Pre GE2025 Watanzania siasa haihitaji ushabiki, siasa inahitaji ufuasi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

hitler2006

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2014
Posts
489
Reaction score
454
Kuna shida sana ya watanzania tulio wengi,tumeathirika sana na ushabiki hasa wa namna ileile ya simba na yanga.

Siasa zinahitaji ufuasi,mfuasi ni mtu anayeelewa barabara kile anchokifuata kimaono, kimtazamo, kisera

Hizi siasa za kishabiki mtu anaunga mkono chama fulani kwa mihemko au kapewa ubwabwa zinaleta tabu sana.

Siasa za kishabiki zinafanywa na watu wajinga na hasa ndo mtaji wa wanasiasa wetu ambao hawawajibiki kwa uma wala kwa vyama vyao.

Matokeo yake wananchi wamegeuka kuwapigia magoti wanasiasa na viongozi wa kisiasa ambao kimsingi sisi wananchi ndo waajiri wao.

WANANCHI TUAMKE TUZIJUE SERA,ITIKADI NA MAONO YA VYAMA HIVI

Maana kuna vingine vinapiga ngoma ya ujamaa huku vikicheza miondoko ya kibepari
 
Mimi naumia sana ninapo ona magoli yanapewa thamani ya fedha na ilihali Bado Kuna wimbi la wanafunzi elimu ya juu hawana mkopo na kupelekea kutoendelea na masomo. Inauma sana tena sana.
 
Kuna shida sana ya watanzania tulio wengi,tumeathirika sana na ushabiki hasa wa namna ileile ya simba na yanga.

Siasa zinahitaji ufuasi,mfuasi ni mtu anayeelewa barabara kile anchokifuata kimaono, kimtazamo, kisera

Hizi siasa za kishabiki mtu anaunga mkono chama fulani kwa mihemko au kapewa ubwabwa zinaleta tabu sana.

Siasa za kishabiki zinafanywa na watu wajinga na hasa ndo mtaji wa wanasiasa wetu ambao hawawajibiki kwa uma wala kwa vyama vyao.

Matokeo yake wananchi wamegeuka kuwapigia magoti wanasiasa na viongozi wa kisiasa ambao kimsingi sisi wananchi ndo waajiri wao.

WANANCHI TUAMKE TUZIJUE SERA,ITIKADI NA MAONO YA VYAMA HIVI

Maana kuna vingine vinapiga ngoma ya ujamaa huku vikicheza miondoko ya kibepari
Lengo la siasa siyo vita wala kusifiana bali ni kupambana na changamoto tunazokumbana nazo wakati huo na kuzimaliza ili kuboresha maisha yetu.
 
Back
Top Bottom