Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?


Wananchi wameshaitaka sana hadi maoni yao yalishakusanywa, tena kisheria. Watawala wa CCM wenye kiburi viburi vya madaraka ndio wameendelea kuizuia katiba hiyo kwa vitisho, hila na ghiliba. Na ww ni mmoja wa hao wafanya ghiliba ili katiba isipatikane. Machafuko tu ndio yataleta katiba mpya.
 
Wananchi gani hao, kama sio wale waliopitia mlango wa vyama vya siasa ambao wamechangia pakubwa kunajisi zoezi zuri la upatikanaji wa katiba? Vya vya siasa kaeni pembeni mchakato uwehuru usiokuwa na chembe ya kiherehere za chama Cha siasa chochote, zoezi liludiwe kama like la kipindi Cha akina walioba na wenzake. Kwa kuwa jambo hili limekua la kisiasa, wananchi Sasa wanaliona kama katiba IMEKUWA ni ya chama Fulani na Kwa matakwa Yao.
 
Mkuu Dp800 asante sana kunitia moyo, faraja yangu ni Matayo 5
5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
9 Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
Amen.
P
 

Kila mtu anataka katiba ifuate maoni yaliyokusanywa na tume ya jaji Warioba. Vyama vya siasa ni watanzania na wana wajibu wa kufuatilia jambo lolote watakalo, ili mradi hawavunji sheria. Usitegemee eti hivyo vyama vya siasa vitakaa kimya bila kuweka msukumo wa kupatikana kwa katiba mpya, kwa kusubiri wananchi waongelee. Kwa hii nchi yetu kila jambo lina watu wanaliwekea msukumo, kisha makundi mengine na wananchi kwa ujumla wanafuata.

Mimi ni mwananchi na ninaona sahihi vyama vya siasa kuweka msukumo kwenye upatikanaji wa katiba mpya. Sasa hao wananchi unaosema wameona ni zoezi la wanasiasa umekusanya wapi hayo maoni? Acha kuwa bendera fuata upepo, ukisikia viongozi wa ccm wanaongelea jambo fulani, na ww unalirukia ili kufanya upotoshaji wa kijinga.
 
Umenena sana lakini kikwazo kikubwa cha Tanzania na waBongo wenyewe. Wanaotuongoza ni waongo na wanafuki sio DC sio mkuu wa Mkoa, sio mbunge na hata Waziri! Wanazuga kila kukicha ili kulinda maslahi yao, Hawa ndio CCM walaji Wakuu!
Akitokea mwenye kusema ukweli anaambiwa hafai na amesaliti chama.
Hivi chama ni wao au ni waTanzania!
KATIBA mpya halikwepeki ni jambo endelevu japo Kuna madilu wanaona ni sakata.
Kwaheri 22 na karibu 23.
 


P,

Mimi kwa mawazo yangu waandishi wa habari inabidi wawe wazalendo. Tusiko kuwa makini katiba itabaki kuonekana ni kwa manufaa ya Chadema badala ya manufaa ya taifa. Hivyo nyie waandishi wa habari mnatakiwa kuongea umuhimu wa katiba mpya bila kuweka siasa na mbele ya vyombo vyote na sio mitandao halafu kwenye tv unabadilika.
 
Sema wewe ni chadema Tena mwenye t.shirt ya chama chako na maandishi ya katiba MPYA ni Sasa. Nyinyi daini katiba ya chama chenu. Katiba ya wananchi itatafutwa na wananchi wasio na chama chochote.
 
Unaelekea ninapodhan ndo option pekee iliyobaka yaan confrotation. Ajab hukuhitimisha tuanzie wapi!
Mpaka sasa kazi inazid kuwa ngumu kwa sabab ushost wa mkandamizaj, ccm, na wenye dunia uko vizur tunabak kujipambania bila external force.
Mbaya zaid kwa sasa hatuna hata kiongoz mwenye dhati wa kutanguliza mbele. Tuliacha kuwaunga mkono kwa wakat muafaka sasa wameamua nao kususa na kukaa na mtesi wa wananchi katika meza ya maakuli. Bila wanasiasa zoez hili ni gumu.
Mwisho, ni HATUJACHELEWA. Ilimrad tukubali kumwaga damu.
 
