Watanzania tuchangamkie fursa. Soko la mayai ni kubwa sana

Mbane

Senior Member
Joined
Jun 6, 2022
Posts
178
Reaction score
436
Habari wakuu

Nimefungua duka la kuuza mayai ya kisasa, nimegundua mayai yanahitajika sana maana mzigo unatoka mno, ila tatizo upatikanaji umekua changamoto, Tanzania tuna wafugaji wachache sana walio serious.

Kama kuna mfugaji mwenye uwezo wa kuniletea trei 500 kila baada ya siku 3 nitafute tufanye kazi. Ntakua mteja wa kudumu.
 
Na watu huwa tunapuuzia Sana biashara za mifugo Kam kuku au ng'ombe, na ndiyo biashara zinazolpa. kuku unawez ukafuga wa mayai au wa nyama ukajiingzia kipato, na ng'ombe ni wa maziwa kwa san so tuchangamkie fursa[emoji3]
 
Nilipo mayai yanazalishwa kwa wingi sana....Ofa yako ni shilingi ngap kwa trei moja?? Na unapatikana wapi??
 
Hujasema uko wapi mkuu!
 
Nilipo mayai yanazalishwa kwa wingi sana....Ofa yako ni shilingi ngap kwa trei moja?? Na unapatikana wapi??
Napatikana kitunda mkuu...! Offer ni 7500 unaniletea mpaka ofisini. Kama nafuata mwenyewe basi 7000.! Nicheki boss tufanye biashara 0654397566
 
Mayai yanazalishwa sana sema uhitaji nao ni mkubwa sana hasa viwanda, Viwanda kama vya Biskuti na vya kuoka keki vina kula mayai mno.
 
Napatikana kitunda mkuu...! Offer ni 7500 unaniletea mpaka ofisini. Kama nafuata mwenyewe basi 7000.! Nicheki boss tufanye biashara 0654397566
Angalau ingekuwa elfu 8 ningekuletea ofisini kwako...
 
Unadhani kazi ya kufuga kuku ni mchezo?

Ila ni kweli maana Tajiri wa Mo na Lake Oil wameanzisha Ufugaji wa kuku wa mayai na nyama.
 
Kufuga kuku mayai sio mchezo.....kuku 1000 kuanzia day 1 hadi anataga unaongelea 20mil in 6 months....hapo wasife zaidi 10% ili uweze kupambana kuuza mayai hela irudii ohhh chakula bei juu sanaaa mayai bei pale pale
 
Bei ya tray 1 ya mayai ni Ile ile toka mwaka juzi,huku chakula,madawa,chanjo na hata mafuta vinapanda bei kila siku 🥹😓😓😥. Leo hii tray moja ilitakiwa iuzwe elf 10 toka kwa mfugaji.
 
Maeneo ya chanika na njia ya bagamoyo kuna wazalishaji wakubwa sana hata kukupa trei 1,500 sio issue.. jaribu kuwaulizia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…