwandamizi wa idara ya sayansi ya siasa na utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati akihojiwa na TBC.

Kiongozi ajaye wa taifa hili na timu yake ametajwa kuwa ni yule asiyegawa fedha kutafuta madaraka na kwamba watanzania wahakikishe ana afya njema kwa tahadhari ya misiba iliyoifika nchi jirani ya Zambia ambayo iliondokewa na Marais wawili, Levy Mwanawasa na Michael Satta.

Aidha ili kuimarisha hadhi ya maamuzi ya dola na vyombo vyake, nidhamu na uwajibikaji, rais ajaye ametajwa kuwa ni mfuatiliaji wa mchana na usiku wa majukumu mbali mbali ya wateule wake na anayeguswa na hali ya umasikini wa raia wake na kwamba atazingatia kuwa yeye ni mtanzania na mwafrika, atakayeshirikiana na majirani, jumuiya za kikanda, kimataifa na mataifa tofauti kwa kanuni na sera zinazoweka maslahi ya Taifa lake mbele.

Watu mbali mbali walioongea na gazeti hili kufuatia hotuba ya rais Jakaya Kikwete mjini Songea wamesema wanaungana naye katika kutafuta Rais bora ajaye.

Hata hivyo, wamesisitiza kuwa wale waliojitokeza kwa upande wa chama tawala na wale wanaotajwa upande wa upinzani hivi sasa hakuna hata mmoja mwenye sifa zinazompa ubora wa kuchaguliwa kuwa Rais ajaye huku wengine wakionekana kuwa na afya zilizotetereka ambao mara kwa mara huelekea nchi za Ulaya kwa matibabu.

Wamesema kwa ajili hiyo taifa linasubiri jina la mtu makini, asiye na makundi, mchapakazi asiye na doa ambaye utendaji wake wa hivi karibuni umeweza kuleta tija kubwa kwa chama fulani au serikali.

Aidha ametajwa kuwa nimwenye uwezo mkubwa wa kijieleza na kufafanua masuala mazito na ambaye anaheshimika kwa jamii kwa elimu, uweledi na uchapakazi wenye tija kwa Taifa.

“Tanzania ina rasilimali nyingi ikiwemo gesi, mafuta, madini, mbuga za wanyama, mifugo, ina njia ya reli, barabara, mito, bahari na maziwa kwa hiyo anahitajika msimamizi imara wa rasilimali hizi na miundombinu yake, atakaeunda timu makini itakayoweka mbele maslahi ya taifa, asiyemuonea haya yeyote, wala chuki na ulipizaji kisasi, ni muwazi ambaye hakwazwi na hofu ya ujamaa au urafiki katika kuchukua uamuzi wenye tija kwa taifa”, amesema Bwana Haji Kaburu mkazi wa jijini.

Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha usimamizi wa fedha(jina linahifadhiwa) amesema, Taifa limeendelea kuwa na kasoro ya kiuongozi iliyomlazimisha Rais kubadilisha watendaji mara kwa mara, hiyo inatokana na ama fitina za wanasiasa na wafanyabishara wenye masilahi binafsi au kutoshilikiwa miiko ya awali ikiwa ni pamoja na kulegezwa kamba ya ufuatiliaji wa karibu wa watendaji ndani ya mfumo wa serikali.

“Hii sasa iwe historia kuwa nchi ilipita katika kipindi cha unyoronyoro na kuoneana haya, serikali na mashirika yake yanahitaji kurejesha enzi ya serikali kuwa na jicho kali miongoni mwa watendaji wa taasisi za serikali ili kujenga nidhamu, kuzuia rushwa, uvivu na kutowajibika ipasavyo kwa kuwa “dola” inafuatilia kwa karibu, hili litawezekana kwa kupata Rais ajaye mwenye mawasiliano nadra na watu ambaye ataunda serikali itakayoongozwa na waziri mkuu anayefanana na Edward Moringe Sokoine si kikabila bali kimatendo na ambaye atakuwa mweledi zaidi kitaaluma”, ameshauri Mhadhiri huyo.

Amesema, timu ya watu watatu watakaokuwa juu lazima iwe na watu ambao kila mmoja atajitosha kimaamuzi, kiumakini na mwenye rekodi ya kuweka mbele maslahi ya Taifa ambaye hatachelea kuamuru lolote lenye kuzingatia maslahi kwa mnasaba wa sera na siasa za chama chake badala ya kusubiri maelekezo ya mkuu wake.

