Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Lazima kuna kitu hakiko sawa akilini mwa viongozi wetu na mashabiki wengi wa siasa wasio na uwezo mkubwa wa kufikiri kwa makini. Leo nasoma bajeti ya serikali, nakutana na maneno kwamba bajeti yetu pia itategemea msaada kutoka kwa washiriki wetu wa maendeleo (development partners).
Sasa mimi nimeona huku ni kuwa wanafiki sana. Ikiwa tunaziona hizi nchi na taasisi za kimataifa kuwa washiriki wetu wa maendeleo, kwamba wanatujali kiasi cha kutoa fedha zao ili kuchangia maendeleo yetu, kwa nini pale ambapo wanatukosoa na kutushauri tunawaita mabeberu? Kama huu sio ulevi na wendawazimu wa kisiasa ni nini basi?
Mtu ambaye anakusaidia katika mambo ya msingi ya maendeleo, ni wazi kuwa kwa kiasi fulani anakuwa na uhalali wa kukushauri au kukukosoa pale ambapo anaona unakosea. Kuna usemi kwamba usiume mkono unaokulisha (dont bite the hand that feeds you), kwa nini viongozi wetu wanakuwa wepesi sana wa kusahau hili wanapokuwa kwenye majukwaa ya kisiasa na kutaka kujiongezea umaarufu kwa kuropoka maneno "mabeberu"?
Hatusemi kwamba tunapaswa kuuza uhuru wetu kwa nchi tajiri au taasisi za kimataifa ambazo ni "washiriki wetu wa maendeleo". Bali twapaswa kuwa waungwana kiasi kwamba hata pale tunapokosolewa au kushauriwa na hatupendi, basi tujue jinsi ya kujibu kistaarabu. La sivyo sisi na viongozi wetu tunajionyesha kuwa wanafiki tu! Ningependa kuona hili linazingatiwa kwanza na Rais Magufuli na wengine watafuata.