Watanzania ni wasahaulifu au wana mioyoni ya kipekee?

Watanzania ni wasahaulifu au wana mioyoni ya kipekee?

Ni kama tulirogwa! Ndiyo maana tuna amani, ambayo hata tukionewa tunakubali na tunatulia ili maisha yaendeleee!
 
Freeman Mbowe alipokamatwa kwa tuhuma za ugaidi, kuliibuka makundi mawili ya watu wenye mitazamo tofauti.

Kundi la kwanza ni la waliokuwa wakiiunga Serikali mkono katika jitihada zake za kumshughulikia "gaidi"

Na kundi la pili ni la waliokuwa wakikichukulia hilo kuwa ni kisingizio cha kukwamisha harakati,a kudai Katiba Mpya. Kwa jinsi watu walivyokuwa na "hasira", kama insingelukuwa kazi "nzuri" ya Jeshi la Polisi kuthibiti maandamano, watu wangefurika mabarabarani na mabango yaliyoandikwa "MBOWE SI GAIDI". Lakini kwa sababu ya uwekedi wa Jeshi la Polisi, hilo halikutokea.

Kesi ikienda mahakamani, lakini kabla ya kuhitimishwa, Serikali ikaichomoa.

Hilo nalo wananchi hawakuihoji Serikali kwamba:

1. Imeamua kumwachia Mbowe baada ya kujiridhisha kuwa si gaidi?

2. Imeimarisha ulinzi kwa namna ambavyo gaidi hawezi kuwa na madhara nchini?

3. Ni sababu gani iliyoifanya kumfutia mashaka mtu mwenye tuhuma nzito kiasi hicho?

4. Ilimwachia Mbowe kwa utashi wake au ilihofia kuwa Wazungu watainyima hela kwa kisingizio kuwa inaihujumu Demokrasia?

5. Ikiwa Mbowe ni gaidi, kwa nini anaachwa achangamane na raia wa kawaida, wakiwemo waliomo kwenye ibada?

6. Au nchi imeingia makubaliano maalum na "gaidi", hasa ikizingatiwa kuwa alipotoka tu gerezani, kituo chake cha kwanza kilikuwa ikulu?

7. Serikali inamchukuliaje Mbowe kwa sasa? Ni gaidi si gaidi?

Hayo yote Watanzania wameshindwa kuihoji Serikali? Au hawajui kuwa ni Kodi zao ndizo zinazotumika kuiendeshea Serikali, ikiwa ni pamoja na kuzihudumia mahakama na ofisi ya Mwendesha mashtaka wa Serikali?

Kama wao wanaiogopa Serikali yao, si wangewatumia wabunge wao kuiweka Serikali kitimoto hadi iseme ukweli wote?
 
Miaka ya nyuma, waliibuka Wabunge wa Watanfanyika wenye uchungu na Tanganyika yao, na kulivalia njuga suala hilo. Walijulikana kama G55, nafikiri, kwa sababu walikuwa 55. Walitaka Tanganyika irejeshewe uhai wake.

Na kama inavyojulikana kuwa watawala wa Tanzania Wana akili sana, walizitumia ipasavyo hadi hilo suala likapoa na kusahaulika kwa muda.

Mbwa anayebweka sana mtupie fupa la nyama lenye tuminofu tugumu. Mbona atakuacha upite kama mwenyeji vile?

Nafikiri, watawala nao walizitumia hiyo mbinu pia kuwanyamazisha G55. Baadhi walipopewa vyeo kama uwaziri walitilulia. Si unajua mtu hapigi kelele anapokula nyama?

Miaka ya hivi karibuni, hilo kumeendelea kuibuka lakini halijapata msisitizo wa kutosha.

Madhalani, baadhi ya wapigania Tanganyika nao wameonekana kufyata mkia kama ilivyokuwa kwa G55.

• Dr. Harrison Mwakyembe alipokuwa akifundisha UDSM, msimamo wake ulikuwa ni Serikali tatu. Lakini alipopewa Uwaziri, wimbo ulibadilika

• Humphrey Pole Pole alifahamika kama mmoja wa wanaharakati waliokuwa wakiidai Tanganyika. Lakini alipoingia rasmi kwenye Siasa, kawa "neutral".

Je! Watanganyika wamesahau kuwa walikuwa wakiidai Tanganyika yao, na kwamba hawatapewa pasipo kuidai?
 
Kwa matukio yaliyowahi kuibuka na kusababisha hasira kwa wengi, lakini baada ya muda hali ikawa kimya, inaweza ikawa ni ishara kuwa Watanzania ni watu wa kipekee sana. Ama ni wasahaulifu au wana mioyo ya kipekee ya kusamehe au kupuuzia mambo.

Nitatoa mifano michache.

Serikali ilipoamua kuwahamisha Wamasai wa Ngoro Ngoro toka kwenye ardhi yao ya asili, watu wengi walipaza sauti wakiitaka Serikali ibadilishe huo mpango.

Kulikoni mbona hilo halizungumziwi tena? Wamasai wameshapatiwa haki yao?
Nadhani ulihamishwa pia ivo unatukumbusha tuendelee kupiga kelele? Umeme Mkuu,hatujui hata tuanzie wapi kupiga yowe
 
Ujinga umezidi kwa watu.
 
Baada ya Tundu Lissu kupigwa risasi, kelele zilipigwa sana lakini zote zikaonekana kama za chura kujaribu kumzuia tembo kunywa maji

Kuna watu waliohisi kuwa ni Serikali ndiyo iliyoifanya huo uhalifu, na kuna waliokuwa na mtazamo tofauti.

