Watanzania na ustaarabu wa chooni...

Watanzania na ustaarabu wa chooni...

Kwanini lalkini?? Ustaarabu wa matumizi ya toilet kwa watz na hata waafrika wengine ni "0"
Je ni tamaduni zetu mbovu au?
Ukiacha public toilets ambazo huwa nI chafu karibu mara zote ukiacha
mahoteli makubwa ( huwa yana wasafishaji stand-by)..hata majumbani mwa baadhi ya watu utashangaa
uchafu ulivyozagaa...mimajimaji chepechepeeeeeee!! Hata maofisini! Miaka ya nyuma kidogo nakumbuka
ukiingia "Hazina" -yaani Wizara ya fedha kilichokua kinakupokea kuanzia mlangoni ni harufu mbaya ya choo!
Bora siku hizi kuna makampuni ya usafishaji yanafanya kazi nzuri lol!
Uswazi watu hufanya mambo yao kwenye mifuko ya "rambo" AU MAGAZETI na kutupa
barabarani usiku!
Binafsi kuna watu wakija nyumbani kwangu napata mashaka sana wakitaka kutumia
toilet!NAKWAZIKA LOL!

Sasa kuna wazo hapa..........nani alishajikuta yuko katikati ya mji au hata nje ya mji na anahitaji kutumia
toilet for short or long call........... utaenda vichakani au utafanyaje? Hata kama kuna choo cha umma au hata
cha "kulipia" sh 100-200/= unaweza ukapata homa ghafla utakapojaribu kuingia humo.
Nafikiria mobile/taxi toilets as an ideal business.... hahahah sipati picha itakavyokuwa .....

We ukienda kushi kibera, ndani ya siku mbili tutakurudisha bongo ndani ya 'sanduku' kweli nakwambia.
 
Hili nalo neno!
Maji chepechepe........ haya nayo huzidi kuchafua choo...
Sehemu nyingine utakuta wameweka vyoo ya kuchuchumaa (Asian type) na vya kukaa ( European type) hakuna "African type' lol...cha ajabu mtu mwenye kupenda majimaji hatumii cha kuchuchumaa, bado anakimbilia cha kuketi na bado anamwaga maji? Kwanini lakini?

Madam hebu ishia hapo hapo, umeshanikumbusha mambo ya Hall 5, UDSM. Choo cha kukaa unakuta mtu kakitumia kwa kuchuchumaa, kingo za basin la choo nyeusiiiiiiiii na njanonjano kiaina.

Hayo mambo ya usafi yanaweza kukupasua kichwa ukiyawaza sana coz wakati mwingine inategemea na makuzi ya mtu tangu utotoni. Inapofika ukubwani wakati mwingine watu wanakuwa wazito kujifunza. Hebu fikiria, mtu anataka kununua mhindi wa kuchoma, lakini ataugusagusa kwa viganja mhindi wote utadhani anaupima joto kama mtu afanyavyo kwa mgonja mwenye homa, agrrrrrrrrrrrrrrrr!
 
Nakumbuka wakati ofisi yetu iko jengo la Barclays House floor ya pili kulikuwa kuna Customer Care ya Vodacom ulikuwa ukienda hicho choo ukifungua mlango unakuta toilet paper zimetupwa chini kwenye dustbin kuna take away box za chakula, ilibidi tuombe uongozi wa jengo tutumie choo mbadala, halafu Ubungo Plaza vyoo vya pale unaweza kujiuliza hivi je niko mtaani au niko kwenye jengo ambalo lina ofisi kubwa na zenye hadhi
 
Mimi nina rafiki yangu mmoja Mghana...sasa siku moja alikuja kunitembelea. Baadaye akaenda haja kubwa halafu haku-flush. Binti yangu baadaye alipoenda chooni akatoka baruti huku kaziba pua kuja kuniambia 'daddy, daddy, Edward left a snicker bar in the toilet'. Nilicheka sana aisee.

Na ndiyo maana kwangu ni marufuku mgeni kutumia bafu na choo changu.
 
Mimi nina rafiki yangu mmoja Mghana...sasa siku moja alikuja kunitembelea. Baadaye akaenda haja kubwa halafu haku-flush. Binti yangu baadaye alipoenda chooni akatoka baruti huku kaziba pua kuja kuniambia 'daddy, daddy, Edward left a snicker bar in the toilet'. Nilicheka sana aisee.

Na ndiyo maana kwangu ni marufuku mgeni kutumia bafu na choo changu.

Sasa wageni wako wakiomba kutumia choo unawaambiaje?
 
Sasa wageni wako wakiomba kutumia choo unawaambiaje?

Hiyo id yako imenikumbusha wimbo flan hivi wa kitambo sana wakati magari aina ya Pajero yako chati.Jamaa alimnunulia mpenzi wake gari hilo huyo mpenzi alikua anaitwa Dora!
 
Niliwahi patwa na emergency call nikiwa mitaa ya Samora Ave. sintosahau ile siku...............
 
Tatizo kubwa ni kwenye highways. Hakuna toilets za public. Sasa huko msituni ukikutana na za mwenzio sijui inakuaje! Ila nadhani this is got something to do with the texture of our skin

Highway is just a manifestation of how we have been behaving in the places that have toilets. Kama kwenye toilets we live as if hakuna vyoo, kwanini highway tujenge vyoo? Nani atakuwa anasafirisha full time?
 
