SoC01 Watanzania tuamke! Wenzetu wa Afrika Mashariki wanatutamani

Stories of Change - 2021 Competition

Gnyaisa

Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
23
Reaction score
24
Tanzania ni miongoni mwa nchi sita (6) zinazounda jumuiya ya Afrika Mashariki yenye nchi za Uganda, Kenya, Rwanda, Sudani ya Kusini, Burundi na Tanzania yenyewe. Eneo lote la Afrika Mashariki (ukiondoa Sudani Kusini) linakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 1,820,664 (ukubwa mara 53.7 wa taifa la Uholanzi). Zaidi ya asilimia 53 ya eneo lote la jumuiya hii ni taifa la Tanzania. Wakati Burundi ikikadiriwa kuwa na wakazi milioni 10.3, Kenya wakazi milioni 43, Rwanda wakazi milioni 12.3 na Uganda wakazi milioni 35.9 hivyo kuyafanya mataifa haya manne kwa pamoja kuwa na jumla ya wakazi milioni 100.5, Tanzania pamoja na ukubwa wa eneo lake inakadiriwa kuwa na idadi ya wakazi milioni 60 pekee na hivyo kuifanya iwe lulu kati ya mataifa wanachama (Hii ni kutokana na makadirio ya sensa za watu na makazi za nchi husika).

Jumuiya hii inajivunia maziwa makuu barani Afrika yakiwemo Viktoria, Tanganyika na Nyasa lililoko kusini mwa Tanzania. Ziwa Viktoria ambalo linaongoza kwa ukubwa barani Afrika na la pili duniani baada ya Ziwa Superior (Amerika ya Kaskazini) linamilikiwa kwa zaidi ya asillimia 50 na taifa la Tanzania huku Kenya na Uganda zikimiliki asilimia chache zinazobaki. Ziwa Tanganyika ambalo ni la kwanza barani Afrika na la pili duniani kwa kina kirefu cha maji baada ya Ziwa Baikal, linamilikiwa na Tanzania kwa zaidi ya asilimia 41 huku mataifa ya Kongo, Burundi na Zambia yakigawana asilimia chache zilizobaki.

Kwa mifano hii michache ni dhahiri kwamba wenzetu wanaounda mtangamano huu wa Afrika Mashariki wanatamani sana kuwa sehemu ya jamii kamili ya watanzania kwa lengo la kuchangamkia fursa tele tulizonazo. Mwishoni mwa mwaka 2014 serikali ya Tanzania iligoma kusaini mkataba unaohusu sera ya Ardhi ambao tayari ulikuwa umekwisha kusainiwa kwa bashasha kubwa na mataifa wanachama ya Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi! Sera hii ilikuwa inatoa ruhusa kwa raia yeyote kutoka nchi mwanachama kumiliki ardhi katika eneo lolote lililo ndani ya jumuiya. Ingawa watanzania wengi waliipongeza serikali yao kwa kutoafiki matakwa ya sera hiyo, ni wazi kwamba siku za usoni itaafikiwa hasa kutokana na malengo ya jumuiya hiyo ya kutaka kutumia sarafu moja ifikapo mwaka 2024 na hatimaye shirikisho kamili la kisiasa.

Badala ya kuendelea kulalamika na kutegemea rehema za serikali kutoridhia sera mbalimbali zenye lengo la kuunda jumuiya imara ya Afrika Mashariki, huu ni wakati muafaka kwa vijana wenzangu kuamka na kuchangamkia fursa hizi za ardhi na maji tele tulizojaliwa na Mungu.

Ukibahatika kuhudhuria makongamano au mikutano yoyote inayowaleta pamoja vijana wa nchi hizi sita za afrika mashariki utasikitika ukiwaona vijana wa Kitanzania wanavyokuwa wanyonge katika kujieleza bila sababu za msingi!

Vijana tuachane na ushabiki wa kisiasa na tujikite zaidi katika kujenga na kuimarisha uchumi wa taifa letu na wa jumuiya yetu ya Afrika Mashariki kwa ujumla. Si vibaya kijana kujihusisha na siasa za nchi lakini inapotokea wimbi kubwa la vijana waliobobea katika tasnia ya habari, fani za uhandisi, kilimo, biashara, teknolojia au ualimu kukimbilia kwenye uongozi wa kisiasa, ni wazi kutakuwa na walakini katika taifa husika!

Kwavile tumeshindwa kujitambua na kuishia kukesha tukilalamika katika mitandao ya kijamii, tayari vijana kutoka mataifa ya Kenya, Rwanda na Uganda wameanza kuingia nchini kwa njia halali na zisizo halali kisha kujichotea fursa zilizopo. Leo hii ukienda katika mahoteli mbalimbali ya kitalii chini utakutana na asilimia kubwa ya wafanyakazi wa mahoteli hayo wakiwa ni raia wa Kenya au Rwanda. Ukienda katika shule nyingi za awali, za msingi na za sekondari nchini zinazotoa elimu yake kwa kiwango cha kimataifa hutashangaa kukuta idadi kubwa ya walimu kutoka Uganda. Ukizungukia makampuni ya kupokea na kuhudumia watalii maeneo ya mbugani yamejaa wafanyakazi kutoka nchi jirani ya Kenya.

Ni ukweli usiopingika kwamba kwa miaka mingi serikali imeshindwa kuweka vipaumbele mahsusi na kujenga mazingira bora kwa vijana kuweza kujitambua na kujiajiri katika sekta mbalimbali nchini lakini bado hicho si kigezo cha vijana wengi kushindwa kuchangamkia fursa lukuki za mama Tanzania. Vijana tuamke! Wenzetu Afrika Mashariki wanatutamani.
 
Upvote 6

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ili nchi iendelee na ipate mafanikio maeneo yote inahitaji yafuatayo:-
1). watu
2). ardhi
3). siasa safi
4). uongozi bora

Kama nchi hatuna uhaba wala shida kwa namba 1 na 2..

Ila namba 3 na 4 ni majanga tupu!
 
Todays wealth is not found in things like land and such, its in KNOWLEGDE, maarifa, na hii ndio watanzania hawana, kuwa na ardhi, maji hakuwezi tu kukufanya uwe tajiri, maarifa ndio inaongoza dunia siku hizi, na watanzania wengi ELIMU BORA hawana, hio ndio tatizo namba moja
 
Vijana wanasoma kuondoa ujinga na si kupata maarifa
Sasa watashindana vipi na waliosoma na kupata maarifa
 
Back
Top Bottom