Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,117
- 16,506
Nimesoma andiko la PASCO wa JF kuhusu kile anachodai ni UJINGA wa watanzania, kwa kuendelea kuichagua CCM ambayo kwa mawazo ya PASCO ni chama kibaya.
1. Naomba kumthibitishia kuwa MIMI na watanzania sio wajinga, tunatambua jema na ovu, tunatambua nani ni mbaya na nani ni mwema..yawezekana yeye ameshindwa kutambua, hivyo siwezi kuzungumzia ujinga wake ila nitazungumzia juu yangu na Watanzania wenzangu ambao kwa Miaka zaidi ya 50 sasa tumeendelea kuiamini CCM.
Na kama ni kile ninachokiona ni MAHABA kwa Upinzani wa nchi hii, niseme tena mimi nimewahi kuwa Mpinzani wa CCM kwa muda mrefu, its no better kwenye upinzani kuliko hata kwa CCM..Hauwezi kulizungumza suala la UONGOZI BORA kwa upinzani..hauwezi kuzungumzia Suala la kukuza ELIMU kwa wapinzani, hauwezi kuliongelea suala la kukomesha Rushwa kwa Wapinzani wa nchi hii...hauwezi kuwaamini kwa lolote wapinzani wa nchi hii..Ni watu wasiojitambua, wasiojielewa, wasio na misimamo, wanaoyumba na baya zaidi WASIOFIKIRI.
Ndio tarehe 25th October 2015, tutaichagua tena CCM, tena kwa kishindo KIKUU, lakini kamwe hatuchagui kwa UJINGA..,tunazo akili, tunajua BAYA na ZURI kwetu, na hivyo..TUMEKUSIKIA, TUMETAFAKARI na TUMESHAAMUA kuwa MAGUFULI ndio Rais wetu wa AWAMU ya TANO..
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CCM.
Njaa ikipanda kichwani ni maafa makubwa kuliko Malaria ikipanda kichwani. Mbona unaimba ngonjera ya maafali kwenye maadhimisho ya mashujaa?
Kwa miaka 50 umeiamini CCM na kwa muda mrefu umekuwa mpinzani. Safi, sasa swali dume ni: YALE ULIYOKUWA UKIYAONA WRONG ULIPOKUWA MPINZANI YAMEREKEBISHWA?
Kizuri cha kutuambia hapa ni kuwa UMEUKWAA ULAJI, tiba kwa njaa ya mifuko yako. Kuniambia wapinzani wa nchi hii hawafikiri, hawajitambui, ........... ni dalili ya kutotumia kichwa ipasavyo. Ikiwa huwezi kufikiri tungekuwaje without opposition basi hata hujui siasa, unajua UNAFIKI.
Nakuhakikishia, kitu pekee kwa sasa unachoweza kukihubiri ni MAGUFULI lakini sio CCM. Credibility ya CCM kama chama imedrop badly, and you know that.
Nitakueleza mfano mdooogo sana wa kwa nini mimi binafsi naamini CCM imefubaa beyond repair. Mkiwa na serikali inayoshindwa kudhibiti uchakachuaji wa Diesel kwa kuwaadhibu wachakachuaji (ambao ni wafanyabiashara wachache) badala yake inapandisha kodi kwenye Kerosene, hamna kitu hapo.
Unaweza ukaliona dogo, lkn ni kukosa collective bargaining kwa serikali ndio maana hakuna aliyefikiri kuwa maamuzi hayo yataathiri MAZINGIRA kwa kiasi gani kutokana na ku-temper na nishati inayotegemewa na wananchi, achilia mbali kuwaumiza wananchi wenyewe.
Mungu atuepushie balaa lako. Tuna utulivu, mioyoni hatuna amani. Hata tembo hawana amani