Kwa mwafrika choo ni mahali pa mwisho anapohitaji kuwepo ama kwenda. Ukirudi nyuma zaidi kwenye historia waafrika hatukuwa na utamaduni wa kujenga vyoo kwani mahitaji yote yalimalizikia porini. Na mpaka sasa kuna jamii ambazo bado hawajengi vyoo hata hivi vya shimo. Hivyo kwa mwafrika choo ni kitu kipya na ndiyo maana ukienda kwenye nyumba nyingi vyoo vinajengwa mbali sana na nyumba ili kuepuka harufu mbaya inayoambatana na uwepo wake. Ukifikiria choo kwa mwafrika unakumbuka harufu mbaya, uchafu na mara zote ni sehemu ambayo unatakiwa kutumia muda mfupi iwezekanavyo ili kuondoka.

Hapo ndipo penye fitna. Tunahitaji kubadilika aisee. Si tunaishi kwenye kijiji-utandawazi? Mbona watu wanaharakisha kurukia ustaarabu mwingine lakini kwenye huu wa choo ni zero?

Hata kwa wale ambao wanaishi mijini na hasa waliopanga kwenye nyumba za uswahilini ambapo watu kadhaa wanatumia choo kimoja bado vyoo vinabeba taswira ileile ya sehemu chafu ambayo kama ungepewa uchaguzi usingekuwa unaenda kabisa. Kwa bahati mbaya hata mashule tunayosoma bado vyoo havijapewa umuhimu unaotarajiwa.
Humo kwenye nyumba za uswahilini nako ni full vituko kwenye vyoo... utasikia mama mwenye nyumba anapanga zamu za kusafisha kama kukomoa vile! Ati " we mama fulani, tunakutaka wewe ndo ushafishe usimtume msichana wa kazi! Mashuleni ndiko kunajenga ustaarabu lakini shule zenyewe nazo unaambiwa vyoo ni vichache ukilinganisha na idadi ya wanafunzi, maji hakuna nk. Hata kama ni kufundisha adabu za matumizi ya vyoo, inakuwa kazi kwelikweli.

Ukitembelea shule za msingi, sekondari na hata vyuoni ambapo ndio tabia za usafi zinajengwa bado kuna tatizo kubwa la uchafu uliokithiri wa vyoo. Wakati ninasoma shule ya msingi na hata sekondari kusafisha choo ilikuwa ni adhabu kubwa na walimu walikuwa wakiitumia kwa watoto wakorofi. Sasa unatarajia mtu ambaye amezaliwa na kukulia kwenye mazingira ya vyoo kuwa vichafu na ambaye amelelewa kuamini kuwa kusafisha choo ni adhabu anaweza kweli kubadilika tu ghafla na kuwa msafi anapoanza kazi? Hata wale waliopewa kazi ya kusafisha choo bado wameathirika na utamaduni uleule wa kuona choo kuwa ni mahali pachafu
.
Kubadili tabia ni kaaazi kubwa aisee.Lakini inakuwaje mtu kama huyu anapokutana kuishi na mtu mwenye usafi? Si ni kasheshe?
Hivi... ukiwa wewe ni mkaka umekulia kwenye utamaduni wa usafi wa vyooni, unakutana na mdada ambaye kagubikwa na utamaduni wa uchafu eneo hilo and vice versa, utafanyaje? Ningependa kusikia visa vya aina hii.
 
Nakumbuka wakati ofisi yetu iko jengo la Barclays House floor ya pili kulikuwa kuna Customer Care ya Vodacom ulikuwa ukienda hicho choo ukifungua mlango unakuta toilet paper zimetupwa chini kwenye dustbin kuna take away box za chakula, ilibidi tuombe uongozi wa jengo tutumie choo mbadala, halafu Ubungo Plaza vyoo vya pale unaweza kujiuliza hivi je niko mtaani au niko kwenye jengo ambalo lina ofisi kubwa na zenye hadhi

Hahahahhah..ulimwengu wa kisasa kwa maisha ya ujima!
Inabidi mtu akianza kazi apatiwe orientation 101 how to use toilets lol...hivi ikitokea kwamba watu wanafanyiwa orientation, im sure "kila mtu' atajifanya - SIHITAJI , NAJUA! Hata walwe wachafu kupindukia.
 
Kuna haja ya kuifanyia utafiti! Mbona blacks wengine hawafanyi kama sisi? Hata ulaya weusi wapo,sema hali ya hewa inasababisha tuwe na texture tofauti za ngozi,lol! Yaani kuna jitu linaingia chooni,maji yapo lakini linaacha pachafu!kama hujui kutumia choo si ungeuliza? Kha!
tx my dear!!..hiyo texture ina nini hadi kuleta kero ivo?
 
Lol! Shurti ukunje sarawili kama unavuka mto! Umenikumbusha mbali!
halafu kuna wale wanamwagia maji bafuni yaani ukiingia maji ni kila mahali utadhani unaenda bwawani.. kwanini vyoo vingi haviwekwi amenities muhimu za kufanya iwe ni sehemu ya starehe?
 
Lol! Shurti ukunje sarawili kama unavuka mto! Umenikumbusha mbali!

Kuna mtu kaninong'oneza ati watu wengine huvua nguo zote wakaziacha nje
kabla ya kuingia chooni maana akiingia nazo atatoka kama kajifukiza lol!
Kweli "siasa" za vyoo!
 
Back
Top Bottom