Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?

Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?

Wanabodi,
View attachment 2473473View attachment 2473476

Leo 30/12/2022 tunapoanza safari ya kuuaga mwaka 2022 hapo kesho na keshokutwa kuukaribisha mwaka mpya wa 2023 hivyo naomba nianze makala yangu hii ya "Kwa Maslahi ya Taifa" kwa kusema "kwaheri 2022, na Karibu 2023, kwa kuwatakia heri ya mwaka mpya 2023 in advance, kwa rai moja tuu, "Mwaka 2023, Tubadilike, Tufanye Kitu!"

Nimegundua sisi Watanzania, kwa jina letu maarufu la Wabongo ni watu wa maneno maneno mengi, kulalamika sana na kulialia lia mwingi!, lakini tukija kwenye matendo, actions na kuchukua hatua, kusema ukweli kabisa, vitendo ni sifuri, zero, 0 nil!.

Kwenye hili la Katiba, Watanzania ni maneno maneno tuu meengii, na kulia lia kwingi!, lakini ukiangalia kwenye matendo, kuchukua hatua, to take actions ni hakuna kitu zaidi ya kelele!. Makala ya leo ni ya swali, huko nyuma tumekuwa tukipiga sana kelele miaka nenda, miaka rudi!, je na mwaka huu wa 2023, tuendeleze kulia lia kwa kupiga kelele kwa maneno maneno matupu au tubadilike tufanye vitendo, tuchukue hatua, tufanye kitu?. Yaani we have to do something!, au tuendelee tuu na maneno maneno, kulia lia na kupiga tuu kelele?.

Wengi huuanza mwaka mpya kwa kuweka malengo ya mwaka, “new year’s resolutions” kwamba mwaka huu nitafanya hili na lile, ila katika kupanga hayo malengo, sii wengi hufanya mapitio ya mwaka ulioisha, walipanga kufanya nini, wametekeleza nini, wamefanikiwa nini na wamekwama nini, ili baadhi ya yale malengo ya mwaka uliopita, ambayo hayakufanikiwa, yabebebwe katika mwaka unaofuata, au kama hayabebeki yafutwe, na sio kila mwaka unakuja na malengo mapya, mwisho wa mwaka hufanyi tathmini wala mapitio ya mwaka ulioisha, kisha unakuja na mengine mapya!, mwisho wa siku, unakuwa huwezi kupima mafanikio yako!.

Katiba ya nchi ndio Biblia ndio Msahafu wa uendeshaji wa nchi yetu. Kama ilivyo Ikulu ni mahali patakatifu, katiba ni kitabu kitakatifu kwa nchi yetu kama vilivyo vitabu vitakatifu vya Biblia Takatifu kwa Wakrusto na Quran Tukufu kwa Waislamu. Hii ndio sheria mama ya uendeshaji wa nchi yetu.

Tofauti pekee kati ya Biblia, Msahafu na Katiba, ni Msahafu haubadiliki, katiba inaweza kubadilishwa, ila mabadiliko yoyote ya katiba, lazima yawe ni mabadiliko halali ya haki.

Katiba ndio sheria kuu kuliko zote za nchi, viongozi wetu wakiisha chaguliwa, tunawaapisha kwa mujibu wa katiba, wanaapa kuilinda na kuitetea katiba ya JMT, na ikitokea hata rais wa JMT akikiuka katiba, anaondolewa madarakani!.

Sheria yoyote ikitungwa, ikiwa ni kinyume cha katiba, sheria hiyo inahesabika ni batili “null and void”, ikitungwa sheria ambayo ni batili, kwa kwenda kinyume cha katiba ya JMT, kisha ubatili huo, ukaja kuchomekewa ndani ya katiba yetu!, huku sasa tukuiteje?, maana kunakuwa sio kuibatilisha katiba, bali ni kuinajisi katiba!.

