Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?

Katiba Mpya ni jukumu letu sote. Hili la kuwa sisi hamna kutenda ni kujaribu kujivua uwajibikaji kiaina lengo likiwa kula matunda bila kuyafanyia kazi. Yaani playing safe.
 
Wanabodi,

I must do something more!. Hii something more ni nini?, naomba kwa sasa nisiiseme baada ya kumuomba sana Mungu anifundishe kunyamaza, hivyo just watch me closely 2023!.
Paskali.
Wanabodi, kwa trends hizi ninazoziona za political dynamism ya siasa zetu, naiona kabisa katiba mpya bora hapa mbele ya macho yangu, its just around the corner!, hivyo sasa naanza kujiuliza if there is a still a need to do something more, or just kuacha tuu mambo mazuri yatokee yenyewe naturally na sìo kwa mashinokizo!.
P
 
Ww ni kama umeshajisalimishwa kwa dola, hivyo utadai katiba kwa njia ya maongezi, wakati hakuna uwezekano wa kupatikana katiba mpya ya kweli bila machafuko.
Mkuu Tindo , nakusalimia tuu!. Mimi nimejisalimisha kwa dola, tunaidai katiba mpya kwa mazungumzo, wipi wewe mwemzangu, bado unaamini kupata katiba mpya ni lazima kwa machafuko?.
P
 
Watanzania buana!, ukiwasikia jinsi walivyo wakali kwenye kupigania maslahi ya taifa, utadhani ni wapiganaji kweli!, na unaweza kuogopa kwa kudhani wanaweza kufanya kitu!, kumbe hawana lolote!, ni maneno maneno matupu!. Hawanaga uwezo wa kufanya lolote!.

Hivyo hata hili la ukodishaji wa Bandari yetu kwa Mwarabu wa Dubai, kilichoamuliwa na serikali yetu makini, ndicho chenyewe, Bunge letu tukufu litaridhia, maisha yaendelee
P
P
 
Na huo ndio ukweli mchungu. !!
 
Wee mbowe anatoa tamko eti patachimbika wakati huo akiongea kajifungia kwenye chumba huko Ulaya . Unatoa matamko kwa zoom. Hakuna mapambano ya ivyo hata siku moja. Acha tujaribu na mwarabu kama Waswahili Wenzetu wameshindwa
 
Hata hili la IGA ya Tanzania na Dubai kuhusu DPW kutuendeshea Bandari yetu, ni maneno maneno matupu mengi!.
IGA imepelekwa Bungeni ikiwa tayari iliishasainiwa toka October 2022, hivyo the role of Bunge ni kuridhia tuu, rubber stamp na sio kuidhinisha!. Bunge limeijadili hiyo IGA ya DPW na kuiridhia vile vile ilivyo!, kitu ambacho ni rubber stamping!.

Lets fight for reforms, kwenye mikataba ya rasilimali muhimu za taifa, the role ya Bunge isiwe kuridhia, ratification ili kui domesticate, bali Bunge liidhinishe mikataba hiyo!.

Lets do something na sio maneno maneno matupu!.
P
 
Wee mbowe anatoa tamko eti patachimbika wakati huo akiongea kajifungia kwenye chumba huko Ulaya . Unatoa matamko kwa zoom. Hakuna mapambano ya ivyo hata siku moja. Acha tujaribu na mwarabu kama Waswahili Wenzetu wameshindwa

Why mbowe aje awapiganie? Watanzania mmeshindwa kusimama kwa miguu yenu hadi mbowe aje?

Anachofanya mbowe ni uhamasishaji, lakini sasa jamii anayo ihamasisha ni ya mdomoni, matendo 0.
Atatokaje kama wahusika wenyewe hamtoki?
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Thubutu....hizo reforms hamwezi fanya labda Ccm ikubali, jambo ambalo ni ndoto.

Kubalini tu ukweli, Tz na raia wake ni mali binafsi ya Ccm.....mali haiwezi kuwa mkubwa kuliko mmiliki wake.
 
Katiba mpya bora ndio muarobaini wa mengi kama sio yote. !! Naamini hata yule Mheshimiwa wa karibu na Kibaigwa analijua hili !!
 
Katiba mpya bora ndio muarobaini wa mengi kama sio yote. !! Naamini hata yule Mheshimiwa wa karibu na Kibaigwa analijua hili !!
Inaweza kuwepo katiba mpya na wasiifatilie vilevile
Kikubwa ni kutii,kuheshimu,kusimamia sheria

Ova
 
Thubutu....hizo reforms hamwezi fanya labda Ccm ikubali, jambo ambalo ni ndoto.

Kubalini tu ukweli, Tz na raia wake ni mali binafsi ya Ccm.....mali haiwezi kuwa mkubwa kuliko mmiliki wake.
Ni Ukweli unaokaribia asilimia 80 ! Watu wengi wanaamini hivyo vyote vinavyogombewa ni kwa maslahi ya wanasiasa na wafanyakazi wa kwenye maeneo husika !!

Wengi wanaamini kinachowahusu wao ni kile wanachokipata kwenye shughuli zao za kila siku za kujipatia riziki ! Mengine it’s none of their business !!
 
Kama wanaamini hivyo basi ni wajinga .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…