Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?

Sawa mkuu
Huko Kundini hakuna Tena chako na upo tiyari kugusa maslai ya wakubwa?
Mkuu HAYA LAND, kwenye Tanzania, katiba ndio kila kitu, hakuna wakubwa zaidi ya katiba isipokuwa mwenye katiba ambaye ni Mtanzania.
Kuna the purported boss na the real boss!,
The purported boss ni yule aliyepewa mamlaka ya kutusimamia kwa kuajiriwa kwa kura zetu na kulipwa mshahara kwa kodi zetu, the real boss ni aliye ajiri, na anayelipa mshahara!.
I work for the real boss and not for the purported boss!.
P
 
Naona we mzee unasema au "watanzania tufanye kitu" kitu gani hicho,tufanye ???

Ova
Kama ni kusema, tumesema sana, kama ni kuandika tumeandika sana, na kama ni kulia tumelia sana!. Sasa we must do something more, yaani lazima tufanye kitu zaidi ya kusema tuu, kuandika tuu na kulialia tuu, jee tufanye nini, hiyo ni subject nyingine, sasa tuko kwenye hatua ya kwanza, tutie Nia, tunuizie kufanya kitu!.
P
 
Hiyo kufanya kitu,hapo tufanye kitu gani au tulianzishe pascal

Ova
 
Mkuu TUJITEGEMEE , nia ndio the most powerful thing hapa duniani. Ukiweka nia ya dhati, hiyo nia inatengeneza powers of will, where there is a will, there is a way
P
 
Ni hivi, bila machafuko hakuna katiba mpya yenye utashi wa wananchi. Hiyo ya kupangwa na dola ndio hiyo hiyo tunayoipigia kelele kila siku.
Mshafanya yapi na yapi hadi sasa uone njia iliyobaki ni machafuko? Kama hao wananchi wanaonekana wengi hawana huo muamko wa kuhitaji katiba mpya na kufanya ionekane chadema(chama cha siasa) ndio wanahitaji katiba mpya kwa hali hiyo ndio unasema kufanyike machafuko? Wenye kufanya hayo machafuko kwa lengo la kupata katika mpya ni akina nani?
 
Ungeanza wewe mwnyw kuonyesha uzalendo wako kwa taifa lako Kwa vitendo
Mimi ni mzalendo wa kweli wa taifa langu, na siku zote nimeonyesha uzalendo wangu kwa kutumia uwezo wangu kufanya kile ninachoweza, uwezo wangu ulikuwa ni kwenye kuandika na kutangaza tuu, hivyo nimeandika sana humu na magazetini, na nimetangaza sana kwenye TV, YouTube na mitandao ya kijamii, haijasaidia kitu kubadili lolote na chochote, sasa ndio mwaka huu naweka nia ya kufanya kitu.
Kwa kupinga blah blah za rafiki yako makamba kila kukichakutukatia umeme akijitetea kwasababu zisizo na mashiko akidhani watanzania wote hatuna akili[emoji3525]
Hili la JM, ni sawa na ninayopitia, kuna watu wana damu ya kunguni, wanachukiwa tuu bila sababu!. Hili halikubaliki!.
P
 
Unasikitisha sana!!!

Kwani kutenda kwa kufanya mikutano na maandamano kudai KATIBA MPYA sio kwa mujibu wa KATIBA, SHERIA na KANUNI za Nchi??

Huo wasiwasi unaouzungumzia ktk hili ni wa kinafiki, acha UNAFIKI...

Mikutano na Maandamano ya kudai KATIBA sio uvunjifu wa SHERIA ni njia sahihi kabisa zinazoruhusiwa na KATIBA iliyopo kudai dai la HAKI...


Hapa ni wewe na wenzako "WatanzaniaChawa" ndio muache UNAFIKI na woga ili 2023 tuidai KATIBA MPYA kwa vitendo.

Inawezekana...ukiacha maneno maneno na UNAFIKI na ukaleta vitendo...

Leta Vitendo 2023 tupate KATIBA MPYA...

Barikiwa.
 

Akina Sisi.
 
 
It can be done Bro! Let us play our part.

Utakuwa ni uwendawazimu, kuingia kwenye uchaguzi mkuu na hii Katiba ya 1977! Kama vipi tulianzishe tu.
 
Katiba mpya lazima iandikwe kabla ya 2030,chamsingi tujiandae na kujipanga kuhakikisha haitatekwa tena na kundi la wachache na kukwama tena.
 
Inakuwaje tena uchochezi mkuu, na wakati ni kweli ikishindikana kudai haki kwa njia ya amani, nguvu hutumika! Au hiyo namba 4 yako hapo inahusu nini?
 
Mkuu Pascal Mayalla hili andiko bora la kufunga mwaka naliunga mkono kwa 100%, tunachotakiwa kufanya sasa 2023 tunachambua kipengele kimoja baada ya kingine cha Katiba ya Mwaka 1977 ili kuone mapungufu yaliyopo na kupendekeza namna bora ya kuendesha nchi yetu. Hii ni nchi yetu sote na wala sio nchi ya familia moja tu ya 'Watu Wazuri Hawafi' tuna kila sababu kuunganisha nguvu kupata Katiba itayosaidia kuboresha uwajibikaji wa viongozi. Ombi langu kwako JM ungeachana naye kwanza anaharibu Cv yako ni kiongozi asiyewajibika katika nafasi yake na anatumia muda mwingi kutunga visingizio vya kujitetea kwenye umma badala ya kutunga utatuzi wa matatizo ya wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…