Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,809
- 6,948
Kuna hili tatizo nimeliona na kulitafakari kwa muda mrefu. Ni huu mtindo na tabia waliyo nayo Watanzania wengi, pale wanapouza vitu walivyotumia mfano gari, simu, nk. kuuza kwa bei ya juu sana.
Kitu ukishakitumia, thamani yake inashuka sana. Wataalamu wanasema hata gari brand new ukiinunua na kuitolea showroom, ikitoka tu pale ukaiendesha nusu kilomita, thamani yake inakuwa imeshuka sana. Hauwezi na haustahili kujaribu kuiuza kwa bei ile uliyonunulia.
Kuna changamoto kubwa ya maadili ya kibiashara katika jamii yetu. Watu hawajui nini ni fair price (bei halali) kulingana na kile anachouza. Tamaa imetutawala sana.
Gari umeitumia kwa miaka 5 tena kwenye hivi vinjia vyetu tunaita barabara, halafu unakuja kutaka kuuza kwa bei uliyonunulia wewe kweli?
Simu umeitumia kwa miaka 2, imepitia masaibu yoote, leo hii unataka uiuze kwa bei ambayo mtu anaweza kupata simu nyingine mpya?
Tukumbuke hata haya magari ya Kijapani tunaweza kuyaagiza na kuyaendesha kwa sababu wenyewe wana utamaduni wa kubadilisha magari baada ya muda fulani. Hivi hivi tusingeweza kuyalipia kama nao wangekuwa na tabia kama zetu?
Tubadilike bwana!