Cicero
JF-Expert Member
- Jan 20, 2016
- 2,924
- 3,074
Itifaki ya soko la pamoja la Afrika Mashariki ambayo imeridhiwa na nchi zote sita wanachama, inatoa uhuru wa wananchi (ajira), fedha, huduma na bidhaa kuhama au kuhamishwa kutoka nchi moja kwenda nyingine bila kikwazo chochote kile, na pia inatoa haki ya raia wa nchi wanachama kujenga makaazi na kuanzisha biashara bila kubughudhiwa.
Tatizo ni kwamba, kwa msisitizo wa Tanzania, kiliongezwa kipengele cha "subject to national laws" hivyo kutoa mwanya kwa nchi wanachama kuzuia baadhi ya hizi rights and freedoms kutumia vigezo (naviita visingizio) kama quality, magonjwa, usalama e.t.c. Lengo la Tanzania huenda lilikuwa ni kuweza kumonitor umiliki wa ardhi yake, which is a good thing.
Baada ya kauli ya jana ya Uhuru Kenyatta, Kenya inakuwa taifa la kwanza kwenye Jumuiya kutekeleza kikamilifu matakwa ya itifaki ya soko la pamoja. Ifahamike kwamba hatutaweza kuendelea na hatua ya sarafu ya pamoja (Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kuridhia itifaki ya umoja wa fedha) bila full implementation ya soko la pamoja. Deadline ya kuwa na sarafu moja (na kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Afrika Mashariki na Ofisi ya Takwimu ya Afrika Mashariki) ni 2024.
Baada ya kupitia maoni ya watanzania wengi juu ya kauli ya Kenyatta, nimegundua wengi hatufahamu muundo (set up) ya soko la pamoja.
Kwa mfano:
1. Kuhusu ardhi na maliasili - wengi wana hofu kwamba wageni watakuja na kunyakua ardhi ya Tanzania kiholela. Wasichokifahamu watu ni kwamba hicho kipengele cha "subject to national laws" kinaiachia Tanzania jukumu la kucontrol umiliki wa ardhi yake. Sheria za Tanzania zinasema nini kuhusu umiliki wa ardhi???
2. Kuhusu ajira na uhuru wa watu kuvuka mipaka - Kwanza kabisa watu waliopewa uhuru wa kuvuka mipaka mostly ni professionals (lawyers, doctors, teachers) etc na ndio maana kuna Mutual Recognition Agreements (MRAs) being signed between professional bodies. Pili, ajira kwenye serikali ya Tanzania zitakuwa reserved for locals, meaning kwamba wageni hawataruhusiwa kuomba au kupewa kazi serikalini. Same for wewe mtanzania ukienda kuishi Uganda/Kenya/Rwanda e.t.c