Freeman Mbowe alipokamatwa kwa tuhuma za ugaidi, kuliibuka makundi mawili ya watu wenye mitazamo tofauti.
Kundi la kwanza ni la waliokuwa wakiiunga Serikali mkono katika jitihada zake za kumshughulikia "gaidi"
Na kundi la pili ni la waliokuwa wakikichukulia hilo kuwa ni kisingizio cha kukwamisha harakati,a kudai Katiba Mpya. Kwa jinsi watu walivyokuwa na "hasira", kama insingelukuwa kazi "nzuri" ya Jeshi la Polisi kuthibiti maandamano, watu wangefurika mabarabarani na mabango yaliyoandikwa "MBOWE SI GAIDI". Lakini kwa sababu ya uwekedi wa Jeshi la Polisi, hilo halikutokea.
Kesi ikienda mahakamani, lakini kabla ya kuhitimishwa, Serikali ikaichomoa.
Hilo nalo wananchi hawakuihoji Serikali kwamba:
1. Imeamua kumwachia Mbowe baada ya kujiridhisha kuwa si gaidi?
2. Imeimarisha ulinzi kwa namna ambavyo gaidi hawezi kuwa na madhara nchini?
3. Ni sababu gani iliyoifanya kumfutia mashaka mtu mwenye tuhuma nzito kiasi hicho?
4. Ilimwachia Mbowe kwa utashi wake au ilihofia kuwa Wazungu watainyima hela kwa kisingizio kuwa inaihujumu Demokrasia?
5. Ikiwa Mbowe ni gaidi, kwa nini anaachwa achangamane na raia wa kawaida, wakiwemo waliomo kwenye ibada?
6. Au nchi imeingia makubaliano maalum na "gaidi", hasa ikizingatiwa kuwa alipotoka tu gerezani, kituo chake cha kwanza kilikuwa ikulu?
7. Serikali inamchukuliaje Mbowe kwa sasa? Ni gaidi si gaidi?
Hayo yote Watanzania wameshindwa kuihoji Serikali? Au hawajui kuwa ni Kodi zao ndizo zinazotumika kuiendeshea Serikali, ikiwa ni pamoja na kuzihudumia mahakama na ofisi ya Mwendesha mashtaka wa Serikali?
Kama wao wanaiogopa Serikali yao, si wangewatumia wabunge wao kuiweka Serikali kitimoto hadi iseme ukweli wote?