“Wakati Edward Moringe Sokoine alipoombwa ashike uwaziri mkuu kwa mara ya pili, alitoa masharti ambayo yalichapishwa katika gazeti la uhuru au mzalendo kama kumbukumbu zangu ziko sawa, masharti hayo yaliakisi uzalendo na nia njema ya kutumikia nchi yake ambayo alitaka kuitekeleza bila kukwaza na wakuu wake kichama na kiserikali kwa kuwa yeye binafsi alikuwa msafi, hakuwa na doa”, amesisitiza.

Mtaalamu kutoka Chuo ch Diplomasia Bwana Mwinjuma amesema, kitaalamu kupata aina ya uongozi utakaosimamia rasilimali za Taifa kwa manufaa ya wananchi hakuna budi kufanywe kwanza na watu wenye dhamiri njema kwa Taifa kisha wazo husika lipelekwe kwa jamii pamoja na kulisimamia kwa hali na mali.

“Kitaalamu kuna aina kadhaa za maongozi katika jumuiya za watu ambapo serikali, ikiwa jumuiya kuu, ina taratibu maalum zinazohitimishwa na uamuzi wa pamoja wa wananchi, ndio maana kuna vyama ambayo vina kamati kuu, halmashauri na mabaraza ya uongozi ambayo hutengeneza mawazo na kuyanyumbua kimaamuzi kabla ya kuyashindanisha na vyama vingine, vivyo hivyo serikali ina taratibu zake za kushawishi kile inachoona ni bora kwa wananchi wake ili kiamuliwe kidemokrasia”, amesema.

Aidha amesisitiza kuwa kama alivyofanya Mwalimu Nyerere wakati wanaingia Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa, aliwapendekeza akasimamia zoezi lote hadi wanakuwa marais, hivyo rais ajaye asimamiwe.

Asimamiwe iwe kutoka Chama tawala au vinginevyo ili atakapochaguliwa awe na ukali kidogo kuendana na historia ya nchi tangu Rais wa kwanza ambapo awamu za uongozi zimekuwa zikitofautiana kitabia na kiuhusiano.

“Kwa kuwa nchi inataka kuelekea kwenye uchumi wa kati mpaka ifikapo 2025 basi wakuu wangepaswa kuumiza vichwa kuangalia ni sifa zipi za watu wanaotakiwa kupelekwa kwenye jamii kwa ajili kupigiwa kura, hapa panahitaji umakini na kutomuonea haya mtu, panahitaji uzalendo na si maslahi binafsi, hivyo watu au wazee wenye kauli katika vyama wavute tafakuri ya kina kuwapima wale wote wenye kuonesha nia na wasioonesha nia, watumie vigezo anuai kulingana na utashi na imani za wananchi, wenye uweledi, uzoefu, utaalamu na umakini”, ameshauri msomi huyo.

Watu kadhaa waliotoa maoni yao wamesistiza kuwa Rais ajaye hanabudi kufichuliwa na akaelezwa wasifu wake kitaifa na kimataifa pamoja na mazuri yake ukiwemo uzalendo na uwajibikaji wake kwa majukumu aliyokwisha yabeba.

Aidha wamesisitiza kuwa kwa kuwa uongozi wa juu ni timu ya watu watatu, Rais ajaye aunganishwe na mwenza wake pamoja na mtendaji wao mkuu katika serikali ijayo, ambao jamii itaridhika na kushawishika kuwa nchi haijawahi kupata timu ambayo kila mmoja atakuwa na wasifu, uwezo na historia yenye kung’aa kimaamuzi pamoja na wasifu binafsi unaojitosha kulingana na yale aliyoyatenda.
 
Hayo maoni yamekusanywa Tanganyika tu ama na kwenye nchi mshirika Zanzibar?
 
Kikwete Hana sifa ya kuweza kutupatia Rais wa kuweza kuikwamua nchi kutoka .Keene
 
WATANZANIA wanaelekea kutegua kitendawili cha nani awe Rais ajaye. Wametaja wasifu wa Rais huyo na kusisitiza kuwa uchaguzi wa mwaka huu umuweke kiongozi huyo kumrithi Rais Jakaya Kikwete.

Wamesema rais ajaye atashika madaraka, kubeba jukumu zito la kuhakikisha anawatoa watanzania katika hali ya umasikini na unyonge.

