Watanzania ni watu wa matukio, tumeshasahau kuwa vifurushi havijashushwa na walioshusha kuna uhuni pia

Watanzania ni watu wa matukio, tumeshasahau kuwa vifurushi havijashushwa na walioshusha kuna uhuni pia

haszu

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2017
Posts
978
Reaction score
2,313
Sasa upepo wote umehamia kwa Samia, tumesahau kabisa kua serikali imetoa agizo lakini hadi leo kuna mitandao haijatekeleza na hata.

Tunataka ile menu ya zamani, kwa nini hatuna ajenda yani tunafuata tu upepo? Tunakubari vipi?

Yaani ulikuwa unanunua GB 7 elfu 10 kwa mwezi, leo unapewa GB 2.5 kweli? Hata kama ni kodi au kupanda kwa gharama ndo maara mbili au zaidi ya 60% kwanini tusiipigie kelele hili?

Kama Serikali inaweza kutoa agizo halafu kisitekelezwe je tuko salama sisi? Hapa yaweza kuwa ni danganya toto au Serikali haina meno.

Watanzania tuwe na agenda na lengo, mada zetu zisibadilishwe na upe wa wanasiasa, wao wana wifi kwao hawajui machungu ya bando la elf tatu gb 1, huu ni unyonyaji, mnaniangusha wa ndugu zangu
 
Sasa upepo wote umehamia kwa Samia, tumesahau kabisa kua serikali imetoa agizo lakini hadi leo kuna mitandao haijatekeleza na hata
Tuna taka ile menu ya zaman, kwa nini hatuna ajenda yani tunafata tu upepo? Tunakubari vipi?
Yan ulikua unanunua GB 7 elfu 10 kwa mwezi, leo unapewa GB 2.5 kweli? Hata kama ni kodi au kupanda kwa gharama ndo maara mbili au zaidi ya 60% kwanini tusiipigie kelele hili?

Kama serikali inaweza kutoa agizo halafu kisitekelezwe je tuko salama sisi? Hapa yaweza kua ni danganya toto au serikali haina meno,
Watanzania tuwe na agenda na lengo, mada zetu zisibadilishwe na upe wa wanasiasa, wao wana wifi kwao hawajui machungu ya bando la elf tatu gb 1, huu ni unyonyaji, mnaniangusha wa ndugu zangu
Kuna huduma zingine zilikuwa ni offer! offer! Offer! ambazo wana uhuru tu wa kuzikatisha na wasiulizwe na yeyote.
 
Hawa wanasubiri Yowe lianze kama la Abass jana

Ngoja utajionea mwenyewe
 
Haya mambo huwa yananishangaza sana! Wakati watumishi wa umma tunapolia humu jukwaani kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja yetu, kuna baadhi ya watu wenye akili fupi, hutukejeli!

Watu hao hao wakipandishiwa gharama za vifurushi, wanapaza sauti zao kulia! Wameshindwa kuelewa ya kwamba hakuna maisha STATIC! Maisha ni Dynamic! Hivyo gharama za maisha hubadilika kutokana na sababu mbalimbali!

Vivyo hivyo kwa hayo Makampuni ya Simu! Na yenyewe yangependa kufanya biashara ya faida na siyo biashara ya kutoa huduma na kuwaridhisha wanyonge! Wananchi wangekuwa na uchumi mzuri mifukoni mwao, sidhani kama kungetokea mpaka wale waliokuwa tayari kuandamana eti kushinikiza vifurushi vishushwe kama zamani.

Udikteta umeshaondoka nchini mwetu! Ni wakati sasa kwa Rais Mpya kurudisha mzunguko wa fedha mtaani! Naamini hivi vilio vyote vitakwisha. Hata sasa, wachache wenye kipato kizuri, siamini kama na wao wanalalamikia hizi bei mpya za vifurushi kama wale wanyonge wa magufuli.
 
Vodacom bado wamekomaa na bando la zamani.
Wamelewe ukiritimba .toka aje mkurugenzi mzalendo ndio matokeo yake ,maana kwa lazima atakua kwenye mrengo mmoja wapo .hiki kiburi kwa serikali sio bure
 
Back
Top Bottom