Watanzania na ustaarabu wa chooni...


We ukienda kushi kibera, ndani ya siku mbili tutakurudisha bongo ndani ya 'sanduku' kweli nakwambia.
 

Madam hebu ishia hapo hapo, umeshanikumbusha mambo ya Hall 5, UDSM. Choo cha kukaa unakuta mtu kakitumia kwa kuchuchumaa, kingo za basin la choo nyeusiiiiiiiii na njanonjano kiaina.

Hayo mambo ya usafi yanaweza kukupasua kichwa ukiyawaza sana coz wakati mwingine inategemea na makuzi ya mtu tangu utotoni. Inapofika ukubwani wakati mwingine watu wanakuwa wazito kujifunza. Hebu fikiria, mtu anataka kununua mhindi wa kuchoma, lakini ataugusagusa kwa viganja mhindi wote utadhani anaupima joto kama mtu afanyavyo kwa mgonja mwenye homa, agrrrrrrrrrrrrrrrr!
 
Nakumbuka wakati ofisi yetu iko jengo la Barclays House floor ya pili kulikuwa kuna Customer Care ya Vodacom ulikuwa ukienda hicho choo ukifungua mlango unakuta toilet paper zimetupwa chini kwenye dustbin kuna take away box za chakula, ilibidi tuombe uongozi wa jengo tutumie choo mbadala, halafu Ubungo Plaza vyoo vya pale unaweza kujiuliza hivi je niko mtaani au niko kwenye jengo ambalo lina ofisi kubwa na zenye hadhi
 
Mimi nina rafiki yangu mmoja Mghana...sasa siku moja alikuja kunitembelea. Baadaye akaenda haja kubwa halafu haku-flush. Binti yangu baadaye alipoenda chooni akatoka baruti huku kaziba pua kuja kuniambia 'daddy, daddy, Edward left a snicker bar in the toilet'. Nilicheka sana aisee.

Na ndiyo maana kwangu ni marufuku mgeni kutumia bafu na choo changu.
 

Sasa wageni wako wakiomba kutumia choo unawaambiaje?
 
Sasa wageni wako wakiomba kutumia choo unawaambiaje?

Hiyo id yako imenikumbusha wimbo flan hivi wa kitambo sana wakati magari aina ya Pajero yako chati.Jamaa alimnunulia mpenzi wake gari hilo huyo mpenzi alikua anaitwa Dora!
 
Niliwahi patwa na emergency call nikiwa mitaa ya Samora Ave. sintosahau ile siku...............
 
Tatizo kubwa ni kwenye highways. Hakuna toilets za public. Sasa huko msituni ukikutana na za mwenzio sijui inakuaje! Ila nadhani this is got something to do with the texture of our skin

Highway is just a manifestation of how we have been behaving in the places that have toilets. Kama kwenye toilets we live as if hakuna vyoo, kwanini highway tujenge vyoo? Nani atakuwa anasafirisha full time?
 
Kubadili tabia ni kaaazi kubwa aisee.Lakini inakuwaje mtu kama huyu anapokutana kuishi na mtu mwenye usafi? Si ni kasheshe?
Hivi... ukiwa wewe ni mkaka umekulia kwenye utamaduni wa usafi wa vyooni, unakutana na mdada ambaye kagubikwa na utamaduni wa uchafu eneo hilo and vice versa, utafanyaje? Ningependa kusikia visa vya aina hii.
 

Hahahahhah..ulimwengu wa kisasa kwa maisha ya ujima!
Inabidi mtu akianza kazi apatiwe orientation 101 how to use toilets lol...hivi ikitokea kwamba watu wanafanyiwa orientation, im sure "kila mtu' atajifanya - SIHITAJI , NAJUA! Hata walwe wachafu kupindukia.
 
Kuna haja ya kuifanyia utafiti! Mbona blacks wengine hawafanyi kama sisi? Hata ulaya weusi wapo,sema hali ya hewa inasababisha tuwe na texture tofauti za ngozi,lol! Yaani kuna jitu linaingia chooni,maji yapo lakini linaacha pachafu!kama hujui kutumia choo si ungeuliza? Kha!
tx my dear!!..hiyo texture ina nini hadi kuleta kero ivo?
 
Lol! Shurti ukunje sarawili kama unavuka mto! Umenikumbusha mbali!
halafu kuna wale wanamwagia maji bafuni yaani ukiingia maji ni kila mahali utadhani unaenda bwawani.. kwanini vyoo vingi haviwekwi amenities muhimu za kufanya iwe ni sehemu ya starehe?
 
Lol! Shurti ukunje sarawili kama unavuka mto! Umenikumbusha mbali!

Kuna mtu kaninong'oneza ati watu wengine huvua nguo zote wakaziacha nje
kabla ya kuingia chooni maana akiingia nazo atatoka kama kajifukiza lol!
Kweli "siasa" za vyoo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…