ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,152
- 33,899
Nipe njia tatu bora za kupigania katibaTatizo katiba mpya wameachiwa wachache kana kwamba hilo lawahusu wao! NB: next year uwe mstari wa mbele kupigania katiba!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nipe njia tatu bora za kupigania katibaTatizo katiba mpya wameachiwa wachache kana kwamba hilo lawahusu wao! NB: next year uwe mstari wa mbele kupigania katiba!!
Nina wasiwasi na usemaji wako katika ukweli.
Mimi ni mmojawapo ambaye kupitia humu jamii forum, ndio nasoma vilio vingi kuhusu katiba,Vtu vingne husindikana kufanyika au uchelewa kufanyika kutokana na uhitaji wa mda uwo nazan katiba mpya inaweza ikawa inazungumziwa sana mitandaoni lakin sio kwa wananchi na kukutana na mijadala ya katiba mpya mtaani ni mara chache sana
Nazan kwa sasa uhitaji wa wananchi sio katiba mpya ila ni uongozi imara na utakao weza kujali maslai ya wananchi na nchi kwa ujumla
Tutatukanana na kuzalauliana sisi ambao tuko mitandaoni ila ukweli ni kwamba wananchi weng bado hawajawa tayari kwa katina mpya na akili yao haioko kwenye katiba na wananchi weng badi wanaamini mattzo yao hayatotatuliwa na katiba mpya
Kuna kitu kimoja wabongo tunashindwa kuelewa asilimia karibu 80% ya watanzania hawako mtandaoni wala hawana acces ya kupata habari muhimu au izo za katiba mpya
Tuache ku ignore ukwel wachache ndo wanajua na kufuatilia na habari za katiba mpya au ata mambo ya muhimu yanayoendelea nchini ila watanzania weng hawajui wala sio wafuatiliaji na apo ndo ugumu unapo anzia
Ntakupa mfano juzi limefunguliwa bwawa la nyerere ila watanzania weng hawajui km limekamilika kwa asilimia 78% weng wanajua ni 100% limekamilika
Watz weng hawajui litazalisha umeme kiasi gan na litatumia mga gan kujaa maji na linabeba lita gap za maji na kuanza uzalishaji wa umeme watz weng hawajui na wala hawajafuatilia kujua
Km kwel tunataka katiba mpya basi wale wenye uwelewa ni muda sasa kutoka mitandaoni na kuingia mtaani na vijijini kutoa elimu kwa wananchi, tuachane na hawa wananchi wa mitandaoni ni wacache na weng habari za katiba mpya wanzazo ila wanachi wa mtaani na vijijini hao hawana
Kutegemea wasomi kupata katiba mpya itakua ni ngumu sabu wasomi weng wa Tanzania ni maskini wa kipato hawana pesa na km huna pesa huwez kua na ushawishi wala huwezi kua na msimamo
Tupunguze maneno tulipe kodi ijenge nchiWanabodi,
Leo 30/12/2022 tunapoanza safari ya kuuaga mwaka 2022 hapo kesho na keshokutwa kuukaribisha mwaka mpya wa 2023 hivyo naomba nianze makala yangu hii ya "Kwa Maslahi ya Taifa" kwa kusema "kwaheri 2022, na Karibu 2023, kwa kuwatakia heri ya mwaka mpya 2023 in advance, kwa rai moja tuu, "Mwaka 2023, Tubadilike, Tufanye Kitu!"
Nimegundua sisi Watanzania, kwa jina letu maarufu la Wabongo ni watu wa maneno maneno mengi, kulalamika na na kulialia, lakini tukija kwenye matendo, Vitendo zero, sifuri, 0 nil!. Kwenye hili la Katiba, ni maneno maneno tuu, na kulia lia, ukiangalia matendo, ni hakuna kitu zaidi ya kelele!, makala ya leo ni ya swali, Jee na mwaka huu wa 2023, tuendeleze kulia lia kwa maneno maneno matupu au tubadilike tufanye vitendo, tufanye kitu, to do something, au tuendelee na maneno maneno na kulia lia tuu?.
