Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?

Tuonyeshe kwanza wewe ni wapi umepaza sauti kuidai katiba/na tume Hulu ya uchaguzi? Au wewe SI miongoni mwetu PASCHAL MAYALLA
 
Wakati wa Mwendazake kelele zilipigwa za kudai Katiba mpya, maandiko yakachapishwa kuwa si kipaumbele cha sasa, leo kelele zinapigwa za Bandari unatwambia bandari ni swala dogo na Katiba ndilo jambo la muhimu; kwa nini umuhimu huu wa Katiba haukuonekana kipindi cha Mwendazake ndo uje kuonekana sasa.?
 
nikataka nishange kuwadi wa soko huria uvute maokoto kwa msigwa uje upinge uuzaji wa bandari.
hili ndo tatizo la waandishi makasuku.
pasco wewe ni chichidodo.
 
P usiamini tu katika maneno ya matumaini ya ufanisi,ila tazama na hawa walio utia ubatili katika sheria zetu,je watashindwa kutia ubatili katika ndoto ya matumaini ya ufanisi unaofikirika kwa siku zijazo🤔
 
Kwa kuwa kipindi kile mambo yalikwenda harijojo kwa mtazamo wako basi ni sahihi pia yaende hivyo hivyo hivi sasa na wakati mwingine wowote ule ujao ??!!

Tujaribu kubadilika ili tuwe tunajifunza kutokana na makosa tunayoyafanya !!

Sio kwamba eti kwa sababu makosa yalifanywa hapo kabla basi ni sahihi tu tuendelee kuyafanya makosa mengine sasa na hata wakati ujao !! KATIBA ndio sheria mama ya Taifa lolote lile ! Kama ina mapungufu matatizo na mikanganyiko lazima itakuwepo !!
 
Sio kwamba eti kwa sababu makosa yalifanywa hapo kabla basi ni sahihi tu tuendelee kuyafanya makosa mengine sasa na hata wakati ujao !!

Umesema vyema hapa.! Hatutaki makosa ya bandari yaje kujirudia kama yalivyo ya Katiba, kwa sasa tupambane na bandari yetu hata kama ni swala dogo kwa mtazamo wenu.! Tukikaa kimya litakapita likija kuibuka huko mbele kauli kama hizi zitakuja kutoka tena.!
 

Itoshe kusema huyu Paskali ni mnafiki na CHAWA
 
Akili zako ni ndogo kujua mzunguko wa mambo ...ili jambo la bandari likipita hata katiba itakuwa vigumu kupatikana maana hao waarabu na mafisadi wanategemea kufanikiwa mamboyao ndani ya hii katiba vinginevyo watapata hasara...aina hii ya uwekezaji wa kifisadi inapo kithiri kwenye nchi basi hata viongozi wa hizo nchi upandikizwa na hao mafisadi ili kilinda ufisadi wao
 
Mentality ya watz wengi ni wizi tuh,mtu akipata nafas Hususan serikalin anachowaza na kuiba tuh,hasa hawa wanaojiita wasomi,mfano propesa tibaijuka had mgao anachukua kenge yule refer escrow,wanaopigia kelele mkataba wa DP World wengi ni wezi tuh
 
Magufuri aliligharim Taifa Kwa kuua demokrasia na kuleta lile bunge dhaifu na kuikanyaga katiba,woote walikuwa kimya,Kila siku uchaguz eti watu wanahama vyama kuunga mkono juhudi na kulitia Taifa hasara Kwa chaguz mpya Kila siku, hakuna aliethubutu kukemea,Leo wanajiona Wana uchungu na uzalendo wa Taifa
 
Badala ushukuru kuwa Watangayika wameanza kuwa smart upstairs then unawakejeli it doesn't make sense kujiona. Wewe una Akili na wengine hawana hiyo ni Ego inakusumbua
 
Paskali unahamisha mjadala kiujanja huku ukizuga uko pamoja nao.USD 50k sio haba
 

Wewe ni mtu wa hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…