kluger
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 2,093
- 1,899
Naaam!
Moja kwa moja kwenye mada. Jamii yetu ya Watanzania tulio wengi tunapenda sana maneno mengi bila vitendo.
Nimekumbuka jambo hili na hatimaye kupata funzo na kukumbushwa maneno mengi bila vitendo haya lipi hata senti tano.
Hii ni baada ya pambano la masumbwi uzito wa juu WBC lililofanyika hapo jana, February 22 huko Marekani.
Pambano hilo lilikutanisha wababe wawili, Tyson Furry wa Uingereza na D. Wilder wa Marekani.
Ambapo mshindi alipatikana kwa TKO katika round ya saba kati ya kumi na mbili zilizotegemewa kuamua mbabe wa pambano.
Kabla ya pambano hili nilishuhudia mahojiano ya mabondia hawa kupitia mtandao wa YouTube.
Bondia aliyepoteza mbabe toka Marekani, kwa kweli huyu Bwana alijiamini sana, aliongea saaana, na mpaka wakati mwingine kutumia lugha ya matusi dhidi ya mpinzani wake toka Uingereza. Kwa jinsi huyu Mmarekani mweusi alivyokuwa anaongea, ni kama mtu aliyekuwa anajiamini sana kushinda.
Matokeo yake sasa, jana mtu kala kichapo kikali sana, tena pambano hili toka round ya nne, jamaa alikuwa hoi kwa kipigo. Mbaya zaidi mpinzani wake aliushughulikia zaidi ule mdomo uliokuwa unatoa maneno ya shombo, bila kusahau sikio lililokuwa halisikii onyo lake la kwamba angemcharaza kwenye mpambano huo.
Baada za mpambano huu, nilijifunza kitu, tusipende maneno mengi, dharau bila vitendo. Tusitukane mamba ingali mto hatujavuka. Ujumbe huu uwafikie wengi wa Watanzania hasa viongozi mbalimbali ambao wanapenda sana "kujimwambafai", wakumbuke huu ni mwaka wa uchaguzi Tanzania, "TUTAWACHAKAZA" kama mwenzenu kwenye picha hapo.
Tusipende sana Maneno na "tararira" nyingi bila vitendo. Jifunzeni kuwa na akiba ya maneno.
Usijiamini sana kupita kiasi, siku zote bakiza asilimia ya mashaka, hii ndiyo itakayo kuweka makini muda wote wa MAPAMBANO yako katika Maisha.
Hongera sana, TYSON FURRY, THE WORLD CHAMPION OF WBC