Watanzania tujikite kwenye uzalishaji tupunguze uchuuzi na biashara za ujanja ujanja

Watanzania tujikite kwenye uzalishaji tupunguze uchuuzi na biashara za ujanja ujanja

Kweli Kabisa Mkuu.
Binafsi swala la uchuuzi wa bidhaa sidhan kama ni ujasiriamali wa kweli.
 
Tatizo ni mifumo mibovu iliyowekwa na serikali mkulima anavuja jasho mwisho wa cku mnsmpangia bei...kiukwel Tanzania hakuna mazingira mazuri kwa mkulima tht y imekuwa ngumu sana kuwashawishi watz kujikita kwny kilimo
 
processing/manufacturing/production and the like lazima uchumi wetu utakua mzuri hii itaongeza ajira zaidi na malighafi zetu kununuliwa hapa hapa nchini

thanks for your utmost and high valued post[/

Sikuwa na nia ya kuchangia ila hii post imesababisha niseme machache.
Sio kweli vijana hawataki kuzalisha na wanapenda kufanya wanachofanya sasa ila mazingira yaliyopo kwa sasa yanakatisha tamaa.Mfano;
Mwaka juzi(2012) tulilima miwa kwa wingi Turiani tukauza kiwandani mpaka sasa hatujalipwa fedha zetu zaidi ya kuambiwa bei ya sukari imeshuka kwa sababu serikali imeingiza sukari toka nje isiyo na kodi hivyo sukari yetu haiuziki kutokana na gharama za uzalishaji.Kumbuka mtaji wetu na kipato chetu kimesimama mpaka leo,unadai zaidi ya Mil. 45 hazilipiki kila siku ahadi suala linashughulikiwa.
Tumebadilisha Kilimo tumelima mahindi mwaka 2013 tumeuzia wakala wa serikali mpaka sasa tumechoka kudai tunasubiri siku wakiamua kulipa sawa.

Kwa kweli Tanzania kuna urasimu mkubwa sana kwa uuzaji wa mazao ukilima kwa kiasi kikubwa huwezi kusafirisha vizuizi vingi pamoja na vibali,kupeleka nje hairuhusiwi unakamatwa inabakia kuishia kutapeliwa na madalali kwenye masoko yetu!Inakera sana na inaumiza sana.

Usione watu hawachangii mada kama hizi ukaona hawataki ila wanaumia kwa kinachotokea katika uzalishaji wanaoufanya.

Njoo shambani tufanye kazi ili nawe ukawasimulie wenzako kwa changamoto za soko tunazokumbana nazo.
 
Mkuu sio rahisi kihivyo labda kama unaongelea Tani 3 mpaka 10.Uzalishaji wa tani 1,000 utachoma chips? Je utapata bei inayokidhi gharama za uzalishaji? au utapata bei ya hasara itakayokufanya usirudi tena shambani?
Ki ukweli serikali na wasomi wetu wanakwamisha kumkomboa mkulima kwani ndo sehemu wanaponea na wanaendelea ku-enjoy jasho la watu.Watu wakitoka ofisini wanataka wapitie fungu la nyanya la sh.200,karoti shs.200,viazi fungu Tshs.300,Pilipili Tshs.100 akiwa na buku abakize chenji akanunue mafuta na chumvi.
Hapo hapo unaambiwa na watu watakwimu gharama za chakula zinatakiwa ziwe chini zikipanda zitasababisha inflation.
Gharama za pembejeo zinaendelea kupanda hao watu watakwimu hawasemi chochote(wasomi wetu),gharama za uzalishaji zinapanda hawasemi chochote ila gharama ya chakula ndo haitakiwi kupanda!

Hakika wote tutakuwa wachuuzi tu hakuna mtu atakayekubali kupata hasara kila mwaka na kukata mtaji,tutaliwa na njaa na tutegemee kuingiza chakula toka nje.
 
