Sitaandika mengi Leo,
Watanzania tujifunze kutoka Libya na pia tusisahau kufuatilia historia ya utajiri wa U.S.
Ila yangu ni haya,
Tusimsikilize U. S kwa lolote kwani U. S hajawai kuwa mtu mwema.
Huwa ni mtu wa ku take advantage nyakati za vita na nyakati za uchaguzi. Rejea vita ya kwanza ya dunia, vita ya pili ya dunia na vita za wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbalimbali.
lakini pia msisahau kurejea hotuba zao kile kipindi cha mwanzo wakati China anapambana na corona huku wao wakichekelea kwamba uchumi wao utaoenda kupanda kwa kasi. Na wakawaahidi China watatengeneza dawa.
Hizi ndio dili za hawa jamaa kuuza silaha wakati sisi tumekorofishana huku wao wanachukua mali zetu.
Rejea Libya tuache ushabiki wa kuwashabikia angalia kizazi chako cha mbele.
Lazima tutumie mbinu zetu wenyewe kutoka nchi zilizo jipatia maendeleo kwa njia halali. Maendeleo yaliyopatikana kwa watu kufanya kazi kwa bidii.
Zipo nchi nyingi.
Na swala la maendeleo ni vitu ni muhimu sana kwani tunahitaji miundombinu imara ili watu wawe na maendeleo.