Nipende kutoa rai kwa watanzania kuacha kushabikia kitendo kilichofanywa na Daktari kupigana na askari tena akiwa katika majukumu yake. Mambo kama haya yakishabikiwa kila mtu kuchukua sheria mkononi Tutahatarisha usalama wetu wenyewe
Hili ni jambo baya na Nashauri Dr. Aliefanya jambo hili inawezekana kwa kushindwa ku control hasira atumie nafasi ya dhamana aliyopewa kuwa huru kumwomba askari aliemshambulia na ikiwezekana kama ataridhia wayamalize kifamilia. Ni pamoja na kuliomba Jeshi la polisi msamaha.
Kama wakiridhia msamaha, aombe radhi na kujutia kitendo alichokifanya kupitia vyombo vya habari ili mfano huu mbaya usije ukaigwa na jamii inayomwona kama shujaa. Asipo pambana kufikia suluhu ya kifamilia anapoteza kila kitu kwani kwa kesi kama hii si rahisi kushinda
Swal la raia kuvamia polisi tukilishabikia tutakuwa kama Haiti. Tusitengeneze askari ambao wanakosa kujiamini kwenye kusimamia sheria mwisho wa siku tutakao umia ni sisi wenyewe.
Fikiria ikitokea Polisi waseme tupo likizo mwezi mmoja kilamtu apambane na hali yake. Je tutakuwa salama? Hivyo tusiwabeze kwani hata alie na degree kumi akipewa Bunduki akaambiwa aende lindo kupambana na maharamia hatoweza.
Kila mtu aheshimu fani ya mwingine kwani tunategemeana. Wote tungekuwa madaktari nani angefanya kazi ya ulinzi?
Inawezekana kulikuwa na Provocation lakini ni muhimu kujifunza kuwa mvumilivu na kutokufanya maamuzi ya jazba kwani madhara yake ni makubwa.