Watanzania tukatae serikali Moja, Mbili au Tatu. Tupiganie REFERENDUM.

Watanzania tukatae serikali Moja, Mbili au Tatu. Tupiganie REFERENDUM.

Hakika ninayo furaha kuiona Tanganyika ikitajwa kwenye rasimu ya katiba mpya,ni ishara kubwa Tanganyika itarejea na kurejea kwake kutarejesha TANU maana Afro shiraz itarejea kwao za Zanzibar na CCM kufa kimiakimia.ooh karibu TANU uturejeshee utu wetu,uzalendo wetu,upendo wetu,aridhi yetu,madini yetu,elimu yetu na maendeleo yetu na utuondolee wanasiasa wanafiki waliosajili vyama kwa ajili ya matumbo yao na ndg zao huku wakijiita wakombozi,kumbe ni wezi wa mchana.karibu TANU,Karibu Tanganyika Uliyetuletea Uhuru wetu.

Hilo ndio CCM hawalitaki maana ukiuwa muungano na yenyewe inakufa....hail TANGANYIKA you all!

COA_Tanganyika_1.jpg
 
tatizo sio kuvunja muungano. bali ni namna ya kuuvunja tuna madeni ya taifa, tuna mipango ya maendeleo ya muda mrefu na sasa ina zaidi ya miaka 20 na inaendelea, kutakuwa na mabadiliko ya majengo ya mabalozi nchi zote m kiti cha umoja wa mataifa vitatakiwa viwili, kuna fungu benki kuu la kugawana na kugawana majeshi na polisi walioko kwenye ajira moja ya muungano yenye pension namafao tofauti. NADHANI KINACHOWATESA NI NAMNA YA KUUVUNJA SIO KUSEMA TU NENO TUVUNJE AU KURA ZA WANANCHI SIO TATIZO. pia na suala la kiusalama hawa wenzetu znz wanaweza kugeuka somalia tukapata maumivu kama wanayoyapata kenya.

Wandugu mchana mwema; Mfano mwingine TALAKA... Mke akingangania talaka na kumburuza Mumewe kwa wahusika, itabidi mume atoe talaka na asiulize we mama watoto wangu utaenda wapi na kuiishi na nani? talaka ikitolewa tu hapo hayamhusu mume tena. huyo ex-mke atajua lake na maisha yake (kumradhi/hashakum awe kahaba au jambazi au gaidi au Barmedi nk,) Kwa hiyo haijalishi awe kama Somaliya au Iraki au Afghanistan !! Sasa hapo ndo tatizo letu Vile Mume atabeba tija na matokeo yote ya mustakabali ( yaani kutunza watoto na kulipia madeni yote) Wakuu Jambo hili ni la kujikamua na kulitafakari kiutu uzima. siyo kufuata mahanjamu na presha la viongozi njaa na wasiyo na misimamo. tukubali
kupoteza machache ili tuokoe shehena kubwa la jahazi. LONG LIVE TANZANIA.
 
Hakika ninayo furaha kuiona Tanganyika ikitajwa kwenye rasimu ya katiba mpya,ni ishara kubwa Tanganyika itarejea na kurejea kwake kutarejesha TANU maana Afro shiraz itarejea kwao za Zanzibar na CCM kufa kimiakimia.ooh karibu TANU uturejeshee utu wetu,uzalendo wetu,upendo wetu,aridhi yetu,madini yetu,elimu yetu na maendeleo yetu na utuondolee wanasiasa wanafiki waliosajili vyama kwa ajili ya matumbo yao na ndg zao huku wakijiita wakombozi,kumbe ni wezi wa mchana.karibu TANU,Karibu Tanganyika Uliyetuletea Uhuru wetu.

