Watanzania ni masikini kwa kuukubali umasikini wa mawazo, tubadilike! Changamkia fursa hii

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Naomba nianze kwa kuwakumbusha maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kuwa Umasikini mbaya kabisa ni umasikini wa mawazo!, kuwaza kimasikini, kujikubali kuwa sisi ni masikini, na kiukweli tumekuja kuwa masikini kweli!. Sasa ni wakati wa kubadilika, tusijikubali tena kuwa sisi ni masikini, tuachane na mawazo ya kimasikini na kuukubali umasikini!.

Total Tanzania wametuletea fursa hii ya kutajirika, tuichangamkie!, naamini wako Watanzania wengi tuu wenye mawazo mazuri ya kibiashara, tatizo lao ni mitaji!. Hii sasa ni fursa kwa mwenye wazo zuri, kampuni ya Total itampa mtaji!.

Tuchangamkie furrsa hii.

[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD="width: 516"][TABLE="align: center"]
[TR]
[TD="width: 516, align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 516, align: left"] Total Tanzania, Kuibua Vipaji vya Ubunifu wa Miradi na Kutoa Mitaji...
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 40"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Paskali
 
Wangapi wanaweza kuandika mawazo ya biashara? Elimu yetu ilisha tu knock out kwenye fursa kama hizi. Napita tu maana kichwani nna disorganised ideas kama 500 hv
 
Wangapi wanaweza kuandika mawazo ya biashara? Elimu yetu ilisha tu knock out kwenye fursa kama hizi. Napita tu maana kichwani nna disorganised ideas kama 500 hv
organize them, choose one with the biggest impact, then try it, hata Bill gates alianza hivi.

Pasco
 
mbona hiyo link haifunguki au umeweka vibay a maan anaifungua haifunguki hawana website ingine hao
 
mbona hiyo link haifunguki au umeweka vibay a maan anaifungua haifunguki hawana website ingine hao
Dar es Salaam, Novemba 9, 2015

TOTAL TANZANIA YAZINDUA SHINDANO LA ? STARTUPPER OF THE YEAR BY TOTAL ?

Kampuni ya Total ya Tanzania, yazindua Shindano la Total ?Startupper of the year by Total?, lililobuniwa na kundi la Makampuni ya Total litakaloshirikisha nchi 34 za Afrika kwa wakati mmoja. Shindano hilo linalenga katika kutambua, kuzawadia na kuwezesha utekelezaji wa miradi bora ya biashara ya ujasiliamali inayoanza au iliyobuniwa chini ya miaka miwili kwa ajili ya maendeleo ya jamii na taifa. Washindi wa miradi bora watapewa tuzo ya ? Startupper of the year 2016 by Total ? itakayoambatana na fedha taslimu itakayotumika kama mtaji wa kuendeleza, na kusimamia uendeshaji wa miradi hiyo.

Shidano hili ni bure kwa raia wote wa Watanzania wenye umri kati ya miaka kumi na nane( (18) hadi miaka thelathini na tano (35).

Fomu za maombi zimeanza kutolewa kuanzia tarehe 1 Novemba 2015 saa 2:00 asubuhi kwenye tovuti: http://startupper.total.com/. Shindano litakuwa wazi hadi Januari 31, 2016 saa 5:00 asubuhi ambapo ndio mwisho wa kurejesha fomu.

Jopo la Majaji linalohusisha wataalamu wa biashara, litachagua miradi kumi bora nchini Tanzania itakayoingia fainali kwa kuzingatia vigezo vya ubunifu, uhalisia na uwezo wa mradi katika kuleta maendeleo na kuboresha hali ya maisha ya jamii kubwa ya Watanzania.


Orodha ya washindi watakaoingia fainali itachapishwa tarehe 28, Februari, 2016 katika tovuti ile ile walipochukulia fomu za kugombea.

Kuanzia tarehe 15 Machi, 2016, Washindi hao kumi, wataingia katika mchuano wa fainali kutafuta tatu bora ambapo washindi watawajibika kuitetea miradi yao mbele ya jopo la majaji ili kupata miradi mitatu bora ambapo mshindi wa jumla atatangazwa na kupewa zawadi katika hafla maalum ya utoaji wa tuzo.


Sheria, taratibu, kanuni na vigezo vya shindano hili zinapatikana bure kwenye tovuti ya (http://startupper.total.com/).

Shindano la
? Startupper of the year by Total ? ni juhudi za Kampuni ya kimataifa ya Total katika kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ili kusaidia nchi zote duniani ambako kampuni ya Total ipo. Shindano hili ni hatua madhubuti yenye lengo la kuvumbua ubunifu wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kuchangia uanzishwaji wa viwanda vidogo vitakavyotoa ajira na kuchangia maendeleo ya jamii na ya nchi za bara la Afrika kwa ujumla. Shindano hili linalenga kuibua miradi mipya, iliyotokana na wananchi wenyewe ambayo inaendana na malengo ya jumla ya uwepo wa kampuni ya Total.

Kwa mawasiliano zaidi, Wasiliana na: Jamila Tindwa,

255 786 999 296

Kuhusu Kampuni ya Total
Total ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi na ni moja ya kampuni ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote. Ina wafanyakazi 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.

Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha ya watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika.
Total imeanzisha mradi kabambe wa utafutaji na uzalishaji wa mafuta kwa kuongeza idadi ya visima vya mafuta huku ikijitahidi kupata nishati endelevu kwa ajili ya Bara la Afrika kwa sasa na baadae. Total imejikita katika uhamasishaji wa utafutaji vya vyanzo vipya vya nishati kwa kutoa kipaumbele cha elimu ya nishati kwa vijana ili kuendeleza uwezo wa kipekee wa bara la Afika kujiletea maendeleo. Mbali na hilo, Kampuni ya Total ndio msambazaji wa kwanza wa bidhaa za mafuta (mafuta ya petroli, dizeli, mafuta ya taa , lami, na GPL, nk) katika bara la Afrika.
Total tunajivunia historia yetu, ubora wa bidhaa na huduma zetu, katika jumla ya vituo 4200 vya mafuta katika nchi arobaini barani Afrika. Vituo vya mafuta vya Total ni vituo tegemeo kwa wafanya biashara binafsi na wateja wake. Lengo letu ni kuwezesha upatikanaji mkubwa zaidi wa nishati, ambayo pia inahusisha kuendeleza upatikani wa vyanzo vingi na mbadala vya nishati na kwa gharama nafuu - kama vile nishati ya jua, kwa kuuza vifaa vya nishati ya jua.
Total tunasikiliza mahitaji ya wadau wetu, na kwenda pamoja nao katika kuleta maendeleo ya kiuchumi, ajira, elimu na afya

www.total.com

Kuhusu
Total Tanzania
Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliyoingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli, vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo huuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum " Total Fuel Card" kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali za magari katika vituo vya mafuta vya Total. Katika kujitanua zaidi kibiashara kuelekea kwenye matumizi ya nishati mbadala, kampuni ya Total Tanzania kupitia mradi wake wa
Total Access to Solar (TATS), inasambaza taa za nishati ya jua zinazoitwa "Awango by Total" kwa jamii ya Watanzania.


 
asante sana kaka Pascal Mayalla nitaijitahidi kwenda kuchukua fomu nijaze ubarikiwe
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…