Watanzania tujivunie amani tuliyonao chini ya Serikali ya CCM

Watanzania tujivunie amani tuliyonao chini ya Serikali ya CCM

Machudaa

Senior Member
Joined
Jan 22, 2018
Posts
123
Reaction score
311
Pongezi za dhati ziende kwa serikali na chama tawala toka uhuru. Amani na stability tuliyo nayo ni tunu.

Vyombo vyote vya usalama TISS, Jeshi Polisi n.k Mungu awabariki kwa kusimamia hili.

Nchi imetulia unasafiri mkoa kwa mkoa bila shida yoyote.

Msumbiji huko hakukaliki. Ethiopia sasa hivi ni Addis Ababa tu ndio kumetulia nchi imefawanyika hadi Serikali imeingilia kati kusaidia watumishi wa umma kwa kuwapa subsidies juu ya mishahara yao kwasababu haitoshi kwa kuwapa chakula vocha na mabasi ya kuwasafirisha.

Msumbiji Cabo Delgado watu wako displaced. Sudan ni shida na njaa.

Ndio kuna mapungufu ya hapa na pale lakini Serikali na CCM inajitahidi sana kusimamia amani na utulivu nchini.

Iendelee hivyo hivyo kuilinda milele amani yetu na utulivu.
 
Imani lazima iwepo, Lazima ipo hamna namna!!!
Hata wale ambao tunajidai hatuna ni waongo tuu maana tunaishi salama ndani ya dola hiihii😂😂😂
 
Imani lazima iwepo, Lazima ipo hamna namna!!!
Hata wale ambao tunajidai hatuna ni waongo tuu maana tunaishi salama ndani ya dola hiihii😂😂😂
Na katika usalama huo unapata hata nafasi ya kutafuta na kupata hata hali ikiwa ngumu. Ndio maana wageni wengi wakija wanatuonea wivu. Ni kwasababu ya serikali thabit hata kama kuna mapungufu flani
 
Hakuna amani bali watawala wametudhibiti tusipige kelele wala kusumbua wakati wa wao wakila.
Ni amani ya kushikiwa virungu na mabunduki.
Hii naweza kusema ndio tafsiri bora ya kile ambacho kinaendelea nchini!

Watu wanavumilia maumivu tu sababu kuna mitutu na virungu tayari tayari 24/7 kusubiria ambaye ataanza kujifanya anazijua sana haki zake. Refer to kilichompata Hole Anti-Pass Lissu!
 
Na katika usalama huo unapata hata nafasi ya kutafuta na kupata hata hali ikiwa ngumu. Ndio maana wageni wengi wakija wanatuonea wivu. Ni kwasababu ya serikali thabit hata kama kuna mapungufu flani

Pokea 😍😍😍
 
Hakuna amani bali watawala wametudhibiti tusipige kelele wala kusumbua wakati wa wao wakila.
Ni amani ya kushikiwa virungu na mabunduki.

Ukiona watawala wameweza kukuthibiti USIPIGE KELELE wala KUSUMBUA tambua kabisa hao watawala ni bora sana

JIPIGE KIFUA USEME MUNGU IBARIKI TANZANIA😍🇹🇿👊👍

😂😂😂😂
 
Ukiona watawala wameweza kukuthibiti USIPIGE KELELE wala KUSUMBUA tambua kabisa hao watawala ni bora sana

JIPIGE KIFUA USEME MUNGU IBARIKI TANZANIA😍🇹🇿👊👍

😂😂😂😂
Tunasemaga ujinga sawa na utajiri,nao tunazidiana! Kwahiyo naheshimu mtizamo wako.
 
Aman inayojengwa na hofu ndani yake sio nzuri maana siku hiyo hofu ikitokea wenda mambo yakawa mabaya zaid ya vile udhaniavyo
 
Tunasemaga ujinga sawa na utajiri,nao tunazidiana! Kwahiyo naheshimu mtizamo wako.

Kwakweli!
Kwa mwenye akili angeisafisha mbeleko badala ya kuichana au kuitupa maana hakuna ujinga unaozidi ule wa kuchana mbeleko iliyokubeba eti sababu tuu ni chafu ilhali huwezi kutembea wala kukaa peke yako.

Tanzania ni baba na mama tuwe wa kuisaidia zaidi ya kuharibu huku tukijua ukweli kwamba hata kama hatuishi humo kwa sasa humohumo wanaishi ndugu na jamaa zetu
 
Back
Top Bottom