Mkuu turudishe na ile kauli mbiu yetu ya "UHURU! KAZI YA TANU"
 
Hilo ndio CCM hawalitaki maana ukiuwa muungano na yenyewe inakufa....hail TANGANYIKA you all!

quote_icon.png
By kimboka one
Hakika ninayo furaha kuiona Tanganyika ikitajwa kwenye rasimu ya katiba mpya,ni ishara kubwa Tanganyika itarejea na kurejea kwake kutarejesha TANU maana Afro shiraz itarejea kwao za Zanzibar na CCM kufa kimiakimia.ooh karibu TANU uturejeshee utu wetu,uzalendo wetu,upendo wetu,aridhi yetu,madini yetu,elimu yetu na maendeleo yetu na utuondolee wanasiasa wanafiki waliosajili vyama kwa ajili ya matumbo yao na ndg zao huku wakijiita wakombozi,kumbe ni wezi wa mchana.karibu TANU,Karibu Tanganyika Uliyetuletea Uhuru wetu.

COA_Tanganyika_1.jpg
Mkuu naheshimu hisia zako na maoni yako fika, Lakini nachokijua mie kuwa " Zama (zamani) hairudi nyuma "
Sidhani kama TIME inajirejesha awali nyuma.
kama upo uhai Tupo tutona.
 
Yaani hapa tumeshachanganywa na kukorogwa, hatujui hata kusini au kaskazini ni wapi! Mara wengine wanaikubali, mara wengine sio yote, mara wengine sijui nini... I don't see how we are going to get organized in this f***n business...

Kwa vyovyote vile, kama wataendelea kung'ang'ania hili limuungano lao, 2014 rasimu inapigwa chini kwenye kura ya maoni... wakilirudisha tena, tunaipiga chini tena... eeh, tuone watafanya nini. Sijui wataamua kutagaza kuwa mchakato wa katiba umeahirishwa hadi tutakapotangaziwa tena?!!!

Maana watu wanajitia kuwasemea watanzania kuwa tunapenda muungano!!! Nani kasema?

Ndiyo yale yale ya tume ya Nyalali kuuliza wananchi kama wanataka kuendelea na mfumo wa chama kimoja au la wakati wanafahamu kabisa wananchi wengi hawana mwamko wa kisiasa na aina za mifumo mbalimbali utawala ikichukuliwa CCM ilikuwa imeshika hatamu za uongozi. Tume ya Nyalali ilifahamu jibu hata kabla ya kwenda kuwahoji wananchi.

Leo wananchi wana mwamko wa kisiasa, wanasiasa wetu kwa kujua hivyo, waliamua kuwekwa kufuli kwenye swala la muungano ndani ya hadidu za rejea kitu ambacho kimewanyima wananchi uhuru wao katika maamuzi ya mstakabali wa nchi yao.
 
Serikali ziwe mbili. Ya Tanganyika, na ya Zanzibar... Bora tuanze upya...
Kukata mzizi wa fitina, watupe hii kura ya referendum tujue moja na kila mmoja arudi majumbani kwake akijua wananchi wengi wanataka nini.

Hii ndiyo maana ya demokrasia yenye mipaka iliyowazi.
 
Mkuu naheshimu hisia zako na maoni yako fika, Lakini nachokijua mie kuwa " Zama (zamani) hairudi nyuma "
Sidhani kama TIME inajirejesha awali nyuma.
kama upo uhai Tupo tutona.

Kaka hata RUSSIA ilimezwa na USSR kwa miaka 80 (1917-1991) bila ridhaa ya wananchi wake na hatimaye ikarudi na bado ipo na USSR is gone.......forever hopefully

Ewe mola tunakuomba
Uibariki nchi yetu
Tanganyika na jirani zetu
Eee Mola

Salum Abdallah Yazid and Cuban Marimba Band- 1961
 
umegusia ukweli japo ni kidogo mkuu, dudu muungano tukiling'ang'ania madhala yake yanaweza kuwa mabaya siku za usoni! tunaweza zalisha vikundi vya upigania uhuru, tuwe tayari kushuhudia mabomu yakilipuliwa, kwa kutumia charisma! madhala ya kutotaka kuongelea muungano yanaweza kuwa mabaya na makubwa!