Wengi huuanza mwaka mpya kwa kuweka malengo ya mwaka, “new year’s resolutions” kwamba mwaka huu nitafanya nini, ila katika kupanga hayo malengo, sii wengi hufanya mapitio ya mwaka ulioisha, walipanga kufanya nini, wametekeleza nini, wamefanikiwa nini na wamwkwama nini, ili baadhi yay ale malengo ya mwaka uliopita, ambayo hayakufanikiwa, yabebebwe katika mwaka unaofuata, au kama hayabebebi yafutwe, na sio kila mwaka unakuja na malengo mapya, mwisho wa mwaka hufanyi tathmini wala mapitio ya mwaka ulioisha, kisha unakuja na mengine mapya!, mwisho wa siku, unakuwa huwezi kupima mafanikio yako!.
Katiba ya nchi ndio Biblia ndio Msahafu wa uendeshaji wa nchi yetu. Kama ilivyo Ikulu ni mahali patakatifu, katiba ni kitabu kitakatifu kwa nchi yetu kama vilivyo vitabu vitakatifu vya Biblia Takatifu kwa Wakrusto na Quran Tukufu kwa Waislamu. Hii ndio sheria mama ya uendeshaji wa nchi yetu.
Tofauti pekee kati ya Biblia, Msahafu na Katiba, ni Msahafu haubadiliki, katiba inaweza kubadilishwa, ila mabadiliko yoyote ya katiba, lazima yawe ni mabadiliko halali ya haki.
Katiba ndio sheria kuu kuliko zote za nchi, viongozi wetu wakiisha chaguliwa, tunawaapisha kwa mujibu wa katiba, wanaapa kuilinda na kuitetea katiba ya JMT, na ikitokea hata rais wa JMT akikiuka katiba, anaondolewa madarakani!.
Sheria yoyote ikitungwa, ikiwa ni kinyume cha katiba, sheria hiyo inahesabika ni batili “null and void”, ikitungwa sheria ambayo ni batili, kwa kwenda kinyume cha katiba ya JMT, kisha ubatili huo, ukaja kuchomekewa ndani ya katiba yetu!, huku sasa tukuiteje?, maana kunakuwa sio kuibatilisha katiba, bali ni kuinajisi katiba!.
Mwaka 2022 tuliipigia kelele najisi fulani ndani ya katiba yetu kwa kulialia na kuisema sema, hivyo tumefika hadi mwisho wa mwaka 2022 bila jambo lolote la maana kufanyika kuiondoa najisi hii, sasa tumeingia mwaka mpya wa 2023, je na mwaka huu 2023, tuendelee tuu kupiga kelele kwa kulialia na kusema sema tuu, bila kufanya tendo lolote, au mwaka huu 2023, tubadilike, badala ya kulia lia na kusema sema, twende hatua moja zaidi mbele kwa kutenda kitu? ( msiwe na wasiwasi kuhusu kutenda huku, sio kwa mikutano ya hadhara au kufanya maandamano, ni kutenda kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni).
Maneno Maneno Yangu Kuhusu Najisi Kwenye Katiba Yetu ya 1977
Sisi Watanzania tuna fani mbalimbali, kuna wenzetu kazi yao ni kufikiri na kupanga mikakati, hawa wanaitwa think tanks, kuna wenzetu ni viongozi, kazi yao ni kutuongoza, kuna wenzetu ni watendakazi, kazi yao ni kutenda kazi kwa kutumia nguvu zao, kuna wengine tukiwemo sisi waandishi wa habari na vyombo vya habari, wa kiasili, yaani “traditional media” kazi zetu kuu ni tatu, kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, hatuna kutenda!. Na tumegawanyika makundi mawili, waandishi wa habari watangazaji na vyombo vya utangazaji (broadcast media) ambao kazi yao ni kutangaza na kuongea tuu, hakuna kutenda lolote!, na waandishi wa habari wa magazeti (print media) ambao kazi yao ni kuandika tuu hakuna kutenda lolote!.
- Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
- Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
- Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
- Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania
- Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
- Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
- Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
- Hukumu ya Mgombea Binafsi Juni 17, 2010
- "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
- Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!. kwa vile Rais Samia ameisha jitanabaisha yeye ni kama Magufuli, hivyo anapaswa kulitimiza na hili!.
Lakini ujio wa mapinduzi ya kidigitali kwenye dunia yetu na ujio wa mitandao ya kijamii, haya makundi mawili ya vyombo vya habari, yaani broadcast media na print media, yameunganishwa na mtandao wa jamii, hivyo kule kwenye mtandao, hakuna print peke yake wala broadcast peke yake. Vyombo vya utangazaji vina kurasa zake za mitandao ya kijamii navyo sasa vinaandika, mtu unaweza kusoma, vyombo vya print, kama magazeti, navyo kwenye kurasa zake, vinatangaza, na kuweka magazeti mtandao, hivyo siku hizi, kupata habari, kuangalia TV au kusoma gazeti, sio lazima ukae nyumbani uwashe TV uangalie habari, ukijisajili tuu na mtandao fulani, wanaita ku subscribe, unaletewa tuu habari, kila inapotokea, hivyo mtu hana tena haja kusubiria taarifa ya habari saa mbili usiku, kila tukio linapotokea linatangazwa live, hivyo kufikia ule muda wa habari, kila kilichotokea, watu wanakijua, magazeti ya kesho yake, sisi tunayasoma leo, maana kwenye kurasa zao za mitandao, kila habari, inachapishwa pale pale inapotokea.
Ujio huu wa mitandao ya jamii, umemfanya sasa kila mtu kuwa ni mwandishi wa habari, kila mtu sasa ni mtangazaji, hali inayopelekea hata sisi ambao ni watangazaji wa kweli wa kusomea hii kazi, kujikuta hatufui dafu mbele ya watangazaji vijana wa kisasa kwenye mitandao ya jamii, hivyo ukiwauliza vijana wa kisasa, unamjua Pasco Mayalla?, atakuuliza, Pascal Mayalla ndio nani?, utamwambia ni mtangazaji maarufu wa kipindi cha Kiti Moto, atakuuliza kiti moto ndio nini?, naomba link yake ni kitazame nikivutiwa, nita subscribe, unajikuta huna cha kumwambia!, hivyo sisi waandishi wakongwe wa ki analojia, ili tuendelee kuwepo ni lazima tubadilike na kwenda kidigitali vinginevyo tunafutika jumla!, hivyo mwaka 2023, Pasco Mayalla nae anakuja kidigitali zaidi!.
Hivyo kwa vile mimi kazi yangu ni kuandika tuu na kutangaza tuu, nikikaa chini na kuutafakari mwaka 2022, nimeandika mangapi na kutangaza mangapi, kuhusu katiba na yapi yamefanyiwa kazi, nimejikuta nimekata shauri kwa mwaka huu 2023, ili kulisaidia taifa na kuisaidia jamii, na kulisaidia taifa, nisiishie kuandika tuu, na kutangaza tuu, ninapaswa nifanye kitu cha ziada kwa kwenda mbele zaidi kwa kufanya jambo la ziada zaidi ya kuandika tuu na kutangaza tuu.
I must do something more!. Hii something more ni nini?, naomba kwa sasa nisiiseme baada ya kumuomba sana Mungu anifundishe kunyamaza, hivyo just watch me closely 2023!.