Mwaka 2022 tuliipigia kelele najisi fulani ndani ya katiba yetu kwa kulialia na kuisema sema, hivyo tumefika hadi mwisho wa mwaka 2022 bila jambo lolote la maana kufanyika kuiondoa najisi hii, sasa tumeingia mwaka mpya wa 2023, je na mwaka huu 2023, tuendelee tuu kupiga kelele kwa kulialia na kusema sema tuu, bila kufanya tendo lolote, au mwaka huu 2023, tubadilike, badala ya kulia lia na kusema sema, twende hatua moja zaidi mbele kwa kutenda kitu? ( msiwe na wasiwasi kuhusu kutenda huku, sio kwa mikutano ya hadhara au kufanya maandamano, ni kutenda kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni).
Maneno Maneno Yangu Kuhusu Najisi Kwenye Katiba Yetu ya 1977
  1. Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli
  2. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  3. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  4. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  5. Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
  6. Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania
  7. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
  8. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  9. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
  10. Hukumu ya Mgombea Binafsi Juni 17, 2010
  11. "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
  12. Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!. kwa vile Rais Samia ameisha jitanabaisha yeye ni kama Magufuli, hivyo anapaswa kulitimiza na hili!.
Sisi Watanzania tuna fani mbalimbali, kuna wenzetu kazi yao ni kufikiri na kupanga mikakati, hawa wanaitwa think tanks, kuna wenzetu ni viongozi, kazi yao ni kutuongoza, kuna wenzetu ni watendakazi, kazi yao ni kutenda kazi kwa kutumia nguvu zao, kuna wengine tukiwemo sisi waandishi wa habari na vyombo vya habari, wa kiasili, yaani “traditional media” kazi zetu kuu ni tatu, kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, hatuna kutenda!. Na tumegawanyika makundi mawili, waandishi wa habari watangazaji na vyombo vya utangazaji (broadcast media) ambao kazi yao ni kutangaza na kuongea tuu, hakuna kutenda lolote!, na waandishi wa habari wa magazeti (print media) ambao kazi yao ni kuandika tuu hakuna kutenda lolote!.

Lakini ujio wa mapinduzi ya kidigitali kwenye dunia yetu na ujio wa mitandao ya kijamii, haya makundi mawili ya vyombo vya habari, yaani broadcast media na print media, yameunganishwa na mtandao wa jamii, hivyo kule kwenye mtandao, hakuna print peke yake wala broadcast peke yake. Vyombo vya utangazaji vina kurasa zake za mitandao ya kijamii navyo sasa vinaandika, mtu unaweza kusoma, vyombo vya print, kama magazeti, navyo kwenye kurasa zake, vinatangaza, na kuweka magazeti mtandao, hivyo siku hizi, kupata habari, kuangalia TV au kusoma gazeti, sio lazima ukae nyumbani uwashe TV uangalie habari, ukijisajili tuu na mtandao fulani, wanaita ku subscribe, unaletewa tuu habari, kila inapotokea, hivyo mtu hana tena haja kusubiria taarifa ya habari saa mbili usiku, kila tukio linapotokea linatangazwa live, hivyo kufikia ule muda wa habari, kila kilichotokea, watu wanakijua, magazeti ya kesho yake, sisi tunayasoma leo, maana kwenye kurasa zao za mitandao, kila habari, inachapishwa pale pale inapotokea.

Ujio huu wa mitandao ya jamii, umemfanya sasa kila mtu kuwa ni mwandishi wa habari, kila mtu sasa ni mtangazaji, hali inayopelekea hata sisi ambao ni watangazaji wa kweli wa kusomea hii kazi, kujikuta hatufui dafu mbele ya watangazaji vijana wa kisasa kwenye mitandao ya jamii, hivyo ukiwauliza vijana wa kisasa, unamjua Pasco Mayalla?, atakuuliza, Pascal Mayalla ndio nani?, utamwambia ni mtangazaji maarufu wa kipindi cha Kiti Moto, atakuuliza kiti moto ndio nini?, naomba link yake ni kitazame nikivutiwa, nita subscribe, unajikuta huna cha kumwambia!, hivyo sisi waandishi wakongwe wa ki analojia, ili tuendelee kuwepo ni lazima tubadilike na kwenda kidigitali vinginevyo tunafutika jumla!, hivyo mwaka 2023, Pasco Mayalla nae anakuja kidigitali zaidi!.

Hivyo kwa vile mimi kazi yangu ni kuandika tuu na kutangaza tuu, nikikaa chini na kuutafakari mwaka 2022, nimeandika mangapi na kutangaza mangapi, kuhusu katiba na yapi yamefanyiwa kazi, nimejikuta nimekata shauri kwa mwaka huu 2023, ili kulisaidia taifa na kuisaidia jamii, na kulisaidia taifa, nisiishie kuandika tuu, na kutangaza tuu, ninapaswa nifanye kitu cha ziada kwa kwenda mbele zaidi kwa kufanya jambo la ziada zaidi ya kuandika tuu na kutangaza tuu.

I must do something more!. Hii something more ni nini?, naomba kwa sasa nisiiseme baada ya kumuomba sana Mungu anifundishe kunyamaza, hivyo just watch me closely 2023!.

