GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Nawalinganisha kama ifuatavyo:
1. Viongozi
Kenya inaweza ikawa na viongozi wengi wabinafsi, sema wanathibitiwa na Katiba yao imara.
Tanzania imeshawahi kuwa na wazalendo wachache kama hayati Nyerere, Magufuli na Sokoine.
Kwa sasa, kuna Tundu Lissu, Jerry Slaa, Joseph Warioba, n.k., lakini kutokana na ubovu wa Katiba, michango yao inaweza isiinufaishe nchi.
3. Vyombo vya dola
Nitajikita kwenye Jeshi la Ulinzi. Kwa Tanzania, sina mashaka na uzalendo wa JWTZ. Lakini kwa KDF, wanakosa maksi kutokana na walichokifanya kwenye sakata la Waste Gate. Waliiba mikate badala ya kufanya kazi waliyotumwa ya kutafuta magaidi.
3. Raia
Hapo maksi zinawaendea Wakenya. Hawana mchezo linapokuja suala la maslahi ya nchi. Huziweka pembeni itikadi zao za kidini, kikabila na Siasa. Ndiyo maana viongozi wao wanawaheshimu. Hawapelekwi kama "mang'ombe".
Ukija kwa Watanzania ni aibu tupu! Uoga umewafanya kuwa wadogo kama piriton. Hata wakitangaziwa kuwa Ikulu imeuzwa nahisi watakaa kimya tu!
Halafu watajifariji kwa kibwagizo cha "nchi yetu ni kisiwa cha amani".
Kwa mlinganyo huo, Kenya inaweza ikajizolea ushindi linapokuja suala la uzalendo!