Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Busta Rhymes akichengua wabongo kwenye Fiesta Tuesday, November 24, 2009 8:00 AM
MSANII mkongwe wa Hip Hop kutoka Marekani, Busta Rhymes amesema kuwa ameridhishwa na ukarimu wa Watanzania hali inayomfanya afikirie kuitangaza Tanzania kwa wasanii wenzake wa nje kuja nchini. MSANII mkongwe wa Hip Hop kutoka Marekani, Busta Rhymes amesema kuwa ameridhishwa na ukarimu wa Watanzania hali inayomfanya afikirie kuitangaza Tanzania kwa wasanii wenzake wa nje kuja nchini.
Busta Rhymes alikuwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mwaliko wa kuwa moja ya wasanii wa kutumbuiza katika tamasha la Fiesta la mwaka huu lililofanyika jumamosi katika viwanja vya Chuo cha Posta.
Mara baada ya kupanda jukwaani na kutakiwa azungumze kidogo, Mwanahip hop huyo maarufu duniani alisema "Sikutegemea kuwa Watanzania wanapenda muziki, ni wakarimu, na hii inanifanya niwakumbuke zaidi na zaidi nikirejea Marekani".
Alisema, atafanya kila analoliweza kuitangaza Tanzania kimuziki, na hata kuwavutia wanamuziki wenzake wakubwa, wakiwemo 50 Cent na Jay Z kuja kwa ajili ya onyesho, ikiwezekana katika onyesho lijalo la Fiesta.
Licha ya msanii huyo kuchelewa kupanda jukwaani, aliweza kutumbuiza zaidi ya saa moja huku akiwa na wasaidizi wake na kuufanya umati uliofika hapo kumshangilia kwa nguvu.
Busta alishangiliwa zaidi pale alipoimba vibao vyake ambavyo vimezoeleka katika masikio ya wapenda muziki kama `Make it Clap` na `Arab money'.
Mbali na nyota huyo kutoka Marekani, onyesho hilo pia lilipambwa na wasanii mbalimbali wa hapa nchini.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3606326&&Cat=8