Watanzania ni wanafiki hasa kuhusu Sakata la BSS

Ujinga wa madam ritha uko hapa;-kutoa zawadi kubwa ya 50 mil wakati hata angesema zawadi mil.5 bado watu wangeshiriki tu,pia ilikuwa ni kama matusi kuna kipindi mshindi wa ligi kuu bara alkuwa anapewa mil.30 afu bss mil.50
 



Hii ingekuwa essay unachukua 1\15
hawana uwezo wa kuwalipa siwanabidi
Wanabidi waandae Mashindano ya Lakimoja au elfu 50 sio lazima kutumia majina ya watu kutapeli
 
Soma vizuri mada yangu utaelewa main point yangu ni ipi
Mkuu, kwenye thread yako hata haueleweki unacholalamikia ni kipi, unasema eti walikuwa wanakaa kwenye hotel ya nyota tano kwa hiyo nini? Hiyo ni sehemu ya mchakato. Ni sawa mtu aje aseme kuwa 'wewe unasema elimu haijakusaidia wakati umeenda kusoma UDOM, chuo chenye majengo bora', je huo ubora wa majengo una manufaa gani ya moja kwa moja katika matumizi ya elimu yangu?. Hiyo ilikuwa ni sehemu ya mchakato na ilikuwa ni lazima wafanue hivyo. Na hao hawakuwa wanakaa hapo bure kwa sababu kuna kitu walnatoa in exchage ambacho ni vipaji vyao, wewe mbona hukwrnda huko kwenye hizo hotel? Ni kwa sababu huna kitu cha kutoa ili ukae kwenye hizo hotel. Kinachoangaliwa ni kuwa lile ni shindano na lengo la shindano linaeleweka., apatikane mshindi na mambo yaende kadiri ya makubaliano.
BSS sio kubwa kiasi cha mtu ukipita pale utapata jina mafanikio kirahisi. Kupata jina na kutangazwa kuwa umeshinda 50m ilhali umepewa sofa ni mzigo mkubwa kwa washiriki na kufanya wasemwe vibaya kuwa wametumia pesa kwa anasa kumbe waliambulia kumbatio tu.
BSS waache janjajanja, walipe pesa.
 
Nyinyi mmejikita kwenye kuwashambulia tu bila hata kuappeciate pia mambo mazuri waliofanya
 


Sasa hapa mnafiki ni nani kama siyo wewe? Mbona ni kitambo sana watu wengi walikuwa wanailalamikia BSS kutokuwa fair, wengi hawakutaka kuifuatilia BSS kwa sababu si wao washiriki, ni kweli BSS ilikuwa a timing bomb. Huwezi kuiba siku zote na kuwafanya watu wajinga, LAZIMA ipo siku utaumbuka tu kama hivi sasa Mme. Ritta alivyoumbuka. Huyu inabidi akamatwe na kunyongwa ama kifungo si chini ya miaka 99 maana ni tapeli na muhujumu uchumi.
 
Nyinyi mmejikita kwenye kuwashambulia tu bila hata kuappeciate pia mambo mazuri waliofanya


BSS imefanya nini cha maana zaidi ya utapeli, au utapeli ndiyo kitu cha maana kwako na wao? Hawa BSS ni sawa tu na kale kajamaa Jamal Malinzi, ni wezi tu na LAZIMA wakamatwe na kunyongwa.
 
Kwa nini mambo ya Kifamilia ya Madam Ritta yanataka kutumika kuichafua BSS?
 
Hebu kijite kwenye ukweli wa mambo.Tuambie unachokijua kuhusu malipo kwa washindi.Mjadala kuhusu BSS umejikita kwenye malipo kwa washindi. Wewe unatuambia kuwa eti wawe na shukurani.Kama ni hivyo,BSS wasingekuwa wanatoa ahadi ya kitita cha fedha hewa kwa washindi.Wangekuwa wakweli na si vinginevyo.

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
Hakika mkuu [emoji120][emoji120][emoji120]

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
Tatizo watz hata maisha yako yakikushinda unatafuta wakumpa lawama lkn bss ilikuwa bonge la fursa kwa vijana.
 
Hoja ya msingi ni ushindi kwa mil 50, na si vinginevyo! Mleta mada aliekwambia kila alieenda bss alihitaji exposure ama kuwa msanii ni nani? Wengine walivutiwa na hicho kitita ili wapate mitaji wakafanye mambo mengine. Usitumie uelewa wako mdogo kukejeli watanzania.
 
Tatizo watz hata maisha yako yakikushinda unatafuta wakumpa lawama lkn bss ilikuwa bonge la fursa kwa vijana.
we unaweza kukubali kufanyiwa unyama kama mchakato wa kumpata mshindi unaenda hadi miezi mitano vijana wanajituma kufanikisha ndoto zao wamepoteza muda wao mwingi halafu kumbe shindano lenyewe ni ukanjanja tu bro inaumiza sana bro fikiria kama kijana angeamua kulima vitunguu huko kwao angekuwa wapi
 
Kwani lengo la BSS ni kuwafundish life style ya mjini au lengo lilikuwa ni lipi??
Wao kuwatoa watu bush siii kwa sababu wanaupendo sana, nope bt wali hitajiana. Waliwahitaji ili kipindi kiendelee watengeneze pesa na wao waweza toka kimuziki.

Hakuna huruma mjini, au kusaidiana bure, BSS ilimtaka kayumba, Khamis na hao wengine ili Bss iendelee ku make pesa na fame, lakini wamepiga zaidi na hawakuwa fair
 
Siku zote walikuwa wapi chanzo cha hili tatizo ni wao wenyewe waliahidiwa nini wakakaa kimya maana sisi watazamaji tunajua wamelipwa.
 
Ujinga wa madam ritha uko hapa;-kutoa zawadi kubwa ya 50 mil wakati hata angesema zawadi mil.5 bado watu wangeshiriki tu,pia ilikuwa ni kama matusi kuna kipindi mshindi wa ligi kuu bara alkuwa anapewa mil.30 afu bss mil.50
Mkuu huo sio ujinga ni kwamba anataka mazingira ya kuchukua ela kubwa toka kwa wadhamini huku akijua atawapa kiduchu washindi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…