Watanzania tujifunze kutoka Libya na pia tusisahau kufuatilia historia ya utajiri wa U.S.

Tunachohitaji Amani na Haki, upupu tu eti Gaddafi unajua sababu za kumpindua, fuateni Katiba sasa Kama unatoa onyo
CHADEMA hawawezi kuiongoza Tanzania kwasasa hilo hata watanzania wanalijua.

Labda wasubiri kwanza watafute viongozi wasomi kuanzia ngazi wabunge. Hapo wataweza ni hayo tu
 
Huko Libya ni mbali sana na wala hata huelewi kuwa ubishi na ubinafsi wa gadafi ndio ulioiponza Libya, tujifunze toka Botswana na nimibia bila kuisahau Mauritius huko kuna democracia na maendeleo ya watu.
Sisi hatuna uwezo wowote wa kushindana na mabeberu .

Hata miaka hii mitano beberu katupeleka sana tunanunua kwake ndege cash anazikamata hapo hapo,Halafu korosho yetu anaikopa
 
Kawafundishe watoto wako unaowalipia karo na kuwanunulia chakula. Hapa JF tuna akili kuliko wewe. Tutampigia kura TL.
Mkuu ww ndio TL mwenyewe hivyo huu uzi huwezi kuuelewa. Lakini hakika nakwambieni wapo watanzania walikifunza kitu kupitia uzi huu,
 
Andika tu kwa kiswahili, hautapungukiwa na kiungo hata kimoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Beberu asingekamata ndege zetu kama sio ninyi wapinzani. Kila mtanzania anajua wazi ninyi ndio chanzo cha ndege zetu kukamatwa na kuzuiliwa kwa mikopo yetu.
 
CHADEMA hawawezi kuiongoza Tanzania kwasasa hilo hata watanzania wanalijua.

Labda wasubiri kwanza watafute viongozi wasomi kuanzia ngazi wabunge. Hapo wataweza ni hayo tu
Unatakiwa kufaham kwamba umetawaliwa sio kuongozwa kwa miaka 60, lakini ukijilinganisha na maendeleo ni tofauti, kuanza upya sio ujinga waanze kufanya marekebisho kwa sehemu walizoharibu, je wamejifunza chochote zaidi ya kuwakandamiza wapinzani na kuminywa kwa haki za binadamu, hata hao marais waliopita walijifunza kuongoza, hata chadema wanaweza kujifunza, kwanini unawaza vita
 
Lissu yuko Ukerewe. Mimi niko Dar. Unatumika sana kusambaza ujinga. Kwa bahati nzuri wazee wa enzi za uhuru wanazidi kupungua. Hii story ya Libya vijana hawazielewi. Kwa nini usiongelee Zambia, Malawi, Kenya? Kwa nini Libya? Acha kuwatishia watu wazima nyau. Kama unaipenda Libya, hamia huko. nani kakukataza?
Mkuu ww ndio TL mwenyewe hivyo huu uzi huwezi kuuelewa. Lakini hakika nakwambieni wapo watanzania walikifunza kitu kupitia uzi huu,
 
U. S, BRITISH, FRANCE, hizi nchi zote zimejipatia maendelea kwa kupora mali
Hizo nchi zina maliasili kama zetu.?
Sisi tumejaliwa kila kitu kitokana na ramani aliyotupatia mkoloni.

Alafu kwani hatuwezi kuiga maendeleo ya nchi zilizoendelea bila kupora? Maana nijuavyo mimi uporaji huleta vurugu, fujo, mauaji na mambo mengi mabaya
 
Alafu Watu Weusi ni wengi kila kona ya mitaa ya majiji yao.

tafakari
Kuna historia ya black American na Black Frances jinsi walivyotokea. Wale ni zao la watumwa mkuu, ambao walikua wakichukuliwa West afrika kwenda kupiga kazi huko kipindi cha mapinduzi ya viwanda.
 
Mkuu andika hoja za kutushawishi hapa tunajifunza hatubishani
 
Kama hauoni hoja utakuwa hauna akili. Kwa nini unatoa mifano ya Libya, nchi ya Waarabu ambayo iko karibu na Ulaya na mbali sana toka Tanzania badala ya Zambia na Malawi, majirani zetu ambao wamebadili viongozi bila tatizo lolote? Ama unataka hoja gani. Naweza tu kuandika hapa. Siwezi kukuwekea hoja kwenye ubongo wako.
Mkuu andika hoja za kutushawishi hapa tunajifunza hatubishani
 
Ukisha jifunza kutoka Libya na ukisha kumbuka historia ya utajiri wa US pia usisahahu usemi usemao

"... baniani (Beberu) mbaya kiatu chake dawa ... "

Lakini pia wahenga walisema usemi usemao

"... asie fadhila hafadhiliki hata umpe tenga la samaki ..."

Kama ivo yaani picha inajieleza halafu kutwa kelele majukwaani Oooh mitano tena katujengea miundo mbinu sijui barabara, flyover sijui ushuzi gani ... unasahau hayo mnayojinadi nayo mmefadhiliwa na kupewa na haohao ambo leo mnaowaponda

Na safari hii nawaambia wamewachoka lazima mng'oke na mkilazimasha sijui mtajinadi na nini tena ...

Mxiueszzz Shuwaini kabisa!!!!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…