Ni Rais anayekabidhiwa jukumu zito la uongozi wa nchi akiandamwa na changamoto ambazo atapaswa kuzikabili kiuweledi, kiadilifu, umakini na uzalendo unaozingatia maslahi ya Taifa, amesema Dkt Benson Banna, Mahadhiri Mwandamizi wa idara ya sayansi ya siasa na utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati akihojiwa na TBC.

Kiongozi ajaye wa taifa hili na timu yake ametajwa kuwa ni yule asiyegawa fedha kutafuta madaraka na kwamba watanzania wahakikishe ana afya njema kwa tahadhari ya misiba iliyoifika nchi jirani ya Zambia ambayo iliondokewa na Marais wawili, Levy Mwanawasa na Michael Satta.

Aidha ili kuimarisha hadhi ya maamuzi ya dola na vyombo vyake, nidhamu na uwajibikaji, rais ajaye ametajwa kuwa ni mfuatiliaji wa mchana na usiku wa majukumu mbali mbali ya wateule wake na anayeguswa na hali ya umasikini wa raia wake na kwamba atazingatia kuwa yeye ni mtanzania na mwafrika, atakayeshirikiana na majirani, jumuiya za kikanda, kimataifa na mataifa tofauti kwa kanuni na sera zinazoweka maslahi ya Taifa lake mbele.

Watu mbali mbali walioongea na gazeti hili kufuatia hotuba ya rais Jakaya Kikwete mjini Songea wamesema wanaungana naye katika kutafuta Rais bora ajaye.

Hata hivyo, wamesisitiza kuwa wale waliojitokeza kwa upande wa chama tawala na wale wanaotajwa upande wa upinzani hivi sasa hakuna hata mmoja mwenye sifa zinazompa ubora wa kuchaguliwa kuwa Rais ajaye huku wengine wakionekana kuwa na afya zilizotetereka ambao mara kwa mara huelekea nchi za Ulaya kwa matibabu.

Wamesema kwa ajili hiyo taifa linasubiri jina la mtu makini, asiye na makundi, mchapakazi asiye na doa ambaye utendaji wake wa hivi karibuni umeweza kuleta tija kubwa kwa chama fulani au serikali.

Aidha ametajwa kuwa nimwenye uwezo mkubwa wa kijieleza na kufafanua masuala mazito na ambaye anaheshimika kwa jamii kwa elimu, uweledi na uchapakazi wenye tija kwa Taifa.

Tanzania ina rasilimali nyingi ikiwemo gesi, mafuta, madini, mbuga za wanyama, mifugo, ina njia ya reli, barabara, mito, bahari na maziwa kwa hiyo anahitajika msimamizi imara wa rasilimali hizi na miundombinu yake, atakaeunda timu makini itakayoweka mbele maslahi ya taifa, asiyemuonea haya yeyote, wala chuki na ulipizaji kisasi, ni muwazi ambaye hakwazwi na hofu ya ujamaa au urafiki katika kuchukua uamuzi wenye tija kwa taifa, amesema Bwana Haji Kaburu mkazi wa jijini.

Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha usimamizi wa fedha(jina linahifadhiwa) amesema, Taifa limeendelea kuwa na kasoro ya kiuongozi iliyomlazimisha Rais kubadilisha watendaji mara kwa mara, hiyo inatokana na ama fitina za wanasiasa na wafanyabishara wenye masilahi binafsi au kutoshilikiwa miiko ya awali ikiwa ni pamoja na kulegezwa kamba ya ufuatiliaji wa karibu wa watendaji ndani ya mfumo wa serikali.

Hii sasa iwe historia kuwa nchi ilipita katika kipindi cha unyoronyoro na kuoneana haya, serikali na mashirika yake yanahitaji kurejesha enzi ya serikali kuwa na jicho kali miongoni mwa watendaji wa taasisi za serikali ili kujenga nidhamu, kuzuia rushwa, uvivu na kutowajibika ipasavyo kwa kuwa dola inafuatilia kwa karibu, hili litawezekana kwa kupata Rais ajaye mwenye mawasiliano nadra na watu ambaye ataunda serikali itakayoongozwa na waziri mkuu anayefanana na Edward Moringe Sokoine si kikabila bali kimatendo na ambaye atakuwa mweledi zaidi kitaaluma, ameshauri Mhadhiri huyo.

Amesema, timu ya watu watatu watakaokuwa juu lazima iwe na watu ambao kila mmoja atajitosha kimaamuzi, kiumakini na mwenye rekodi ya kuweka mbele maslahi ya Taifa ambaye hatachelea kuamuru lolote lenye kuzingatia maslahi kwa mnasaba wa sera na siasa za chama chake badala ya kusubiri maelekezo ya mkuu wake.