kwa upande wa CCM wanawakalilisha vijana wao kuwa muungano uliopo unafaa, pasi kuangalia viashiria tulivyoanza kuvishuhudia! vijana wanacopy ideal za zamaani saana! nimemsikia kijana mmoja kwenye tv akichemka!

suala wanalotetea wale wanaopenda mfumo wa sasa uendelee ati ni ghalama za uendeshaji wa serikali itakuwa kubwa, they dont state upande gani utazidiwa na ghalama! kwa upande wa tanganyika kwa mtazamo wangu ghalama zitapungua tuu! hebu fikiria watanganyika tumekopa mpaka mawaziri kwa wenzetu! kwa ghalama zetu, achiambali mlalahoi wa bara kumlipia umeme wenzetu! tena wengine wenye uwezo! hebu tuangalie kwakina hoja zetu!
 
Kitu cha kushangaza ni kuona kuwa vyama vyetu vya siasa pamoja na asasi zimerukia hii bandwagon ya serikali tatu kana kwamba huu ndiyo muarobaini wa matatizo ya muungano wakati kiini cha tatizo na mazingira ya kisiasa kwa sasa hayawezi kutatuliwa na kuwepo kwa serikali tatu achilia mbali gharama za kuziendesha.

Wanasiasa wetu wameamua kuwa non-committal kwa kujificha kwenye hadidu za rejea zilizoainisha misingi muhimu ya kuzingatia kana kwamba hayo yalikuwa ni makubaliano na wananchi wengi.
 
Kijana haujatafakari vizuri bali umekalili nani aliwahi kusema nini. tunachotaka wewe utushawishi nacho ni hoja yako ya referendum ina faida gani ukilinganisha na hoja iliyoletwa mbele yetu. Maana naamini muungano wa wazazi wako uliukuta hata kama baba na mama wanagombana kila siku huwezi kuja mtoto kuitisha referendum ya kujadili muungano wa wazazi wako. hii ni kwa sababu muungano unafaida kuliko matatizo yanayojitokeza ndani yake ambayo yanaweza kujadiliwa na kutatuliwa. naamini watanzania wote tutasapoti maboresho ya muungano labda anayetaka kutushawishi aje na hoja za kutuambia tunapata hasara gani ndani ya muungano ambazo tunaweza kuzieupuka nje ya muungano na alinganishe na faida tunazozipata ndani ya muungano ili tuangalie uzito mkubwa uko wapi. muungano si wa mtu au kundi Fulani bali muungano ni wa watanzania hivyo tushawishiwe kwa hoja zinazochambua watanzania sio kundi Fulani lilikuwa hivi au mtu Fulani alisema hivi.

Hapo ndugu yangu si kweli umelinganisha vitu ambavyo kwa namna yoyote hailingani kabisa. Unaweza kuwa na point lakini mifano ikakupoteza hivyo hata poiny yako ikawa ni pointless. Jaribu kutafuta mifano mingine lakini siyo huo. Baba na mama ni wazazi Muungano si mzazi. Baba au mama au wote wakifariki mtoto anaitwa yatima mbona Russia haiitwi yatima baada ya muungano kufa na maisha yanasonga mbele? "Si kila unachofikiri ukiseme bali kila unachosema ufirkiri"
 
Mm nahisi watanganyika wanaona aibu kuirejesha tanganyika yao,mbona kule zanzibar wanajinasibu kwa zanzibar yao sio zanzibar pekee yenye kujinasibu bali pia kenya,italiy,rwanda wanajinasibu kwa utaifa wao,tanzania ni jina la mpito tu lakini asili yenu ni watanganyika tu,mkataa kwao mtumwa.
 
