Watanzania tuamke, Bunge la chama kimoja limezaa tozo

Mzoee tu Mambo ya Tozo,Wafanyakazi Kila mwezi wanakamuliwa PAYE na wakilalamika mnawasema
 
subira? wakati tunaendelea kuumia
Naam, ili dawa ituingie vizuri. Watanzania tumezidi mno kuwa mazoba. Bila watanzania wote kupandwa hasira na kusema sasa basi, hakuna kitakachofanyika. Tunahitaji kuwa jasiri kama Wazambia
 
Hivi ni mpinzani gani mzalendo anayetaka kuona UKAMILIFU WA MIRADI YA KIMKAKATI NA UPANUZI WA HUDUMA ZA AFYA VIJIJINI akaiona TOZO YA MIAMALA YA SIMU kuwa ni MBAYA NA ADUI WA TAIFA?!!!
Kachemka kama yule zulumati....
 
Ahaa kumbe kale ka lugha laini 'solidarity fund' kalikuwa ka kuzugia tu, ukweli ni 'tii sheria bila shurti'
 
Tatizo si kulipa Bali ni matumizi.
 
Bunge Batili na Nyang'anyi liliowekwa na Mtu mmoja haliwezi kuwatetea wananchi.Bunge hili 2025 tupa kule. Likachunge Ng'ombe!!
 
Bunge Batili na Nyang'anyi liliowekwa na Mtu mmoja haliwezi kuwatetea wananchi.Bunge hili 2025 tupa kule. Likachunge Ng'ombe!!
Ili hilo lifanyike basi nguvu ya pamoja inahitajika bila kujali itikadi zetu za u ccm na upinzani.
 
Nchi hii wasaliti wakubwa wanaopaswa kuja kufikishwa mahakamani ni vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
Badala ya kuwa na wananchi wao wanatumika na wanasiasa kuiba chaguzi.Hopeless kabisa.
 
Yaani Serikali ya huyu mama wa viti maalum imeamua kutupora hela Watanzania, mfano kodi ya majengo ya mwaka wa fedha 2021/22 tulikwishalipa kabla ya July mosi 2021 lakini leo tunaambiwa tulipie kodi ya mwaka mwingine upya, huu si ni wizi na uporaji? Wanasheria hebu litazameni suala hili kwa jicho pana zaidi ili mfungue kesi Mahakamani kupinga unyanganyi huu wa Serikali. Wameshindwa kubuni vyanzo stahiki vya mapato wameamua kutupora kwa nguvu pesa zetu kupitia Huduma ambazo hatuwezi kuzikwepa
 
Wenye nyumba Crimea na johnthebaptist
 
La upinzani lilikuwa na kususia vikao ila cha ajabu walikuwa wepesi wakupokea marupurupu bila kufanyakazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…