sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Ni kawaida sana kwa hapa nchini wanyama kuteswa, kunyanyaswa, kupigwa, n.k na hii iaonekana kawaida sana, hata kesi yake faini ni laki moja ama kifungo cha mwezi.
Hawa wanyama nao ni viumbe kama sisi licha ya tofauti tulizonazo lakini nao wana hisia, nao wanasikia maumivu, hawapendi kunyanyaswa, n.k. kama ilivyo kwetu.
Binafsi nilikuwa mshamba wa haya mambo ila mwaka jana kuna siku nilikijikuta naangalia video moja baada ya nyingine kuhusu makala za wanyama na nilielmika.
Kwa sasa paka hapa nyumbani kwangu anapewa maziwa kila asubuhi na jioni, chakula solid huwa ni dagaa ama samaki wadogo waliochemwa, kupaswa kama ni wale ambao wameshaandaliwa sokoni,n.k, pia anapenda mboga za majani.
Ana sehemu tayari ya kujisaidia akiyofundwa aitumie, hivyo si tatizo kuhofia kwamba atajisaidia ovyo
Kuhusu sehemu ya kulala pia, kila jumamosi anawekewa boksi jipya na sheet nyingine, boksi la zamani na sheet yake vinachomwa au kutupwa, hii ni kuondoa vijidudu na bacteria ili nae walau alale kwa amani.
Pia ana jina lake na likitumika anasikia, ni kumkosea heshima kumwita nyau au paka, that's too low.
Naye kwa sasa ni kama mwanafamilia ndani ya nyumba, hakuna kitu kikubwa tunachopungukiwa kwa kumjali paka wetu zaidi ya kuamini kwamba nae kaumbwa na mwenyezi Mungu kuishi katika dunia hi kama ilivyo kwetu.