matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Kwa sababu hofu ya Mungu imekuwa kubwa kwa watu wengi siku hizi wameanza kumtumia Mungu kisiasa.
Kunq mqma mmoja namkumbuka aliwahi kuomba hadi analia Mungu afanye miujiza ya kumpa pesa wakati pesa alikuwa nayo ya kutosha. Lengo ilikuwa ni kuwaaminisha watu wa hapo nyumbani (wageni) wajue anahali mbaya wasimuombe kitu. Hii ni kutumia maombi kisiasa.
Leo mwanasiasa kwa sababu amejua watu wengi wanamuogopa Mungu, atatumia kauli za kimungu ili kuhalalisha uongo wake. Atatumia Mungu, Biblia ili kuhalalisha kukweoa wajibu aliotakiwa kuufanya.
Leo watu wavivu nao wanamtumia Mungu kisiasa kwa kusema eti Mungu amewapangia wawe masikini. Wanaona ni halali wao kupewa msaada na watu ambao ni kama wao sema wao waliamka na kuchakarika.
Wanamaombi wa kitanzania wanakesha maporini wakiomba miujiza ya kiuchumi na kiafya badala ya kufanya kazi siku sita na sabato Jumamosi kuitumia siku nzima na Mungu ili wabarikiwe. Hii ni siasa ya kukwepa wajibu na uwajibikaji.
Wakuu tuache kumtumia Mungu kisiasa.
Ni hayo tu
Mbarikiwe
Mtumishi Matunduizi