kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kama yupo anaetutakia amani na nchi yetu kwenye kipindi hiki basi atusaidie kuifanya Tume ya uchaguzi isiyumbishwe na wanasiasa wote.
Afande Sirro ni msomi sana na muelewa, Maaskofu na Masheikh ni waelewa sana, wananchi ni wapenda amani na ni waelewa sana. Makundi yote haya washirikiane kupambana na mtu yeyote yule anaeiamuru au kuishawishi Tume isiweze kufanya kazi yake ya kitaaluma, maana Tanzania ni kubwa kuliko mtu au chama cha siasa.
Mheshiwa Afande Sirro, watu wa dini na wananchi simameni nyuma ya Tanzania sio nyuma ya mtu, chama au maslahi. Tuwaache watanzania waamue nani wawe viongozi wao, tuwaache wanasiasa wakaukiwe makoo yao kwa kuwashawishi wapiga kura kwa usawa. Historia itakuja kutuhukumu vizuri au vibaya kwa matendo yetu, amani ikitoweka kwa kupigana au vikwazo tutajilaumu sana sisi wenyewe na vizazi vyetu vitatulaumu pia. Historia lazima itakuja kuandikwa kuhusu nani kasababisha nini kwasababu gani.
Viongozi wa tume hampendi historia ije iandikwe vizuri kuhusu nyinyi? Msitishwe tendendeni haki hata kama haki itawagarimu, hakuna anaeingia peponi akiwa hai.