Watanzania tubadilike tulifeli pakubwa kwenye drill ya UVIKO-19

Watanzania tubadilike tulifeli pakubwa kwenye drill ya UVIKO-19

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,334
Reaction score
2,463
Yajayo yanaogyofya,

Dunia nzima mwaka 2019 ilifanya Drill ya kupima utayari wa nchi kukabiliana wa virusi. Tanzania kama mojawapo ya nchi ilipuuzia kwa kiwango kikubwa Drill hio. Hali hii inafanya watanzania kutokuwa watiifu kwa mamlaka husika endapo watapewa tahadhari juu ya ujio wa janga lingine.

Kuna viongozi waliibuka mashujaa kwa kutokutingwishwa! Nachoshauri tusiwe na haraka kupongeza wakati mchezo bado haujaisha. Huku kusua sua kwa Tanzania kwenda na wakati ni kasumba ambayo inatutafuna sana, kwanza tulikuwa nyuma kufungua uchumi wetu hali iliyotuathiri sana, sasa tena tukarudia makosa yaleyale kutokwenda na beat.

Tujiangalie sana au serikali itenge fedha kadhaa za kujiandaa kikamilifu na majanga ya namna ile.

Narudia tena yajayo yanatisha.
 
Back
Top Bottom