Waambie wananchi Ukweli.
Waambie Wananchi kuwa hatuwezi kuandika Katiba mpya bila Ridhaa ya Mkuu wa Jumuiya ya Madola....Na ndio maana nashikilia kidete Tuondoke katika Jumuiya hiyo.

Tuambiane ukweli badala ya kujivua nguo na kutokujieshimu kwa kuitana hatuna Akili, kuwa mambo yetu ni Zero! Inauma iwe kweli au la.

We must, change our mindset.

Kuandika au Kubadilisha Katiba kunahitajika kufanya Maamuzi magumu bila kutetereka. Vishinikizo haviko hapa kwetu vipo nje. Mabakuli yanatusumbua.

Amani-Heri ya Mwaka Mpya Inshallah.
 
Nilishalisema hili lakn kwa kuwa ss ni watanzani hakuna wa kubadilika. Acha tuendelee na tuachokijua ~kulalamika~
 
Sema wewe ni chadema Tena mwenye t.shirt ya chama chako na maandishi ya katiba MPYA ni Sasa. Nyinyi daini katiba ya chama chenu. Katiba ya wananchi itatafutwa na wananchi wasio na chama chochote.

Hao wananchi wataanza lini kuidai hiyo katiba mpya? Ama hao cdm sio wananchi? Kama CDM wameamua kuidai wataendelea kuidai, na hawamzuii mwananchi yoyote kuidai.
 
Duh! Bro kama unajisahaulisha hivi? Hivi kwani wewe umeshalia au kujiliza mara ngapi humu jukwaani? Achilia mbali kulia na kupiga ukunga kuleee kwenye Mnavu na Mchicha.
 
Uligombea Kawe, ukapigwa chini, ukogombea East Africa, ukapigwa chini, Hapa JF wakakushindanisha kwenye jukwaa la siasa ukapigwa chini. Unajua sababu? Sababu ni kwamba wewe ni pangu pakavu tia mchuzi. Huna msimamo, huaminiki, unaweka tumbo mbele na mishipa ya aibu ilishakatika.
 
Uligombea Kawe, ukapigwa chini,
Ni kweli, niligombea na kitu cha kwanza ni kuleta sababu za kugombea, , niligombea
nilizidiwa sifa na niliogombea nao, nikakubali matokeo na humu JF nikayaleta Uchaguzi 2020 - Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!
ukogombea East Africa, ukapigwa chini,
Ni kweli, kabla ya kugombea EALA pia militia sababu, Ubunge EALA, Wito Kwa CCM, Msiangalie Ukwasi, Tuteulieni, Wazalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Wenye Uwezo na Uzoefu wa Kimataifa Kutuwakilisha Ipasavyo nikagombea, nikazidiwa sifa nimeshindwa na kukubali matokeo EALA: Waliopitishwa CCM, ni Kwa Haki!, Tulioachwa ni kwa Haki, Tumezidiwa Vigezo!. Thanks4 for Support, Nimekubali Matokeo Kiroho Safi! Kazi Iendelee!
Hapa JF wakakushindanisha kwenye jukwaa la siasa ukapigwa chini.
Pia ni kweli, nako pia nimezidiwa vigezo nikashindwa!.
Unajua sababu? Sababu ni kwamba wewe ni pangu pakavu tia mchuzi. Huna msimamo, huaminiki, unaweka tumbo mbele na mishipa ya aibu ilishakatika.
Hili pia ni kweli, Luna vitu mtu unapewa kabla hujazaliwa na vingine baada ya kuzaliwa, aibu ni kitu kinachotolewa baada ya kuzaliwa, hivyo nilipozaliwa ilipofika wakati wangu wa kuzaliwa mgao wa aibu, ikatokea bahati mbaya, Sikh hiyo tulikuwa wengi zaidi ya aibu zilizokuwepo hivyo wenzetu waliobahatika wakapata mgao wao, sisi tusio na bahati tukakosa mgao!.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…