Ndipo yale maneno ya rais kijana wa Marekani, John F. Kennedy aliyowaeleza Wamarekani, “usijiulize Marekani imekufanyia nini, jiulize wewe umeifanyia nini Marekani?”. Hivyo tunapoukaribisha mwaka mpya, wa 2023, kama kila mmoja wetu atajitafakari kwa kujiuliza “jee ameifanyia nini Tanzania” akijikuta hajaifanyia kitu chochote cha maana huko nyuma, basi mwaka huu wa 2023, abadilike kwa kupanga malengo yenye mipango mkakati kwa kujiuliza, “jee ataifanyia nini Tanzania?”, Inawezekana kama kila mtu atatimiza wajibu wake kikamilifu.

Mwaka huu wa 2023, tupunguze maneno maneno, na kuongea ongea sana, tupunguze maandishi kuandika andika sana, hayo maneno maneno tunayoongea ongea sana, badaya ya kuishia kuongea ongea tuu, na kuandika andika tuu, tufanye jambo, tufanye na vitendo, tutende,!. Hivyo jambo langu kuu la kwanza kwa mwaka huu 2023 ni Katiba!. Japo kuna mambo mengi muhimu ya kuyashughulikia, lakini kwangu mimi kwa mwaka huu, naona muhimu kuliko yote ni hili la Katiba!, kwenye hili la Katiba, sasa tufanye kitu, tusiishie kuongea tuu na kuandika tuu, tufanye kitu cha ziada!, jee tufanye nini?, ungana nami wiki ijayo, nikiianzisha safari ya Katiba!, “it can be done, play your part” .
Kwa heri 2022, karibu 2023
Happy New Year!, Heri ya Mwaka Mpya!.
Paskali.
Katiba Mpya ni jukumu letu sote. Hili la kuwa sisi hamna kutenda ni kujaribu kujivua uwajibikaji kiaina lengo likiwa kula matunda bila kuyafanyia kazi. Yaani playing safe.
 
Wanabodi,

I must do something more!. Hii something more ni nini?, naomba kwa sasa nisiiseme baada ya kumuomba sana Mungu anifundishe kunyamaza, hivyo just watch me closely 2023!.
Paskali.
Wanabodi, kwa trends hizi ninazoziona za political dynamism ya siasa zetu, naiona kabisa katiba mpya bora hapa mbele ya macho yangu, its just around the corner!, hivyo sasa naanza kujiuliza if there is a still a need to do something more, or just kuacha tuu mambo mazuri yatokee yenyewe naturally na sìo kwa mashinokizo!.
P
 
Ww ni kama umeshajisalimishwa kwa dola, hivyo utadai katiba kwa njia ya maongezi, wakati hakuna uwezekano wa kupatikana katiba mpya ya kweli bila machafuko.
Mkuu Tindo , nakusalimia tuu!. Mimi nimejisalimisha kwa dola, tunaidai katiba mpya kwa mazungumzo, wipi wewe mwemzangu, bado unaamini kupata katiba mpya ni lazima kwa machafuko?.
P
 
Wanabodi,

Nimegundua sisi Watanzania, kwa jina letu maarufu la Wabongo ni watu wa maneno maneno mengi, kulalamika sana na kulialia lia mwingi!, lakini tukija kwenye matendo, actions na kuchukua hatua, kusema ukweli kabisa, vitendo ni sifuri, zero, 0 nil!.

Paskali.
Watanzania buana!, ukiwasikia jinsi walivyo wakali kwenye kupigania maslahi ya taifa, utadhani ni wapiganaji kweli!, na unaweza kuogopa kwa kudhani wanaweza kufanya kitu!, kumbe hawana lolote!, ni maneno maneno matupu!. Hawanaga uwezo wa kufanya lolote!.

Hivyo hata hili la ukodishaji wa Bandari yetu kwa Mwarabu wa Dubai, kilichoamuliwa na serikali yetu makini, ndicho chenyewe, Bunge letu tukufu litaridhia, maisha yaendelee

Na huo ndio ukweli mchungu. !!
 
Wee mbowe anatoa tamko eti patachimbika wakati huo akiongea kajifungia kwenye chumba huko Ulaya . Unatoa matamko kwa zoom. Hakuna mapambano ya ivyo hata siku moja. Acha tujaribu na mwarabu kama Waswahili Wenzetu wameshindwa
 
Wanabodi,

rai moja tuu, "Mwaka 2023, Tubadilike, Tufanye Kitu!"

Nimegundua sisi Watanzania, kwa jina letu maarufu la Wabongo ni watu wa maneno maneno mengi, kulalamika sana na kulialia lia mwingi!, lakini tukija kwenye matendo, actions na kuchukua hatua, kusema ukweli kabisa, vitendo ni sifuri, zero, 0 nil!.

