Watanzania, na sisi tumempata Isaac Maliyamungu wetu?

Watanzania, na sisi tumempata Isaac Maliyamungu wetu?

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592
Naomba nianze kwa kunukuu kidogo maelezo mafupi kuhusu wasifu wa Isaac Maliyamungu na kwa nini ataendelea kukumbukwa. Natanguliza samahani kwa wasiojua lugha ya Kiingereza katika huu utangulizi, nitajaribu niwezavyo kutoa ufafanuzi tunavyoendelea.

Brigadier Isaac Maliyamungu

Isaac Maliyamungu was one of Idi Amin's most evil and feared Lieutenant who was in charge of quelling dissent in the army.

Before he joined the army, he had been a mere gatekeeper at Nyanza Textile Industries. At the time of the coup, he commandeered a tank with which he shot up the entrance to the Entebbe airport terminal, killing two priests.

After the coup he headed Amin's execution gangs, with unlimited power to execute anybody in the army, even officers senior to him. His modes of execution were as atrocious as anything imaginable. He was fond of disemboweling his victims.

Along with several other officers, he is known to have executed his victims by having them run over by tank. But perhaps the grisliest episode concerned Francis Walugembe, who had previously been Mayor of Masaka.

In September 1972, Walugembe was arrested, had his genitals cut off and was paraded through the streets before being killed and dismembered.

So violent and brutal was Malyamungu that even Amin once admitted fearing him believing he was going mad.

Flashback 1971.
Mwaka 1971, mapinduzi ya kijeshi yalifanyika nchini Uganga yaliyomuondoa madarakani Rais wa kwanza wa nchi hiyo Dr. Milton Obote.

Mapinduzi aliyoyafanya Idi Amin Dada yalipokewa kwa shangwe kubwa na Baganda, kabila kubwa nchini Uganda, ambao hawakufurahia jinsi Rais wao wa kuchaguliwa Dr. Milton Obote alivyompiga vita Mfalme wao, Kabaka wa 35.

Mfalme huyo Kabaka Muteesa II ilibidi aikimbie nchi na kutorokea Uingereza kusalimisha maisha yake. Hivyo Baganda walimuona Idi Amin kama mkombozi na walisherehekea ujio wake kwa namna ambayo haikuwahi kushuhudiwa awali.

Je Isaac Maliyamungu alitokea wapi? Itaendelea......

NB: Ombi kwa mods, kwa kuwa maelezo yangu yatajikita zaidi katika hali ya kisiasa na kijamii ndani ya taifa letu, naomba hii mada ibaki humu humu jukwaa la siasa.
 
A well known killer during Idd Amin tyrany rule! Mtu alikuwa anaomba kukutana na amin kuliko Maliyamungu. Same na Bashite.
 
Pia kuna kumbukumbu google kuwa Uganda iliwahi kuendeshwa bila Bunge kwa miaka minane yaani wabunge walipelekwa likizo ya lazima na serikali iliyokuwa madarakani wakati wa utawala wa kidikteta. Na wananchi wa Uganda walishangilia wamepata kiongozi mpya aliyeteremshwa na Mungu na uthubutu wakufuta Bunge na kuleta matumaini mapya.

Je Bunge letu la Tanzania awamu hii pia limepelekwa likizo ya lazima ''kiaina'' kwa kushindwa kuisimamia serikali na mhimili huu wa Bunge umeshindwa kuheshimiwa na mhimili mwingine wa dola/serikali kiasi unapewa maelekezo toka ngazi za juu nje ya Bunge.

Eight-Year Rule With No Parliament
Ahead of Uganda's 54th Independence Day, Richard Olwenyi explores Idi Amin's eight-year rule without a Parliament.

Source: NBS TV Uganda
 
Isaac-Maliyamungu..jpg

Hakuna anayejua kwa uhakika Isaac Malyamungu (wakati mwingine huandikwa Malyamungu) alikuwa mzaliwa wa wapi kati ya Congo, Uganda na Sudan lakini inadaiwa alikuwa ni wa kabila la Kakwa kutoka Congo. Wakakwa wengi wao ni Waislaam na ni wazaliwa wa Kusini Magharibi mwa Sudan ingawa ni kweli pia wako Congo na Kaskazini Magharibi mwa Uganda.

Kabla ya mapinduzi ya mwaka 1971 nchini Uganda, Isaac Maliyamungu alikuwa ni mlinzi katika kampuni iliyoitwa Nyanza Textila Industries. Wakati mapinduzi yanafanyika na katika hali ya sintofahamu iliyojitokeza aliweza kuteka moja ya matanki ya Jeshi na kuongoza mashambulizi ya kuuteka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe.

Kitendo chake hicho kilimpendeza kiongozi wa mapinduzi Idi Amin Dada ambaye mara moja alimpandisha cheo na kuwa Kanali Isaac Maliyamungu. Ukatili na ujasiri aliouonesha katika shambulio hilo na mengine yaliyofuata uliwapa hofu si wananchi tu bali hata wanajeshi wenzie wakiwemo wakubwa wake jeshini.

Ilipotokea tafrani au maasi yoyote yaliyohitaji mtu wa kuyazima Isaac Maliyamungu ndiye aliyepewa kazi hiyo. Kuna wakati alivamia kituo cha kati cha polisi mjini Entebbe alichodai kimempa hifadhi mtuhumiwa aliyemtaka na kesho yake kituo kilibaki kitupu baada ya polisi wote kufika hospitali kwa matibabu kufuatia kipigo kutoka kwa wanajeshi wake.

Je vyombo vya habari navyo vilipona? Itaendelea...
 
Back
Top Bottom