Watanzania tujikite kwenye uzalishaji tupunguze uchuuzi na biashara za ujanja ujanja

Kweli Kabisa Mkuu.
Binafsi swala la uchuuzi wa bidhaa sidhan kama ni ujasiriamali wa kweli.
 
Tatizo ni mifumo mibovu iliyowekwa na serikali mkulima anavuja jasho mwisho wa cku mnsmpangia bei...kiukwel Tanzania hakuna mazingira mazuri kwa mkulima tht y imekuwa ngumu sana kuwashawishi watz kujikita kwny kilimo
 
 
Mkuu sio rahisi kihivyo labda kama unaongelea Tani 3 mpaka 10.Uzalishaji wa tani 1,000 utachoma chips? Je utapata bei inayokidhi gharama za uzalishaji? au utapata bei ya hasara itakayokufanya usirudi tena shambani?
Ki ukweli serikali na wasomi wetu wanakwamisha kumkomboa mkulima kwani ndo sehemu wanaponea na wanaendelea ku-enjoy jasho la watu.Watu wakitoka ofisini wanataka wapitie fungu la nyanya la sh.200,karoti shs.200,viazi fungu Tshs.300,Pilipili Tshs.100 akiwa na buku abakize chenji akanunue mafuta na chumvi.
Hapo hapo unaambiwa na watu watakwimu gharama za chakula zinatakiwa ziwe chini zikipanda zitasababisha inflation.
Gharama za pembejeo zinaendelea kupanda hao watu watakwimu hawasemi chochote(wasomi wetu),gharama za uzalishaji zinapanda hawasemi chochote ila gharama ya chakula ndo haitakiwi kupanda!

Hakika wote tutakuwa wachuuzi tu hakuna mtu atakayekubali kupata hasara kila mwaka na kukata mtaji,tutaliwa na njaa na tutegemee kuingiza chakula toka nje.
 
[QUOTE=kombokokingachi;9517024
Mkuu Kakende sio kwamba napingana na hoja yako ila nafikiri ni vizuri tuchangamkie fursa zilizopo kama mleta uzi huu anavyotuasa. Kwa mtazamo wangu tuache kujifariji kwa kuitupia serikali lawama. Hata serikali ingetusaidia vipi kama mtu huna juhudi binafsi ya kujiongeza huwezi kufanikiwa. Vijana wenzangu tuchangamke. Wakati wa kutenda ni sasa

Mkuu siye tulishajituma ila soko hatuna naomba utusaidie kupata soko,mie nina Tani 100 za mahindi hazina soko nina tani 20 za mpunga hazina soko,kama una soko ni PM unisaidie kurudisha gharama zangu.
 
 
Kweli kwa nchi hii ku import chakula ni aibu, bonde la rufiji liko idle na rutuba yake
 

always ni kweli.wazalishaji ndio wanakuwa haraka.si wachuuzi na wauzaji.
 

uozo na rushwa au.sasa inamaana wamefika sehemu wanafanya vitu ambavyo sizani mtu mwenye akili timamu na mchumi anaweza fikiri.au hatuna wachumi nchi hii
 
Nakubaliana na wadau wote ambao wameutambua uvivu na kukosekana kujituma kwa vijana wengi wa kitanzania. Lakini niwahakikishieni kwamba maisha ya sasa yamebadili fikra za vijana wengi na fursa za kilimo zingeweza kusaidia kuinua kipato ha mtanzania lakini wanakosa vitu viwili,
1. Elimu ya kutosha kuhusu kilimo na fursa zake kiuchumi.
2. Fedha za kianzio ( uzalishaji kwa kiasi kikubwaunahitaji fedha).

Ni rai yangu kuwa tusichoke kukumbushana na kuelekezana juu ya fursa mbalimbali za kiuchumi. mabadiliko yanaanzia kwetu halafu kwa wengine pia.

Nawasilisha.
 

Wengine ndio kabisaa wanaacha vya maana wanaenda kuhatarisha maisha yao kuuza sembe wakat fursa za utajiri ziko kibao, na watanyongwa sana tu. Yan TZ watu bado wamelala tena usingizi wa kukoroma. TZ ukiwa na akili kidogo tu, unaua tembo kwa ubua, watu bado wajinga mno !! Yan na ukienda huko vijijini ndio kabisaaaaa !!! Wacha tuendelee kuokota hela wakizinduka hela zimeshaisha kitambo. LoL
 
Ni kweli kabisa kwamba mchango wa serikali katika kukiendeleza kilimo ni mdogo sana, kauri mbiu ni nyingi lakini kinachofanyika hakuna. mfano mzuri wa kumdidimiza mkulima wa Tanzania ni kuruhusu uingizwaji holela wa bidhaa za kilimo Tanzania mfano mchele mbovu toka nchi za Asia ambao huuzwa kwa bei nafuu na hivyo kuua soko la wakulima wa Tanzania ambao kulingana na gharama kubwa za uzalishaji wanashindwa kuhimili bei ya soko.
 
Mbona ni Rahisi? Kwani wakina Azam wanatumia Madalali? Zalisha Viazi process uza crips, Mihogo yako saga na uza unga.
mkuu shughuli ipo kwenye upatikanaji wa hizo mashine za kuprocess hivyo vitu au bei iko poa?
Nalog off
 

Linapokuja suala la biashara zenye faida fikirieni biashara za burdani na chakula baaaasi hiyo ni hint tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…