Ni zaidi ya miaka sita sasa tokea tukio hilo la kutisha litokee, na inaonekana kama vile limeshasahaulika.

Watanzania wameshindwa kuhoji hadi wapate majibu ya kuridhisha?

1. Jeshi la Polisi lilishindwa kuanza upelelezi kwa sababu Lissu alikuwa nje ya nchi. Hatua imefikia wapi kwa sasa hasa ikizingatiwa kuwa Lissu yupo nchini?

2. CHADEMA walitaka wapelelezi toka Uingereza wapewe jukumu la kumsaka mhalifu aliyetaka kumuondoa Lissu duniani kabla ya wakati wake lakini Serikali ya kipindi kile ikaweka mgomo. Kwa nini wasiishinikize Serikali ya sasa kuunda tume ya kulichunguza hilo? Au hata kuomba wapelelezi wa Uingereza kuja kilisaidia hilo?

3. Kuna baadhi ya wanasiasa walioituhumu CHADEMA na viongozi wake, hasa Mbowe, kuwa ndiyo walihusika kumshambulia Lissu. Je! Jeshi la Polisi liliigopa kumkamata Mbowe ili alisaidie Polisi katika hilo? Au halikusikia tuhuma zilizokuwa zikotolewa na wanasiasa, hasa wabunge wa CCM, kuwa Mbowe anahusika?

4. Watanzania wameshaludahau hilo au wameamua kulipuuzia?
 
Kipindi fulani, mgombea Urais kupitia CCM aliahidi million hamsini kwa kila kijiji. Japo alifanikiwa kuukwaa Urais, lakini sikumbuki ni vijiji vingapi vilitimiziwa hiyo ahadi.

Watanzania wangapi wanaikumbuka hiyo ahadi? Ni wangapi waliifuatilia?

Au waliridhishwa na zawadi ya fulana n kofia zenye rangi za kuvutia?
 
Baada ya gesi kuanza kuvunwa Mtwara, Serikali iliwatia wananchi moyo kuwa hayo mafanikio yangewaletea unafuu kwenye gharama ya nishati ya umeme na gesi ya kupika. Wengi walitarajia kuwa suala la kutumia kuni kupikia lingebaki Historia. Zingeendeleaje kutumika wakati gesi ingekuwa bei rahisi kuzidi kuni na mkaa?

Mimi nipo kijijini. Hali ikoje huko mijini? Watu wameshaachana na mkaa?
 
Alipita popobawa na tukasahau. Kila jioni, eatv lazma mtu aseme kaingiliwa ila tumesahau.
Hayo mengine ni kuomba tu reformtukikwama huwa tunatulia
 
Labda wewe
Hata ukijaribu ku Exclude watanzania wote na mpumbavu nikabaki mwenyewe.

Sidhani kama kuna chochote cha maana kinafanyika kwa ufasaha zaidi na watanzania.

Hivyo uhalisia uko palepale watanzania wana shida.
 
Nadhani ulihamishwa pia ivo unatukumbusha tuendelee kupiga kelele? Umeme Mkuu,hatujui hata tuanzie wapi kupiga yowe
Ila wanasiasa wajanja sana! Mkizidisha kelele mnatengenezewa tukio la kuwahamisha kwenye mstari, na baada ya muda kelele zinapungua kwa kuhamishiwa kwingineko.
 
Kwa matukio yaliyowahi kuibuka na kusababisha hasira kwa wengi, lakini baada ya muda hali ikawa kimya, inaweza ikawa ni ishara kuwa Watanzania ni watu wa kipekee sana. Ama ni wasahaulifu au wana mioyo ya kipekee ya kusamehe au kupuuzia mambo.

Nitatoa mifano michache.

Serikali ilipoamua kuwahamisha Wamasai wa Ngorongoro toka kwenye ardhi yao ya asili, watu wengi walipaza sauti wakiitaka Serikali ibadilishe huo mpango.

Kulikoni mbona hilo halizungumziwi tena? Wamasai wameshapatiwa haki yao?
Hivyo ndivyo tulivyo.Yalianza zamani za miaka ya 70's,watu walichomewa miji yao ili wahamie vijiji vya ujamaa.Baada ya miaka michache, watu wengine wakapewa tena yale maeneo na maisha yanaendelea bila kuhoji.
Kuna kipindi viongozi waliwapitisha watu kwenye maisha ya ajabu sana kuogea sabuni ilikuwa ni anasa kubwa.Lakini maisha yaliendelea tu.Alietuloga alikufa kitambo sana
 
Ila wanasiasa wajanja sana! Mkizidisha kelele mnatengenezewa tukio la kuwahamisha kwenye mstari, na baada ya muda kelele zinapungua kwa kuhamishiwa kwingineko.
Yaan acha tu,sahivi watu wamesahau siasa wanamzungumzia ziara za makonda🦶🏿
 
Hivyo ndivyo tulivyo.Yalianza zamani za miaka ya 70's,watu walichomewa miji yao ili wahamie vijiji vya ujamaa.Baada ya miaka michache, watu wengine wakapewa tena yale maeneo na maisha yanaendelea bila kuhoji.
Kuna kipindi viongozi waliwapitisha watu kwenye maisha ya ajabu sana kuogea sabuni ilikuwa ni anasa kubwa.Lakini maisha yaliendelea tu.Alietuloga alikufa kitambo sana
Aisee!
 
Back
Top Bottom