Ndipo yale maneno ya rais kijana wa Marekani, John F. Kennedy aliyowaeleza Wamarekani, “usijiulize Marekani imekufanyia nini, jiulize wewe umeifanyia nini Marekani?”. Hivyo tunapoukaribisha mwaka mpya, wa 2023, kama kila mmoja wetu atajitafakari kwa kujiuliza “jee ameifanyia nini Tanzania” akijikuta hajaifanyia kitu chochote cha maana huko nyuma, basi mwaka huu wa 2023, abadilike kwa kupanga malengo yenye mipango mkakati kwa kujiuliza, “jee ataifanyia nini Tanzania?”, Inawezekana kama kila mtu atatimiza wajibu wake kikamilifu.
Mwaka huu wa 2023, tupunguze maneno maneno, na kuongea ongea sana, tupunguze maandishi kuandika andika sana, hayo maneno maneno tunayoongea ongea sana, badaya ya kuishia kuongea ongea tuu, na kuandika andika tuu, tufanye jambo, tufanye na vitendo, tutende,!. Hivyo jambo langu kuu la kwanza kwa mwaka huu 2023 ni Katiba!. Japo kuna mambo mengi muhimu ya kuyashughulikia, lakini kwangu mimi kwa mwaka huu, naona muhimu kuliko yote ni hili la Katiba!, kwenye hili la Katiba, sasa tufanye kitu, tusiishie kuongea tuu na kuandika tuu, tufanye kitu cha ziada!, jee tufanye nini?, ungana nami wiki ijayo, nikiianzisha safari ya Katiba!, “it can be done, play your part” .
Kwa heri 2022, karibu 2023
Happy New Year!, Heri ya Mwaka Mpya!.
Paskali.
Akina nyie machafuko yenu humu mitandaoni tumeshayaona sana tu.Akina Sisi.
Lakini nyie wananchi tunaambiwa kuwa ndio mliyotaka wenyewe katiba mpya, maana yake mliweza kuona mapungufu ya katiba ya sasa?Mimi ni mmojawapo ambaye kupitia humu jamii forum, ndio nasoma vilio vingi kuhusu katiba,
Lakini ambacho nasoma ni kuwa tunataka katiba mmpya, au kitu fulani kimekuwa hivi sababu ya hii katiba,.
Lakini wakati mwengine nasikia hata katiba hihii ambayo tunayo inavunjwa au kukiukwa na hakuna kinachofanyika,
Sasa je hiyo katiba tunaitaka itafanyaje mpaka isivunjwe kama hii ambayo tunayo?,
Mimi nadhani umefika wakati kwa wajuzi wa humu kuanza kutuonyesha udhaifu wa katiba hii na umuhimu wa katiba mpya kama somo ili kutuondolea ujinga huu ambao tunao ili hata na mimi nikiulizwa kuhusu ubovu wa katiba hii iwe rahisi kuelezea .
Paschal nakutegemea uanze kutupa Elimu hii.
Na utuelewesha namna katiba mpya isivyoweza kuvunjwa kama hii,
Maana wakati unaweza kuzani kwamba tunahitaji katiba saana, kumbe ni uvunjaji wa sheria tu.
Mkuu tamsana, kwenye hili la katiba, sijananga mtu!.Mkuu wewe binafsi umetoa mchango gani katika kufanikisha upatikanaji wa katiba mpya? Tatizo hili jukumu tumewaachia baadhi ya vyama vya upinzani. Sisi wengine tunawatazama tu na mwisho wa siku tunakuja na mabandiko kama haya kuwananga wapinzani.
Akina nyie machafuko yenu humu mitandaoni tumeshayaona sana tu.
Kipi mlihamasishana mitandaoni athari yake ikaonekana huku mitaani?Huku mitandaoni ni sehemu ya kuhamasishana maana watu wataumia, au unadhani maandamano dhidi ya jambo lisilopendwa na serikali ni sawa na maandamano ya kumbukumbu ya moyo mtakatifu wa Yesu?
Mimi binafsi, hayo mapungufu ya katiba iliyopo bado sijaambiwa na siyajui,Lakini nyie wananchi tunaambiwa kuwa ndio mliyotaka wenyewe katiba mpya, maana yake mliweza kuona mapungufu ya katiba ya sasa?
