Watanzania na waafrika kwa ujumla tuna wajibu wa kimaadili kupeleka ustaarabu ulaya na Marekani!

Watanzania na waafrika kwa ujumla tuna wajibu wa kimaadili kupeleka ustaarabu ulaya na Marekani!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Kwa kawaida huwa tunapokezana wajibu kwa mzunguko. Kuna wakati katika historia Afrika ilikuwa nyuma sana katika kiwango cha ustaarabu, maadili na utu!! Machifu walikuwa kama miungu watu, chochote atakachokipenda chifu anaamua kukichukua hata kama ni shamba lako, mke wako, ng,ombe wako nk. Chifu akifa, husindikizwa na mtu mzima huko kaburini wakati wa mazishi yake!! Zamu ikimwangukia mwanao kumsindikiza chifu huna cha kufanya.

Ni wazungu waliotuletea nguo na mavazi ya kusitiri miili yetu! Wakati huo tulikuwa tunatembea tu uchi uchi!!

Lakini kikubwa pia na masuala ya ibada. Tulikuwa tunaabudu mizimu, hatukuwa tunamjua Mungu wa kweli. Leo hii mtu asipomwamini Mungu wa kweli ni maamuzi yake binafsi lakini Wamishionari toka ulaya na Marekani walikuja kutupa habari ya Mungu wa kweli na ni hiari ya mtu kumwamini au la!!

Kwa sasa hao waliotuletea maisha ya ustaarabu, wamekengeuka kuliko mfano wowote! Wamerudi kwenye maisha ya ushenzi usiokuwa na mfano!! Hao waliotuletea nguo wao leo wanavaa nusu uchi, wakati mwingine uchi kabisa!! Kwa bahati mbaya sana dada zetu wanawaiga na wao kutembea nusu uchi!! Mtu ananunua nguo iliyotobolewa kwenye mapaja halafu anavaa!! Huu ni ushenzi!!

Wanakataa kuwa jinsia aliyozaliwa nayo mtu ndiyo jinsia yake! Wamefikia kiasi ambacho mtoto akizaliwa cheti chake cha kuzaliwa hakiainishi kama ni ke au me! Wanadai atakuja kuamua mwenyewe jinsia yake!! Wanaoana ke kwa ke au me kwa me. Wakati mwingine mtu anaoa mke huku yeye pia japo ni mume lakini ameolewa pia na mume mwenzake!! Awali uchafu na ushenzi huu walikuwa wanauonea aibu na kuufanya siri. Lakini leo ndio kitu wanachojivunia na wanapambana kueneza ushenzi huu duniani kote wakidai ni sehemu ya uhuru wa binadamu!

Badala ya kuwacheka naona ni zamu ya Afrika kuvuka mipaka na kwenda ulaya na marekani kupeleka huko ustaarabu wa kweli! Watakuja kutushukuru baadaye. Tuanze kupeleka wamishionari wa ustaarabu na dini huko ulaya na marekani! Tukawafundishe jinsi ya kuvaa kwa unadhifu na heshima!! Tukawafundishe kumcha MUngu aliyeumba mbingu na nchi!! Tukawafundishe kuheshimu utu wa mtu!! Tukawafundishe kuwa ni zaidi ya unyama me kuoana na me, au ke kuoana na ke!! Tuwaambie kuwa wamepotoka!! Watakuja kutushukuru!!

Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunalipa fadhila walizotutendea awali kwa kutuletea ustaarabu wa kuvaa nguo na wa kumwamini Mungu wa kweli na kuachana na mizimu!! Tusipofanya hivyo ni sawa na kumwona mgonjwa na kumwacha bila msaada japo uwezo wa kumsaidia unao!! Wazungu ni wagonjwa wa kimaadili ni zamu yetu kuwasaidia. Tukifanya hivyo tutakuwa tumehifadhi kizazi cha uadilifu huko ulaya na marekani!! Nani ajuaye huenda huko mbele na Afrika inaweza kuja kupotoka kimaadili na wao wakaja tena kutuletea ustaarabu maana maisha ni mzunguko!! Tukiwaacha wazungu waharibike huenda mbegu yenye uadilifu ikapotea kabisa duniani na huko mbele afrika wakiharibika hakutakuwa na watu wa kuweza kuwarejeza upya!! Tukubali wajibu na tuchukue hatua ya kuwasaidia wazungu maana wamepotoka sana kimaadili!!
 
Write your reply...mwanafunzi anarud kumfundisha mwalimu wake
 
Walutheri(wazungu wa mwanzo kuja) wanakuja tabora walitukita tukitengeneza nguo zetu wenyewe,viwanda vyetu' simpo,tulivaa mgolole,walikuta waarabu wameshamleta Allah sw siku nyingi
 
Pole sana mtoa mada. Umesoma hata hizo tamaduni zetu ukaona zilikuwaje hapo mwanzo. Na zimeathiriwa vp na wageni

Binafsi sijasoma sana lakini nilizopitia zimetosha kunipa mwanga 1. Imani za jadi za kisukuma na Liwelero Cha Bujora na 2. Facing Mount Kenya Cha Jomo Kenyatta.

Ushauri wangu ni wewe mtoa mada kwenda kuwasikiliza waafrika wenyewe wanasemaje kuhusu mila zao na sio kuzisikia kwa mzungu. Brainwashing is real.
 
Back
Top Bottom