Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?

Mimi ni mmojawapo ambaye kupitia humu jamii forum, ndio nasoma vilio vingi kuhusu katiba,

Lakini ambacho nasoma ni kuwa tunataka katiba mmpya, au kitu fulani kimekuwa hivi sababu ya hii katiba,.

Lakini wakati mwengine nasikia hata katiba hihii ambayo tunayo inavunjwa au kukiukwa na hakuna kinachofanyika,

Sasa je hiyo katiba tunaitaka itafanyaje mpaka isivunjwe kama hii ambayo tunayo?,

Mimi nadhani umefika wakati kwa wajuzi wa humu kuanza kutuonyesha udhaifu wa katiba hii na umuhimu wa katiba mpya kama somo ili kutuondolea ujinga huu ambao tunao ili hata na mimi nikiulizwa kuhusu ubovu wa katiba hii iwe rahisi kuelezea .

Paschal nakutegemea uanze kutupa Elimu hii.

Na utuelewesha namna katiba mpya isivyoweza kuvunjwa kama hii,

Maana wakati unaweza kuzani kwamba tunahitaji katiba saana, kumbe ni uvunjaji wa sheria tu.
 
Tupunguze maneno tulipe kodi ijenge nchi
 
Lakini nyie wananchi tunaambiwa kuwa ndio mliyotaka wenyewe katiba mpya, maana yake mliweza kuona mapungufu ya katiba ya sasa?
 
Mkuu wewe binafsi umetoa mchango gani katika kufanikisha upatikanaji wa katiba mpya? Tatizo hili jukumu tumewaachia baadhi ya vyama vya upinzani. Sisi wengine tunawatazama tu na mwisho wa siku tunakuja na mabandiko kama haya kuwananga wapinzani.
Mkuu tamsana, kwenye hili la katiba, sijananga mtu!.
Happy New Year!.
P
 
Akina nyie machafuko yenu humu mitandaoni tumeshayaona sana tu.

Huku mitandaoni ni sehemu ya kuhamasishana maana watu wataumia, au unadhani maandamano dhidi ya jambo lisilopendwa na serikali ni sawa na maandamano ya kumbukumbu ya moyo mtakatifu wa Yesu?
 
Huku mitandaoni ni sehemu ya kuhamasishana maana watu wataumia, au unadhani maandamano dhidi ya jambo lisilopendwa na serikali ni sawa na maandamano ya kumbukumbu ya moyo mtakatifu wa Yesu?
Kipi mlihamasishana mitandaoni athari yake ikaonekana huku mitaani?
 
Lakini nyie wananchi tunaambiwa kuwa ndio mliyotaka wenyewe katiba mpya, maana yake mliweza kuona mapungufu ya katiba ya sasa?
Mimi binafsi, hayo mapungufu ya katiba iliyopo bado sijaambiwa na siyajui,

Ninachojua ni ukiukaji wa katiba iliyopo,

Kiufupi wanaotakiwa kufuata katiba hawaifuati, au wanavunja sheria za katiba makusudi,

Kwa nini tusianze kwanza na kupiga kelele kuhusu uvunjwaji wa katiba ya sasa, kuliko kutaka katiba mpya ambayo hata kama ikija na uvunjwaji ukawa hivi hivi, bado tutadai katiba nyingine.
 
Kipi mlihamasishana mitandaoni athari yake ikaonekana huku mitaani?

Unauliza au unapigia jibu mstari? Husikii mara kwa mara serikali ikitoa ufafanuzi huku ikisema kutokana na maoni yaliyoko mitandaoni? Kwani siku hizi serikali inasikilizia wapi maoni ya wananchi zaidi ya mitandaoni. Ama unataka kujitoa ufahamu?

Mfano punguzo la tozo za miamala ya simu. Ufafanuzi kuhusu mabewa ya treni huku viongozi wa serikali wakipishana kauli kutokana na shinikizo la wanaohoji kuhusu mabehewa hayo huku mitandaoni. Au umewahi kuona watu wamekutana mahali wakifanya mkutano kutaka wapewe majibu ya mabehewa kubwa ni mapya au mtumba zaidi ya mitandaoni? Na kama mitandao haina impact hiyo, kwanini wakati wa uchaguzi mkuu mitandao ya kijamii ilizimwa?
 
Naunga mkono hoja, the powers now lies with mitandao!, jambo likiuliziwa mitandaoni, serikali inakuja kulijibu rasmi.
P
 
Nimeuliza kuhusu kuhamasishana kwamba mkahamasishana kufanya jambo na kweli tukaona matokeo huku mitaani, sio kujadili jambo tu mtandaoni.

Mangapi yamelalamikiwa humu mitandaoni na bado serikali inayapotezea?
 
Kwani hiyo serikali imetekeleza yale yote inayoyataka hadi useme imeyapotezea yaliyolalamikiwa tu huku mitandaoni?
 
Kwani hiyo serikali imetekeleza yale yote inayoyataka hadi useme imeyapotezea yaliyolalamikiwa tu huku mitandaoni?
Nasema imeyapotezea kwa maana hata ya kutoyatolea ufafanuzi au wakati mwengine kutolea majibu ya dharau kwa kuonekana ni kelele za mitandaoni tu.

Kimsingi huku mitandaoni hatuna nguvu hiyo mnayofikiri tunayo.
 
Ukiona hawajajibu ujue hawana majibu, na wakijibu kwa dharau ujue sababu ni uwezo wao mdogo. Vyovyote iwavyo kwa dunia ya sasa mitandaoni ndio sehemu kubwa ya kupatia maoni ya wananchi toka maeneo mbalimbali. Na uzuri huku mitandaoni watu wanafunguka vizuri kuliko huko mtaani wanakoweza kudhuriwa.
 
Ndio maana nasema hakuna athari hatuwezi kubadili tusiyoyataka kwa kupiga kelele za mitandaoni ambazo hazina athari huko mitaani.
 
Ndio maana nasema hakuna athari hatuwezi kubadili tusiyoyataka kwa kupiga kelele za mitandaoni ambazo hazina athari huko mitaani.

Mitandaoni pia ni mtaani boss, labda kama unadhani mitandaoni ni nje ya nchi. Huku mitandaoni ni mtaa digital.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…