Hoja imepita, wanokubali sema ndiyooooooooooooooooo, wanokataa sema siyoooooooooooooooooooooo
 
Walivunja azimio la Arusha ambalo lilikuwa na impact kubwa kwa mstakabali wa taifa letu, wanashindwaje kuvunja muungano ambao hata faida yake haionekani. Nchi zilizokuwa nchi moja hapo zamani kama Ethiopia na Eritrea, Sudan na Sudan kusini, zinatengana, iwe ajabu kwetu ambaye unaunganishwa na nchi mbili huru?

Naiona Tanzania Kusini na Tanzania Kaskazini zinakuja kwa mbaaaaaali!
 
Muamerika aitwaye H.P. Lovecraft aliwahi kusema, The oldest and strongest emotions of humankind is fear, and the oldest and strongest kind of fear is fear of the unknow.

Sisi hatutakuwa wa kwanza katika dunia hii na kuna mifano ambayo pamoja na muungano kuvunjika, nchi zimeweza kupiga hatua mbele za kimaendeleo. Nchi nyingi za ulaya ya mashariki ziliweza kuachana na zimeweza kusonga mbele.

Kibaya zaidi, muungano umekuwa kama ni siri ambaye wananchi wa kawaida hawatakiwi kuuchimba ili kuufahamu kwa undani zaidi ya kupata dodoso za hapa na pale kutoka kwa wanazuoni mbali mbali.

Kwa nini sisi tuwe tofauti na nchi zilizofanikiwa baada ya kuachana na muungano.

Tatizo liko hapo kwenye namna ya kuuvunja. tukiwaambia znz kuwa katika deni la taifa tulilonalo mfano tirioni 300 nyie mtatakiwa kulipa tirioni 50 hiyo pekee inatosha kuanzisha vurugu kati ya tanganyika na znz kama ilivyo kwa hizo nchi za sudan na sudan kusini, hao wanajeshi tutakao gawana ni wengi sana tangu vijana walioko sasa mpaka wazee wa miaka 80 au 70 bado wako kwenye muungano kwa vyovyote znz haitaweza kuwalipa kama walivyolipwa kwenye muungano nini kitatokea?kumbuka znz hakuna chochote cha kuingiza pesa zaidi ya utalii,bandari na vikarafuu ambapo. waznz wanaakili za kiarabu wanacholilia kikubwa tu ni kujiunga oic na kuwa moja ya nchi huru za kiislam hiyo ndio hoja yao kuu sasa watu hawa ni wakuangalia sana, nigeria walilia hivyo hivyo kujitenga walipojitenga bado wanalazimisha viongozi wote wa serikali wawe waislam, yaani ni watu wakulalamika tu na vurugu bila vita hawana raha, sasa watu hawa wanacholilia kujitenga nini kama ni gesi tanganyika in a gesi ya kusambaza africa mashariki na kati kwa muda mrefu kama ni uranium ipo nyingi tanganyika. hawa watu wanataka kutuletea matatizo tu, wengine wana viramani feki wanasema 10km za dar ni ardhi yao na ndivyo wanavyoamini
 
Tatizo hiyo referendum haimo kwenye hadidu rejea za rasimu iliyotangazwa.

Kingine kinachonitatiza ni juu ya uelewa wa wananchi juu ya maana halisi ya serikali,muundo wake na namna yake ya uajibikaji. Pengine sawa serikali tatu,je nini taswira kimataifa?

Binafsi ningefikiri labda tungepiga hatua nyingine ya nchi mbili hizi kuungana moja kwa moja kupata nchi moja kubwa yenye nguvu ya ushawishi wa kiuchumi.Na hii ingekuwa vema hata kwa majirani zetu wajifunze ili ile azma ya kuelekea EAC na AU iweze kufanikiwa.
Kiukweli serikali tatu italeta mgongano si tu wa kimaslahi bali hata ule wa kihitifaki katika siasa za afrika na dunia.
 
Back
Top Bottom