Shooter Again

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
5,603
Reaction score
9,263
Kama kichwa cha habari kinavyosema.

Mimi binafsi nipo tayari kumwaga damu yangu Kwa ajili ya hili taifa, najua ipo siku nitakufa kwanini niogope kifo wakati huyo atakayenishoot na yeye ipo siku atakufa pia?

Tunaona serikali inatuibia, tuzinduke usingizini tunaibiwa na wakufanya hii hali ipotee ni sisi vijana wa miaka hii sababu tuna elimu, tusikubali.

Najua watu watasema mimi ni keyboard warrior ila nipo tayari. Binafsi roho yangu iondoke duniani kwajili ya taifa hili, Wakenya wametupa Somo, nafikiri wenyewe mmeona.

Vijana tuamke tunaibiwa nchi hii, wakunitafuta anitafute nipo tayari kwa lolote ila ajipange sababu maisha yote nimeishi, kama pesa ninayo na utajiri naujua upoje ila kinachoniuma kuna mijitu inaibia wananchi bila huruma na mwananchi anaishi maisha ya kimasikini na Kodi analipa tena ya hali ya juu.

TANZANIA GENERATION Z IS COMMING SOON.

====

Pia soma: Gen Z gather here: Tuko wapi mbona hatuonekani? Kenya wametuonesha njia tunaweza washughulikia kigeneration yetu!
 
Kwenye fake id 🐼
 
Hii Bongoland generation ya Insta, Tiktok, Vilevi na umalaya?

Ngoja tuone!
 
Tupo wengi Tunakuunga mkono wakati mwingine hakuna furaha ya maisha kuona watu wanaibiwa halafu hawajui ni kwa Nini ni masikini

Hebu fikiria vijana watakosa boom mwezi wa 10 kwa sababu serikari imefuja hela kwa ufisadi
 
Haya ni matumizi mabaya ya akili kumwaga damu haipaswi kuwa 1st option.
 
Wacha waibiwe mpaka akili ziwakae sawa
 
Tofauti ya Tz na Kenya...
Kenya: Taasisi, mikoa, nk..inaongozwa na watu wenye weledi kwahiyo shida inabaki Juu tu
Tanzania: sitaki kusema mchek CAG
Kwahiyo, tuanze kubadili utaratibu wa kuwapata ma DED, RC,DC nk
 
Tupo wengi Tunakuunga mkono wakati mwingine hakuna furaha ya maisha kuona watu wanaibiwa halafu hawajui ni kwa Nini ni masikini

Hebu fikiria vijana watakosa boom mwezi wa 10 kwa sababu serikari imefuja hela kwa ufisadi
Tuamke bila sisi vijana wa kiume kuamka hamna mwingine wa kuamka
 
Ujinga wa keyboard warrior unahama kutoka kwetu ma generation A na B unawaingia madogo sasa wa generation Z
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…