[QUOTE=kombokokingachi;9517024
Mkuu Kakende sio kwamba napingana na hoja yako ila nafikiri ni vizuri tuchangamkie fursa zilizopo kama mleta uzi huu anavyotuasa. Kwa mtazamo wangu tuache kujifariji kwa kuitupia serikali lawama. Hata serikali ingetusaidia vipi kama mtu huna juhudi binafsi ya kujiongeza huwezi kufanikiwa. Vijana wenzangu tuchangamke. Wakati wa kutenda ni sasa

Mkuu siye tulishajituma ila soko hatuna naomba utusaidie kupata soko,mie nina Tani 100 za mahindi hazina soko nina tani 20 za mpunga hazina soko,kama una soko ni PM unisaidie kurudisha gharama zangu.
 
processing/manufacturing/production and the like lazima uchumi wetu utakua mzuri hii itaongeza ajira zaidi na malighafi zetu kununuliwa hapa hapa nchini

thanks for your utmost and high valued post[/

Sikuwa na nia ya kuchangia ila hii post imesababisha niseme machache.
Sio kweli vijana hawataki kuzalisha na wanapenda kufanya wanachofanya sasa ila mazingira yaliyopo kwa sasa yanakatisha tamaa.Mfano;
Mwaka juzi(2012) tulilima miwa kwa wingi Turiani tukauza kiwandani mpaka sasa hatujalipwa fedha zetu zaidi ya kuambiwa bei ya sukari imeshuka kwa sababu serikali imeingiza sukari toka nje isiyo na kodi hivyo sukari yetu haiuziki kutokana na gharama za uzalishaji.Kumbuka mtaji wetu na kipato chetu kimesimama mpaka leo,unadai zaidi ya Mil. 45 hazilipiki kila siku ahadi suala linashughulikiwa.
Tumebadilisha Kilimo tumelima mahindi mwaka 2013 tumeuzia wakala wa serikali mpaka sasa tumechoka kudai tunasubiri siku wakiamua kulipa sawa.

Kwa kweli Tanzania kuna urasimu mkubwa sana kwa uuzaji wa mazao ukilima kwa kiasi kikubwa huwezi kusafirisha vizuizi vingi pamoja na vibali,kupeleka nje hairuhusiwi unakamatwa inabakia kuishia kutapeliwa na madalali kwenye masoko yetu!Inakera sana na inaumiza sana.

Usione watu hawachangii mada kama hizi ukaona hawataki ila wanaumia kwa kinachotokea katika uzalishaji wanaoufanya.

Njoo shambani tufanye kazi ili nawe ukawasimulie wenzako kwa changamoto za soko tunazokumbana nazo.
MILLIONS TACTICS .... kwanza you are never serious kwasababu hata quotation ya posts unayoifanya is not okay i mean unakosea na hauirekebishi kwani unayonafasi hapa jf kuomba msaada kwa fellow members au moderators

please accept and retract to normal congruent flow

naona bado unaendelea kulalama bila sababu hakuna shughuli even not for profit ambayo haina changamoto (challenge) think of SWOT analysis in a traditional way before you start business by asking yourself ? who are my customers? where did they buy before? who are my competitors? and who are my business enemies? what are the benefit of my biz? what risk is there if someone copy and paste my business, if the business is too common what else can i do? if the raw materials are not available localy how can i do? what is an expension plan .... is marketing essential? what is the utmost satisfaction of my product ... what is the my quality of my products compared to standards set? .... what is the delivery time strength? ..... are customers happy or unhappy with the services and not the product?

do i need to complain/condemn or support my business


usilalame sana crack your brain ... masoko yapo na hayajatoshelezwa na supply in a serious manner (quality and standards)

the last advice is ..... never regret when you meet a challenge (changamoto)
 
hilo ndo tatizo kubwa kwa wabongo, tumejikita kufanya uchuuzi, kuuza bidhaa za nje, na ukijaribu kumsoma aliko dangote anakuambia moja ya biashara ambazo zinaweza kukufanya uwe tajiri basi ni kazi za procesing, na si ku chuuza, huwezi ukafanya uchuuzi halafu uwe tajiri hata siku moja

always ni kweli.wazalishaji ndio wanakuwa haraka.si wachuuzi na wauzaji.
 
ndugu yangu mwakajana watu tuliwekeza kwenye kilimo mfano wilaya ya kilombero tulizalisha mpunga kiasi kikubwa sana watu wakawa wana sema sasa umaskini bai!!!!! Cha ajabu serikali ikaruhusu makampuni makubwa walete mchele toka theiland na ukafurika na wakafunga mipaka mchele wa tanzania usiuzwe nje wakati watu huko ethiopia wananjaa. Sasa mpunga umebaki umelundikana hakuna pa kupeleka watu tunalia tumekata mitaji hivi unadhani serikali hii inania njema na wakulima? Kwa hali hii bado utamshawishi mtu awekeze kwenye kilimo?