Ndipo yale maneno ya rais kijana wa Marekani, John F. Kennedy aliyowaeleza Wamarekani, “usijiulize Marekani imekufanyia nini, jiulize wewe umeifanyia nini Marekani?”. Hivyo tunapoukaribisha mwaka mpya, wa 2023, kama kila mmoja wetu atajitafakari kwa kujiuliza “jee ameifanyia nini Tanzania” akijikuta hajaifanyia kitu chochote cha maana huko nyuma, basi mwaka huu wa 2023, abadilike kwa kupanga malengo yenye mipango mkakati kwa kujiuliza, “jee ataifanyia nini Tanzania?”, Inawezekana kama kila mtu atatimiza wajibu wake kikamilifu.

Mwaka huu wa 2023, tupunguze maneno maneno, na kuongea ongea sana, tupunguze maandishi kuandika andika sana, hayo maneno maneno tunayoongea ongea sana, badala ya kuishia kuongea ongea tuu, na kuandika andika tuu, tufanye jambo, tufanye na vitendo, tutende,!.
Paskali.
Hata hili la IGA ya Tanzania na Dubai kuhusu DPW kutuendeshea Bandari yetu, ni maneno maneno matupu mengi!.
IGA imepelekwa Bungeni ikiwa tayari iliishasainiwa toka October 2022, hivyo the role of Bunge ni kuridhia tuu, rubber stamp na sio kuidhinisha!. Bunge limeijadili hiyo IGA ya DPW na kuiridhia vile vile ilivyo!, kitu ambacho ni rubber stamping!.

Lets fight for reforms, kwenye mikataba ya rasilimali muhimu za taifa, the role ya Bunge isiwe kuridhia, ratification ili kui domesticate, bali Bunge liidhinishe mikataba hiyo!.

Lets do something na sio maneno maneno matupu!.
P
 
Wee mbowe anatoa tamko eti patachimbika wakati huo akiongea kajifungia kwenye chumba huko Ulaya . Unatoa matamko kwa zoom. Hakuna mapambano ya ivyo hata siku moja. Acha tujaribu na mwarabu kama Waswahili Wenzetu wameshindwa

Why mbowe aje awapiganie? Watanzania mmeshindwa kusimama kwa miguu yenu hadi mbowe aje?

Anachofanya mbowe ni uhamasishaji, lakini sasa jamii anayo ihamasisha ni ya mdomoni, matendo 0.
Atatokaje kama wahusika wenyewe hamtoki?
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Hata hili la IGA ya Tanzania na Dubai kuhusu DPW kutuendeshea Bandari yetu, ni maneno maneno matupu mengi!.
IGA imepelekwa Bungeni ikiwa tayari iliishasainiwa toka October 2022, hivyo the role of Bunge ni kuridhia tuu, rubber stamp na sio kuidhinisha!. Bunge limeijadili hiyo IGA ya DPW na kuiridhia vile vile ilivyo!, kitu ambacho ni rubber stamping!.

Lets fight for reforms, kwenye mikataba ya rasilimali muhimu za taifa, the role ya Bunge isiwe kuridhia, ratification ili kui domesticate, bali Bunge liidhinishe mikataba hiyo!.

Lets do something na sio maneno maneno matupu!.
P
Thubutu....hizo reforms hamwezi fanya labda Ccm ikubali, jambo ambalo ni ndoto.

Kubalini tu ukweli, Tz na raia wake ni mali binafsi ya Ccm.....mali haiwezi kuwa mkubwa kuliko mmiliki wake.
 
Katiba mpya bora ndio muarobaini wa mengi kama sio yote. !! Naamini hata yule Mheshimiwa wa karibu na Kibaigwa analijua hili !!
 
Katiba mpya bora ndio muarobaini wa mengi kama sio yote. !! Naamini hata yule Mheshimiwa wa karibu na Kibaigwa analijua hili !!
Inaweza kuwepo katiba mpya na wasiifatilie vilevile
Kikubwa ni kutii,kuheshimu,kusimamia sheria

Ova
 
Thubutu....hizo reforms hamwezi fanya labda Ccm ikubali, jambo ambalo ni ndoto.

Kubalini tu ukweli, Tz na raia wake ni mali binafsi ya Ccm.....mali haiwezi kuwa mkubwa kuliko mmiliki wake.
Ni Ukweli unaokaribia asilimia 80 ! Watu wengi wanaamini hivyo vyote vinavyogombewa ni kwa maslahi ya wanasiasa na wafanyakazi wa kwenye maeneo husika !!

Wengi wanaamini kinachowahusu wao ni kile wanachokipata kwenye shughuli zao za kila siku za kujipatia riziki ! Mengine it’s none of their business !!
 
Kama wanaamini hivyo basi ni wajinga .
 
Back
Top Bottom