Kipi mlihamasishana mitandaoni athari yake ikaonekana huku mitaani?
Naunga mkono hoja, the powers now lies with mitandao!, jambo likiuliziwa mitandaoni, serikali inakuja kulijibu rasmi.Unauliza au unapigia jibu mstari? Husikii mara kwa mara serikali ikitoa ufafanuzi huku ikisema kutokana na maoni yaliyoko mitandaoni? Kwani siku hizi serikali inasikilizia wapi maoni ya wananchi zaidi ya mitandaoni. Ama unataka kujitoa ufahamu?
Mfano punguzo la tozo za miamala ya simu. Ufafanuzi kuhusu mabewa ya treni huku viongozi wa serikali wakipishana kauli kutokana na shinikizo la wanaohoji kuhusu mabehewa hayo huku mitandaoni. Au umewahi kuona watu wamekutana mahali wakifanya mkutano kutaka wapewe majibu ya mabehewa kubwa ni mapya au mtumba zaidi ya mitandaoni? Na kama mitandao haina impact hiyo, kwanini wakati wa uchaguzi mkuu mitandao ya kijamii ilizimwa?
Nimeuliza kuhusu kuhamasishana kwamba mkahamasishana kufanya jambo na kweli tukaona matokeo huku mitaani, sio kujadili jambo tu mtandaoni.Unauliza au unapigia jibu mstari? Husikii mara kwa mara serikali ikitoa ufafanuzi huku ikisema kutokana na maoni yaliyoko mitandaoni? Kwani siku hizi serikali inasikilizia wapi maoni ya wananchi zaidi ya mitandaoni. Ama unataka kujitoa ufahamu?
Mfano punguzo la tozo za miamala ya simu. Ufafanuzi kuhusu mabewa ya treni huku viongozi wa serikali wakipishana kauli kutokana na shinikizo la wanaohoji kuhusu mabehewa hayo huku mitandaoni. Au umewahi kuona watu wamekutana mahali wakifanya mkutano kutaka wapewe majibu ya mabehewa kubwa ni mapya au mtumba zaidi ya mitandaoni? Na kama mitandao haina impact hiyo, kwanini wakati wa uchaguzi mkuu mitandao ya kijamii ilizimwa?
Nimeuliza kuhusu kuhamasishana kwamba mkahamasishana kufanya jambo na kweli tukaona matokeo huku mitaani, sio kujadili jambo tu mtandaoni.
Mangapi yamelalamikiwa humu mitandaoni na bado serikali inayapotezea?
Nasema imeyapotezea kwa maana hata ya kutoyatolea ufafanuzi au wakati mwengine kutolea majibu ya dharau kwa kuonekana ni kelele za mitandaoni tu.Kwani hiyo serikali imetekeleza yale yote inayoyataka hadi useme imeyapotezea yaliyolalamikiwa tu huku mitandaoni?
Nasema imeyapotezea kwa maana hata ya kutoyatolea ufafanuzi au wakati mwengine kutolea majibu ya dharau kwa kuonekana ni kelele za mitandaoni tu.
Kimsingi huku mitandaoni hatuna nguvu hiyo mnayofikiri tunayo.
Ndio maana nasema hakuna athari hatuwezi kubadili tusiyoyataka kwa kupiga kelele za mitandaoni ambazo hazina athari huko mitaani.Ukiona hawajajibu ujue hawana majibu, na wakijibu kwa dharau ujue sababu ni uwezo wao mdogo. Vyovyote iwavyo kwa dunia ya sasa mitandaoni ndio sehemu kubwa ya kupatia maoni ya wananchi toka maeneo mbalimbali. Na uzuri huku mitandaoni watu wanafunguka vizuri kuliko huko mtaani wanakoweza kudhuriwa.
Ndio maana nasema hakuna athari hatuwezi kubadili tusiyoyataka kwa kupiga kelele za mitandaoni ambazo hazina athari huko mitaani.