Wakati Edward Moringe Sokoine alipoombwa ashike uwaziri mkuu kwa mara ya pili, alitoa masharti ambayo yalichapishwa katika gazeti la uhuru au mzalendo kama kumbukumbu zangu ziko sawa, masharti hayo yaliakisi uzalendo na nia njema ya kutumikia nchi yake ambayo alitaka kuitekeleza bila kukwaza na wakuu wake kichama na kiserikali kwa kuwa yeye binafsi alikuwa msafi, hakuwa na doa, amesisitiza.

Mtaalamu kutoka Chuo ch Diplomasia Bwana Mwinjuma amesema, kitaalamu kupata aina ya uongozi utakaosimamia rasilimali za Taifa kwa manufaa ya wananchi hakuna budi kufanywe kwanza na watu wenye dhamiri njema kwa Taifa kisha wazo husika lipelekwe kwa jamii pamoja na kulisimamia kwa hali na mali.

Kitaalamu kuna aina kadhaa za maongozi katika jumuiya za watu ambapo serikali, ikiwa jumuiya kuu, ina taratibu maalum zinazohitimishwa na uamuzi wa pamoja wa wananchi, ndio maana kuna vyama ambayo vina kamati kuu, halmashauri na mabaraza ya uongozi ambayo hutengeneza mawazo na kuyanyumbua kimaamuzi kabla ya kuyashindanisha na vyama vingine, vivyo hivyo serikali ina taratibu zake za kushawishi kile inachoona ni bora kwa wananchi wake ili kiamuliwe kidemokrasia, amesema.

Aidha amesisitiza kuwa kama alivyofanya Mwalimu Nyerere wakati wanaingia Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa, aliwapendekeza akasimamia zoezi lote hadi wanakuwa marais, hivyo rais ajaye asimamiwe.

Asimamiwe iwe kutoka Chama tawala au vinginevyo ili atakapochaguliwa awe na ukali kidogo kuendana na historia ya nchi tangu Rais wa kwanza ambapo awamu za uongozi zimekuwa zikitofautiana kitabia na kiuhusiano.

Kwa kuwa nchi inataka kuelekea kwenye uchumi wa kati mpaka ifikapo 2025 basi wakuu wangepaswa kuumiza vichwa kuangalia ni sifa zipi za watu wanaotakiwa kupelekwa kwenye jamii kwa ajili kupigiwa kura, hapa panahitaji umakini na kutomuonea haya mtu, panahitaji uzalendo na si maslahi binafsi, hivyo watu au wazee wenye kauli katika vyama wavute tafakuri ya kina kuwapima wale wote wenye kuonesha nia na wasioonesha nia, watumie vigezo anuai kulingana na utashi na imani za wananchi, wenye uweledi, uzoefu, utaalamu na umakini, ameshauri msomi huyo.

Watu kadhaa waliotoa maoni yao wamesistiza kuwa Rais ajaye hanabudi kufichuliwa na akaelezwa wasifu wake kitaifa na kimataifa pamoja na mazuri yake ukiwemo uzalendo na uwajibikaji wake kwa majukumu aliyokwisha yabeba.

Aidha wamesisitiza kuwa kwa kuwa uongozi wa juu ni timu ya watu watatu, Rais ajaye aunganishwe na mwenza wake pamoja na mtendaji wao mkuu katika serikali ijayo, ambao jamii itaridhika na kushawishika kuwa nchi haijawahi kupata timu ambayo kila mmoja atakuwa na wasifu, uwezo na historia yenye kungaa kimaamuzi pamoja na wasifu binafsi unaojitosha kulingana na yale aliyoyatenda.
Kwa bahati mbaya paragraph ya nne tukaipuuzia 🥲

CC: Erythrocyte
 
Uzi huu unasadifu ajaye 2025 sio huyu kabisa au!!?

Ametumia fedha sana hadi sasa kana kwamba analazimisha kuwa ajaye kama kina lowasa na Membe!!?

Basi ajaye lazima awe mwadilifu!!Hana kashfa za uuzaji wa bandari!!?au kugawa rushwa za usafiri!!!?

Najiuliza kama wengine!labda ajaye sio huyu anaeimbwa!!

Mungu ibariki Tanzania!
 
Swadakta
 
Back
Top Bottom