Watanzania ni wanafiki hasa kuhusu Sakata la BSS

Watanzania ni wanafiki hasa kuhusu Sakata la BSS

Watanzania wengi wanatatizo lakuwa wanafiki na wasio na shukrani hata kidogo, nimeona wengi wakiiponda BSS na wengine kwenda mbali zaidi kuitukana na kutoa lugha chafu juu yao Cha ajabu mpaka washiriki wenyewe walioshiriki bss nao wameingia kwenye Huu mkumbo.

Pamoja na BSS kutuumiwa kula hela ya washiriki lakini pia tusisahau bss wanamchango mkubwa Sana kwa Hawa washiriki wasio na shukrani hata kidogo hiv leo hii bila bss Nani angemfahamu kayumba au hamisi,Nimeangalia interview ya hamisi imenisikitisha Sana ametumia lugha chafu kuisema BSS.

Washiriki wengi walikuwa wanafanyiwa audition wakiwa hata kupaka make up walikuwa hawajui na wengine walikuja ikiwemo hamisi na mavazi ya ajabu ajabu wakafundishwa kuvaa wakawa wanatrainiwa vocal pamoja na kuimba na bendi ili watu hawaoni na washiriki wenyewe hawaoni zaidi ya kutoa lugha chafu.

walikuwa pia wanakaa kwenye hotel za nyota 5 Kama kambi na Zina gharama kubwa Sana kweli tunashindwa hata kuliona hili kweli?

Hao washiriki wanaoisema vibaya BSS mbona hatuoni juhudi zao katika mziki? Kazi yao Ni kutupia zigo lote kwa BSS bila hata wao wenyewe kujiangalia.kuna wasanii wengi hawajapata hata bahati ya kupata platform kubwa ya kuonekana ya BSS lakini wametoboa kwenye mziki wao wameshindwa vipi kutoboa?

NB: Ni kweli BSS wanakula hela lakini hiyo haimaanishi tusione uzuri wao waliofanya kwenye hii tansia ya mziki.
Mngewalipa hela zao zote heshima yenu msinge itia dosari... Wa Tz waliwaamini sana hamjui tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ivi mtoa mada unalenga kitu gani..naomba nijibu kwa kutumia sentesi moja tu
 
Jamani Vyuma vimebana sana..na ukiona mtu anatangaza fursa fursa jua wewe ndo fursa yenyewe( wahenga walishasema)!! huo uhuni upo kwenye sekta nyingi sana watu wanavutia upande wao..
Ila walichomfanyia kijana wa watu sio poa hata kidogo
 
Hivi watu walikuwa wanashiriki BSS ili wakalale kwenye mahotel ya gharama, au lengo, lilikuwa washinde, wapate zawadi zao, stahiki zao kama vile waandaaji walivyojitangaza?? Maisha yao yasonge..
Zawadi siyo fadhila??

Waandaaji wawape washindi washiriki stahiki zao, waache ubabaishaji!! Hilo ndilo linalogomba hapa..

Hayo ya kulala kwenye mahotel 5STAR, ni mipango ya waandaaji, hayawahusu washiriki...

Everyday is Saturday.......................😎
 
ivi mtoa mada unalenga kitu gani..naomba nijibu kwa kutumia sentesi moja tu
Mtoa mada lengo lake ni kutunanga watanzania tuliotokea Nanjilinjili, kuwa hatuna shukurani, BSS ndiyo imetuleta mujini, tumejua kulala 5 star hotel, so hatuna haki ya kulalamika hatujapokea zawadi kama ilivyotangazwa...
Turudi kijijini tukakate mkaa..
😀😀😀😀😀😀

Nonsense!

Everyday is Saturday.....................😎
 
Tanzania kuna vipaji vingi havipewi nafasi mfano amin,ben paul, barnaba hawa ni wanamuziki wazuri sana lakini tazama hatua waliyopo ni ya kawaida sana,hawa walitakiwa wapewe support kubwa
Nafasi ipi wapewe unayozungumzia ww?
 
Write your reply...hayo uliotaja ndo mazuri uki compare na dhuluma wanazofanya ?

daah aibu nimeskia Mimi sio kwa hoja za kitoto kama hizi kama tamasha na shindano wanaandaa wao ulitegemea hivyo vitu ulivyotaja sio malazi sjui five star afanye nani ?
 
Nyinyi mmejikita kwenye kuwashambulia tu bila hata kuappeciate pia mambo mazuri waliofanya

Kwako wew mambo Mazuri n Kufundisha watu kupaka make up??

kuweka watu kwny hotel ya nyota5??

Kukatisha vijana tamaa kuwa hawawezi na bdae vjana kutusua ( Kondeboy )

Kuzurumu washindi pesa zao halali ??

Ama hayo mambo mazuri ni yepi mkuu??
 
Kwahiyo ' Upuuzi ' wako wote huu uliouandika hapa ndiyo ' unahalalisha ' huo ' Uhuni ' wa Bongo Star Search ya Madam Rita na Washirika wake kwa huyo Kijana wa Watu ambaye anazunguka kila Mwezi kutokea Mkoani kuja Jijini Dar es Salaam tena hadi Wazazi wake wakiwa Wanakopa Pesa kwa Watu ili Kupigania Haki ya Mtoto ( Kijana ) Wao?

Kuna Watu uwezo wenu wa Kujenga Hoja unakera hadi Kutusikitisha. Siku zingine kama mnajijua ni ' Watupu ' Vichwani mwenu msiwe mnatupotezea muda kwa Kuja na ' Hoja ' za hovyo hovyo kama hizi. Hiyo Kampuni imefanya si tu ' Uhuni ' bali ni ' Ukatili ' kabisa kwa Mshindi huyo Kijana wa Watu. Hebu Wewe vaa Viatu vyake ungejisikiaje?

Tena nitashukuru kama Wizara husika itaipa Adhabu Kali hiyo Kampuni na ikiwezekana hata Kuifungia kama si Kuifuta kabisa ili iwe Fundisho kwa ' Wahuni ' wengine nchini.

Haha.. Nikionaga michango yako Mkuu huwa nacheka kwanza. Nasogeza glass ya Maji. Kisha nasoma kwa utulivu.. Barikiwa sana aise
 
Tatizo huyo jamaa anajiona ana akili sana. Lakini ni kilaza balaa. Magazeti yake huwa sisome kwa kuwa ni pumba tu na kujiboast boast sana.
Jamaa ndo alivyo ujuaji mwingi.
 
Kwako wew mambo Mazuri n Kufundisha watu kupaka make up??

kuweka watu kwny hotel ya nyota5??

Kukatisha vijana tamaa kuwa hawawezi na bdae vjana kutusua ( Kondeboy )

Kuzurumu washindi pesa zao halali ??

Ama hayo mambo mazuri ni yepi mkuu??
Mbona suala la kuwapa platform pana wasanii ya kuonekana na watanzania wengi ulisemi?
 
Mbona suala la kuwapa platform pana wasanii ya kuonekana na watanzania wengi ulisemi?

Platfom bila ela wapi na wapi..

Hizo nyimbo utarekord vipi..

Videos nazo jeh..?

Utaendelea kuishi kwenu..

Utakula platforms?

'Sanaa sio kiwanda cha kutengeneza maskini wenye majina makubwa '

Acha kuwaza utoto bwana mdogo..
 
Madam Rita alisema wadhamini wamekwama China sababu ya Covid19....ghafla wadhamini wakajitokeza na kusema walishamalizana naye.....duh ngoja tusubiri BSS ya mwakani
 
Back
Top Bottom