uozo na rushwa au.sasa inamaana wamefika sehemu wanafanya vitu ambavyo sizani mtu mwenye akili timamu na mchumi anaweza fikiri.au hatuna wachumi nchi hii
 
Nakubaliana na wadau wote ambao wameutambua uvivu na kukosekana kujituma kwa vijana wengi wa kitanzania. Lakini niwahakikishieni kwamba maisha ya sasa yamebadili fikra za vijana wengi na fursa za kilimo zingeweza kusaidia kuinua kipato ha mtanzania lakini wanakosa vitu viwili,
1. Elimu ya kutosha kuhusu kilimo na fursa zake kiuchumi.
2. Fedha za kianzio ( uzalishaji kwa kiasi kikubwaunahitaji fedha).

Ni rai yangu kuwa tusichoke kukumbushana na kuelekezana juu ya fursa mbalimbali za kiuchumi. mabadiliko yanaanzia kwetu halafu kwa wengine pia.

Nawasilisha.
 
Hilo Ndo Tatizo kubwa kwa Wabongo, Tumejikita kufanya uchuuzi, kuuza Bidhaa za nje, Na ukijaribu kumsoma Aliko Dangote anakuambia moja ya biashara ambazo zinaweza kukufanya uwe tajiri basi ni kazi za Procesing, na si ku chuuza, Huwezi ukafanya uchuuzi halafu uwe tajiri hata siku moja

Wengine ndio kabisaa wanaacha vya maana wanaenda kuhatarisha maisha yao kuuza sembe wakat fursa za utajiri ziko kibao, na watanyongwa sana tu. Yan TZ watu bado wamelala tena usingizi wa kukoroma. TZ ukiwa na akili kidogo tu, unaua tembo kwa ubua, watu bado wajinga mno !! Yan na ukienda huko vijijini ndio kabisaaaaa !!! Wacha tuendelee kuokota hela wakizinduka hela zimeshaisha kitambo. LoL
 
Ni kweli kabisa kwamba mchango wa serikali katika kukiendeleza kilimo ni mdogo sana, kauri mbiu ni nyingi lakini kinachofanyika hakuna. mfano mzuri wa kumdidimiza mkulima wa Tanzania ni kuruhusu uingizwaji holela wa bidhaa za kilimo Tanzania mfano mchele mbovu toka nchi za Asia ambao huuzwa kwa bei nafuu na hivyo kuua soko la wakulima wa Tanzania ambao kulingana na gharama kubwa za uzalishaji wanashindwa kuhimili bei ya soko.
 
Mbona ni Rahisi? Kwani wakina Azam wanatumia Madalali? Zalisha Viazi process uza crips, Mihogo yako saga na uza unga.
mkuu shughuli ipo kwenye upatikanaji wa hizo mashine za kuprocess hivyo vitu au bei iko poa?
Nalog off
 
Wakuu salaamu,
Kichwa cha habari kinahusika.Ukisoma kwenye kijitabu cha muongozo cha kituo cha uwekezaji Tanzania 2013-2014(Tanzania investment guide book 2013-2014) utaona kwamba nchi yetu ina maeneo mengi sana mazuri kwa ajili ya shughuli za kilimo na nyenginezo.Nanukuu toka kwenye kijitabu'

Potential irrigable
farmland in Tanzania is approximately 29
million hectares, out of which only 280,000
hectares are under irrigation farming'.

Lakini watu wengi wamejikita katika shughuli za uchukuzi,za kiujanja ujanja na utapeli mara sijui thailand mara china sijui uganda wakati Bongo hii fursa kibao.Nina uhakika kama tutaamua kuwekeza nguvu kubwa kwenye kuitumia ardhi iyo bila shaka tungekuwa mbali sana.Tatizo kubwa ni uthubutu.Tutafakari.

Linapokuja suala la biashara zenye faida fikirieni biashara za burdani na chakula baaaasi hiyo ni hint tu
 
Back
Top Bottom