Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Wenzetu wa mataifa ya ulimwengu wa Kwanza hupigana kufa na kupona kupata kitu Bora kiwe Mali yao hata kama kiasili hakikuwa cha kwao.
Hispania iliwahi kupigana kidiplomasia ili Lionel Messi awe raia wao wapate kumtumia timu ya Taifa japokuwa ilishindikana kutokana na mapenzi ya mchezaji na hofu yake ya kupoteza asili yake. Waliendelea na mtindo huu wakafanikiwa Kwa Diego Costa.
Waingereza wamefanikiwa Kwa watu wengi Wenye vipaji kielimu au kimichezo kama walivyofanya Kwa binti wa kitanzania Pridensiana Kimiti (MBE) Mtoto wa mwanasiasa mkongwe Paulo Petro Kimiti na madaktari pamoja na wasomi kadhaa.
Kwa Muda mrefu Kenya wamekuwa walijotahidi kuidanganya dunia kwamba Mlima Kilimanjaro uko kwao Kwa vile tu ulikuwa unaweza kuingilia Kenya na ukapanda Mlima, yaani Mlima haujifichi hata ukiwa Kenya unaonekana na mtalii ameshatoka Ulaya au America amefika Kenya, hata akigundua amedanganywa lazima atimize azima yake na wakati huo Wakenya wanakuwa wameshachukua kamisheni yao maisha yanaendelea.
Mwaka Jana tumefanya Jambo kubwa Sana upande wa mchezo wa Soka. Tuligundua kuna mchezaji mzuri aliyekulia kwetu lakini si mwwnzetu.
Na Kwa vile wenzetu hawakuwa wamegundua kipaji chake basi Sisi tukawawahi na kumpa uraia. Huyu si mwingine ni KIBU DENIS PROSPER a.k.a KIBUDENGA ambaye Kwa Sasa anakiwasha na Wekundu wa Msimbazi Simba.
Jambo kama hili lisiishie Kwa Kibu pekee, vyuo vyetu vinapogundua Wachumi, Madaktari, Waandisi NK àmbao siyo ràia wawe Wazalendo kujulisha mamlaka za kielimu ili "tuibe" WATAALAMU watupe faida ambayo tusingeipata Kwa Watanzania kama tulivyofanya Kwa KIBU.